< Malaki 2 >

1 Sasa, ninyi makuhani, amri hii ni kwa ajili yenu. 2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtalichukua hili mioyoni mwenu na kunipa utukufu kwa jina langu, “asema Bwana wa Majeshi, Kisha nitatuma laana kwenu, na nitalaani baraka zenu. Kiukweli, nilishawalaani tayari, kwa sababu hujaweka sheria zangu moyoni. 3 Tazama, nitakikemea kizazi chako, na nitapaka mavi juu ya uso wako, mavi ya dhabihu zenu, na mtachukuliwa pamoja nayo. 4 Na mtajua kwamba nimetuma hii sheria kwenu, kwamba agano langu litakuwa ni juu yangu na Lawi,” asema Bwana wa Majeshi. 5 Agano langu na yeye lilikuwa agano la uhai na amani, na nilimpa vitu hivi kama njia ya kuniheshimu. aliniheshima na alisimama akawa na hofu kwa jina langu. 6 Mafundisho ya kweli yalikuwa kwenye kinywa chake, na uovu haukupatikana kinywani mwake. Alitembea na mimi kwa amani na unyoofu, na aliwarudisha wengi kutoka dhambini. 7 kwa sababu midomo ya makuhani huhifadhi maarifa, na watu watatafuta maagizo kutoka kwenye kichwa chake, kwa sababu ni mjumbe wa Bwana wa Majeshi. 8 lakini umepita mbali na njia ya kweli. Umesababisha wengi kuwa na mashaka ya kutii sheria. umeliharifu agano la Lawi,” asema Bwana wa Majeshi. 9 Kwa hiyo nimewafanya ninyi nanyi kudharauliwa mbele ya watu, kwa sababu hamkutunza njia zangu, lakini badala yake mnapendelea katika maagizo yenu. 10 Sisi sote hatuna baba mmoja? Siyo Mungu yule mmoja aliyetuumba sote? kwa nini tunafanyiana hila kila mtu na ndugu yake, mnariharibu agano la baba zetu? 11 Yuda amefanya hila na ameona kinyaa kwa vitu vilivyowekwa katika Israeli na Yerusalem. Yuda amenajisi mahali patakatifu pa Bwana ambapo anapapenda, na ameoa binti wa miungu migeni. 12 Mungu akukatilie mbali kutoka kwenye hema ya Yakobo na uzao wa mtu aliyefanya haya, hata yule anayeleta sadaka kwa Bwana wa Majeshi. 13 Na wewe pia fanya hivyo. Unafunika madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kilio na kuugua, kwa sababu hatakubali sadaka na kuzipokea kutoka mikononi mwako. 14 Lakini wasema, ni kwa sababu gani?” Kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati yako wewe na mke wako wa ujana wako, kinyume chake umekuwa si mwaminifu, ingawa yeye ni mwenzako na mke wa agano lako. 15 Je yeye hakuwafanya kuwa mmoja, hata kwa sehemu ya roho yake? Sasa ni kwanini aliwafanya ninyi kuwa mmoja? Kwa sababu alikuwa anategemea kupata watoto wacha Mungu. Kwa hiyo jiepushe mwenyewe ndani ya moyo wako, na asiwepo mtu asiye mwaminifu kwa mke wa ujana wake. 16 “Nakuchukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israel, “afunikizaye nguo yake kwa udhalimu,” asema Bwana wa Majeshi. “Kwa hiyo jilinde ewe mwenyewe ndani ya roho yako na usiwe mtu asiye mwaminifu.” 17 Mmechosha Bwana na maneno. Lakini mwasema, “Tumekuchoshaje?” Kwa kusema Kila mmoja aliyefanya uovu ni mzuri kwa upande wa Bwana, na anafuraha nao;” au “Yuko wapi Mungu wa Haki?”

< Malaki 2 >