< Luka 7 >

1 Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu. 2 Mtumwa fulani wa akida, aliyekuwa wa thamani sana kwake, alikuwa mgonjwa sana na alikuwa karibu ya kufa. 3 Lakini akiwa amesikia kuhusu Yesu, yule Akida alimtuma kiongozi wa kiyahudi, kumwomba aje kumwokoa mtumwa wake ili asife. 4 Walipofika karibu na Yesu, walimsihi kwa bidii na kusema, “anastahili kwamba unapaswa kufanya hivi kwa ajili yake, 5 kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu”. 6 Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. “Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu. 7 Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona. 8 Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu “Nenda” na huenda, na kwa mwingine, “Njoo” naye huja, na kwa mtumishi wangu 'Fanya hiki', na yeye hufanya”. 9 Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema.”Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu. 10 Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima. 11 fulani baada ya haya, ilitokea kuwa Yesu alikuwa anasafiri kwenda mji ulioitwa Naini. wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambana na umati wa watu. 12 Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye. 13 Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie”. 14 Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka” 15 Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake. 16 Kisha hofu ikawajaa wote. wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema “Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu” na “Mungu amewaangalia watu wake” 17 Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani. 18 Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote. 19 Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie? 20 Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, 'Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?” 21 kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona. 22 Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema. 23 Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa”. 24 Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo? 25 lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme. 26 lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii. 27 Huyu ndiye aliyeandikiwa, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu, 28 Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.” 29 Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye Haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana. 30 Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe. 31 Tena naweza kuwalinganisha na nini watu wa kizazi hiki? Wakoje hasai? 32 Wanafanana na watoto wanaocheza kwenye eneo la soko, wanaokaa na kuitana mmoja baada wa mwingine wakisema, 'Tumepuliza filimbi kwa ajili yenu, na hamkucheza. tumeomboleza na hamkulia.' 33 Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema “Ana pepo. 34 Mwana wa Mtu amekuja amekula na kunywa na mkasema, “Angali ni mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! 35 Lakini hekima imetambulika kuwa ina haki kwa watoto wake wote.” 36 Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale. 37 Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato. 38 Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato. 39 Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. 40 Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia. “Akasema” “Kiseme tu mwalimu!” 41 Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini. 42 Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi? 43 Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.”Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.” 44 Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake. 45 Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu. 46 Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato. 47 Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.” 48 Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa” 49 Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?” 50 Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani”

< Luka 7 >