< Luka 5 >

1 Basi ilitokea wakati watu walipomkusanyikia na kumzunguka Yesu na kusikiliza neno la Mungu, ambapo alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti.
Siku moja Yesu alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti, watu wengi wakiwa wanasongana kumzunguka ili wapate kusikia neno la Mungu,
2 Aliona mashua mbili zimetia nanga pembeni mwa ziwa. Wavuvi walikuwa wametoka na walikuwa wakiosha nyavu zao.
akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao.
3 Yesu akaingia katika mojawapo ya zile mashua, ambayo ilikuwa ya Simoni na kumwomba aipeleke majini mbali kidogo na nchi kavu. Kisha akakaa na kufundisha kutokea kwenye mashua.
Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.
4 kuongea, akamwambia Simoni, “Ipeleke mashua yako mpaka kwenye kilindi cha maji nakushusha nyavu zako ili kuvua samaki.”
Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, “Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki.”
5 Simon akajibu na kusema, Bwana, tumefanya kazi usiku wote, na hatukukamata chochote, lakini kwa neno lako, nitazishusha nyavu.
Simoni akamjibu, “Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu.”
6 Walipofanya hivyo walikusanya kiasi kikubwa cha samaki na nyavu zao zikaanza kukatika.
Nao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika.
7 Hivyo wakawaashiria washirika wao kwenye mashua nyingine ili waja na kuwasaidia. Walikuja wakazijaza mashua zote, kiasi kwamba zikaanza kuzama.
Wakawaashiria wavuvi wenzao kwenye ile mashua nyingine ili waje kuwasaidia. Wakaja, wakajaza mashua zote mbili samaki hata zikaanza kuzama.
8 Lakini Simoni Petro, alipoona hivyo, alianguka magotini pa Yesu akisema,”Ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi Bwana.”
Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni mwa Yesu na kumwambia, “Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!”
9 Kwa sababu alishangazwa, na wote waliokuwa pamoja naye, kwa uvuvi wa samaki waliokuwa wameufanya.
Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wameshangazwa sana na wingi wa samaki waliokuwa wamepata.
10 Hili liliwajumuisha Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo, ambao walikuwa washirika wa Simoni. Na Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea utavua watu.”
Vivyo hivyo wenzake Simoni, yaani Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walishangazwa pia. Ndipo Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu.”
11 Walipokwishazileta mashua zao nchi kavu, waliacha kila kitu na kumfuata yeye.
Hivyo wakasogeza mashua zao mpaka ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata.
12 Ilitokea kwamba alipokuwa katika mji mmojawapo, mtu aliyekuwa amejaa ukoma alikuwa huko. Wakati alipomuona Yesu, alianguka akiinamisha uso kwake mpaka chini na kumuomba, akisema, “Bwana, ikiwa unataka, waweza kunitakasa.”
Ikawa siku moja Yesu alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Yesu, alianguka chini mpaka uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.”
13 Kisha Yesu alinyoosha mkono wake na kumgusa, akisema, “Nataka. Takasika.” Na saa ileile ukoma ukamwacha.
Yesu akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Na mara ukoma wake ukatakasika.
14 “Alimwagiza asimwambie mtu yeyote, lakini alimwambia, “Nenda zako, na ukajionyeshe kwa makuhani na utoe sadaka ya utakaso wako, sawasawa na kile Musa alichokiamuru, kwa ushuhuda kwao.”
Yesu akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu yeyote, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”
15 Lakini habari kumuhusu yeye zikaenea mbali zaidi, na umati mkubwa wa watu ukaja pamoja kumsikiliza akifundisha na kuponywa magonjwa yao.
Lakini habari zake Yesu zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
16 Lakini mara kwa mara alijitenga faraghani na kuomba.
Lakini mara kwa mara Yesu alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba.
17 Ilitokea siku moja kati ya hizo siku alikuwa akifundisha, na walikuwapo Mafarisayo na waalimu wa sheria wamekaa hapo ambao walikuja wakitokea vijiji vingi tofauti katika mkoa wa Galilaya na Yudea, na pia kutokea katika mji wa Yerusalemu. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kuponya.
Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na walimu wa sheria, waliokuwa wametoka kila kijiji cha Galilaya na kutoka Uyahudi na Yerusalemu, walikuwa wameketi huko. Nao uweza wa Bwana ulikuwa juu yake kuponya wagonjwa.
18 watu kadhaa walikuja, wamembeba kwenye mkeka mtu aliyepooza, na wakatafuta njia ya kumwingiza ndani ili kumlaza chini mbele ya Yesu.
Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Yesu.
19 Hawakupata njia ya kumwingiza ndani kwa sababu ya umati, hivyo walipanda juu ya paa la nyumba na kumshusha yule mtu chini kupitia kwenye vigae, juu mkeka wake katikati ya watu, mbele kabisa ya Yesu.
Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya matofali, wakamteremsha yule mgonjwa kwa mkeka wake hadi katikati ya ule umati pale mbele ya Yesu.
20 Akiangalia imani yao, Yesu alisema, “Rafiki, dhambi zako umesamehewa.”
Yesu alipoiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Rafiki, dhambi zako zimesamehewa.”
21 Waandishi na Mafarisayo waliaanza kuhoji hilo, wakisema, “Huyu ni nani anayeongea makufuru? Ni nani anaweza kusamehe dhambi ila Mungu pekee yake?”
Mafarisayo na wale walimu wa sheria wakaanza kuuliza, “Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”
22 Lakini Yesu, akitambua nini walichokuwa wakifikiri, aliwajibu na kuwaambia, “Kwa nini mnaulizana hili mioyoni mwenu?
Yesu akijua mawazo yao akawauliza, “Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu?
23 Kipi ni rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama utembee?'
Je, ni lipi lililo rahisi zaidi, kumwambia, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’?
24 Lakini mjue ya kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi, Nakwambia wewe, 'Amka, chukua mkeka wako na uende nyumbani kwako.'”
Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.”
25 Wakati huo huo akaamka mbele yao na akachukua mkeka wake aliokuwa ameulalia. Kisha akariudi nyumbani kwake akimtukuza Mungu.
Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake, akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu.
26 Kila mmoja alishangazwa na wakamtukuza Mungu. Walijawa na hofu, wakisema, “Tumeona mambo yasiyo ya kawaida leo.”
Kila mmoja akashangaa na kumtukuza Mungu. Wakajawa na hofu ya Mungu, wakasema, “Leo tumeona mambo ya ajabu.”
27 Baada ya mambo haya kutokea, Yesu alitoka huko na akamwona mtoza ushuru aliyeitwa Lawi amekaa eneo la kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate.”
Baada ya haya, Yesu alitoka na kumwona mtoza ushuru mmoja jina lake Lawi akiwa amekaa forodhani, mahali pake pa kutoza ushuru. Akamwambia, “Nifuate.”
28 Hivyo Lawi akanyanyuka na kumfuata, akiacha kila kitu nyuma.
Naye Lawi akaacha kila kitu, akaondoka, akamfuata.
29 Kisha Lawi akaandaa nyumbani kwake karamu kubwa kwa ajili ya Yesu. Walikuwapo watozaushuru wengi kule na watu wengi walioketi mezani wakila pamoja nao.
Kisha Lawi akamfanyia Yesu karamu kubwa nyumbani kwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao.
30 Lakini Mafarisayo na waandishi wao walikuwa wakiwanung'unikia wanafunzi, wakisema, “Kwa nini mnakula na kunywa na watoza ushuru pamoja na watu wengine wenye dhambi?”
Lakini Mafarisayo na walimu wa sheria waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”
31 Yesu akawajibu, “Watu walio katika afya njema hawahitaji tabibu, ni wale tu wanaoumwa ndiyo watakao mhitaji mmoja.
Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa.
32 Sikuja kuwaita watu wenye haki haki wapate kutubu, bali kuwaita wenye dhambi wapate kutubu.”
Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.”
33 Wakamwambia, “Wanafunzi wa Yohana mara nyingi hufunga na kuomba, na wanafunzi wa Mafarisayo nao hufanya vivyo hivyo. Lakini wanafunzi wako hula na kunywa.”
Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”
34 Yesu akawaambia, “Inawezekana mtu yeyote akawafanya waliohudhuria harusi ya Bwana Arusi kufunga wakati Bwana Arusi bado yu pamoja nao?
Yesu akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao?
35 Lakini siku zitakuja wakati Bwana Arusi atakapoondolewa kwao, ndipo katika siku hizo watafunga.”
Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo watakapofunga.”
36 Kisha Yesu aliongea pia kwao kwa mfano. “Hakuna anayechana kipande cha nguo kutoka kwenye vazi jipya na kukitumia kurekebisha vazi la zamani. Kama akifanya hivyo, ataichana nguo mpya, na kipande cha nguo kutoka vazi jipya kisengefaa kutumika na nguo ya vazi la zamani.
Yesu akawapa mfano huu, akawaambia: “Hakuna mtu achanaye kiraka kutoka kwenye nguo mpya na kukishonea kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, atakuwa amechana nguo mpya, na kile kiraka hakitalingana na ile nguo iliyochakaa.
37 pia, hakuna mtu ambaye huweka divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai mpya ingepasua kile chombo, na divai ingemwagika, na viriba vingeharibika.
Hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo yote itamwagika.
38 Lakini divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya.
Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya.
39 Na hakuna mtu baada ya kunywa divai ya zamani, hutataka mpya, kwa sababu husema, 'Ya zamani ni bora.”'
Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, bali husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’”

< Luka 5 >