< Luka 17 >

1 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, Lakini ole wake mtu anayeyasababisha! 2 Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi. 3 Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe. 4 Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, 'ninatubu,' msamehe!” 5 Mitume wake wakamwambia Bwana, “tuongezee imani yetu.” 6 Bwana akasema, “kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, 'n'goka na ukaote baharini,' nao ungewatii. 7 Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, 'Njoo haraka na keti ule chakula? 8 Je hatamwambia, 'Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa? 9 Hata mshukuru mtumishi huyo kwasababu katimiza yale aliyoamriwa? 10 Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni 'Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.' 11 Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya. 12 Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali 13 wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.” 14 Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika. 15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu. 16 Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria. 17 Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?” 19 Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.” 20 Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana. 21 Wala watu hawatasema, 'Angalia hapa!' au, 'Angalia kule!' kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” 22 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. 23 Watawaambia, 'Angalia, kule! Angalia, hapa!' Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuafata, 24 kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake. 25 Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki. 26 Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokua katika siku ya Mwana wa Adam. 27 Walikula, walikunywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile ambayo Nuhu alipoingia katika safina na gharika ikaja na kuwaangamiza wote. 28 Ndivyo ilivyokua katika siku za Lutu, walikula, kunywa, wakinunua na kuuza, kulima na walijenga. 29 Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ikawaangamiza wote. 30 Hivyo ndivyo itakavyo kuwa siku ile ya Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. 31 Siku hiyo, usimruhusu aliye kwenye dari ya nyumba ashuke kuchukue bidhaa zake ndani ya nyumba. Na usimruhusu aliyeko shambani kurudi nyumbani. 32 Mkumbuke mke wa Lutu. 33 Ye yote anaejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa. 34 Nakwambia, usiku huo kutakua na watu wawili katika kitanda kimoja. Mmoja atachukuliwa, na mwingine ataachwa. 35 Kutakua na wanawake wawili wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” 36 37 Wakamwuliza, “Wapi, Mungu?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai hukusanyika kwa pamoja.”

< Luka 17 >