< Luka 10 >

1 Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake. 3 Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. 4 Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani. 5 Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, 'Amani iwe katika nyumba hii.' 6 kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu. 7 Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine. 8 Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu, 9 na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, 'Ufalme wa Mungu umekuja karibu yanu' 10 Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni, 11 'Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.' 12 Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahamilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo. 13 Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, Wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu. 14 Lakini itakuwa usitahamilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu. 15 Wewe Kapernaumu, Unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu (Hadēs g86) 16 Atakaye wasikiliza ninyi anisikiliza mimi, na yeyote atakaye wakataa anikataa mimi, na yeyote anikataaye mimi anmtakaa aliyenituma” 17 Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.” 18 Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi. 19 Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru. 20 Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.” 21 Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.” 22 “Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.” 23 Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona. 24 Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.” 25 Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?” (aiōnios g166) 26 Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?” 27 Akajibu akasema, “Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.” 28 Yesu akasema, “Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi.” 29 Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, Akamwambia Yesu, “Na jirani yangu ni nani?” 30 Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu akiwa nusu mfu. 31 Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine. 32 Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine. 33 Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. alipomuona, alisukumwa kwa huruma. 34 Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia. 35 Siku ilyofuata alichukua dinari mbili, na akampatia mmiliki wa nyumba ya wageni na kumwambia, 'Muhudumie na chochote cha ziada utakacho tumia, nitakulipa nitakaporudi.' 36 Ni yupi kati ya hawa watatu, unafikiri, alikuwa ni jirani kwake yeye aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?” 37 Mwalimu alisema, “Ni yule aliyeonesha huruma kwake.” Yesu akamwambia, “Nenda na ukafanye vivyo hivyo” 38 Sasa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake. 39 Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake. 40 Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, “Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie.” 41 Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, “Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi, 42 lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake.”

< Luka 10 >