< Mambo ya Walawi 2 >

1 Yeyote akitoa sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake lazima iwe unga safi, na atamwaga mafuta juu yake na kuweka ubani juu yake.
Anima cum obtulerit oblationem sacrificii Domino, simila erit eius oblatio; fundetque super eam oleum, et ponet thus,
2 Atachukua sadaka kwa wana wa Haruni, makuhani na pale kuhani atachukua konzi moja ya unga safi pamoja na mafuta na ubani. Kisha kuhani atateketeza hiyo sadaka juu ya madhabahu kuwa shukrani kwa uzuri wa Bwana. Italeta harufu nzuri sana kwa Bwana, itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
ac deferet ad filios Aaron sacerdotes: quorum unus tollet pugillum plenum similæ et olei, ac totum thus, et ponet memoriale super altare in odorem suavissimum Domino.
3 Unga wowote uliobaki utakuwa ni wa Haruni na watoto wake. Ni takatifu sana kwa Bwana iliyotolewa sadaka kwa Bwana kwa moto.
Quod autem reliquum fuerit de sacrificio, erit Aaron et filiorum eius, Sanctum sanctorum de oblationibus Domini.
4 Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate lainiya unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta.
Cum autem obtuleris sacrificium coctum in clibano: de simila, panes scilicet absque fermento, conspersos oleo, et lagana azyma oleo lita.
5 Kama matoleo yako ya nafaka yameokwa na kikaango cha chuma ni lazima iwe unga safi bila chachu uliochanganywa na mafuta.
Si oblatio tua fuerit de sartagine, similæ conspersæ oleo et absque fermento,
6 Utagawanya katika vipande na kumwaga mafuta juu yake. Hii ni sadaka ya nafaka.
divides eam minutatim, et fundes super eam oleum.
7 Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa katika kikaango, ni lazima iwe imetengenezwa kwa unga safi na mafuta.
Sin autem de craticula fuerit sacrificium, æque simila oleo conspergetur:
8 Utaleta matoleo ya nafaka yaliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana, italeta kwa kuhani, ambaye ataleta mbele ya madhabahu.
quam offerens Domino, trades manibus sacerdotis.
9 Ndipo kuhani atachukua baadhi ya sadaka ya nafaka ya shukrani ya Bwana, ataitekeza katika madhabahu. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, italeta harufu nzuri kwa Bwana.
Qui cum obtulerit eam, tollet memoriale de sacrificio, et adolebit super altare in odorem suavitatis Domino,
10 Itakayobaki sadaka ya nafaka itakuwa ya Haruni na wanawe. Itakuwa takatifu kamili ya Bwana kutoka matoleo kwa Bwana yatolewayo kwa moto.
quidquid autem reliquum est, erit Aaron, et filiorum eius, Sanctum sanctorum de oblationibus Domini.
11 Sadaka ya nafaka itolewayo kwa Bwana isiwe na chachu, hautatekeza chachu wala asali kama matoleo yatakayotekezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana.
Omnis oblatio, quæ offeretur Domino, absque fermento fiet, nec quidquam fermenti ac mellis adolebitur in sacrificio Domino.
12 Utayatoa kwa Bwana kama mazao ya kwanza, lakini hayatatumika kama matoleo ya harufu nzuri ya moto juu ya madhabahu.
Primitias tantum eorum offeretis ac munera: super altare vero non imponentur in odorem suavitatis.
13 Utaweka chumvi katika kila matoleo yako ya nafaka. Usipungukie chumvi ya agano la Bwana katika matoleo yako ya unga. Matoleo yako yote hayatapungukiwa na chumvi.
Quidquid obtuleris sacrificii, sale condies, nec auferes sal fœderis Dei tui de sacrificio tuo. In omni oblatione tua offeres sal.
14 Kama ukitoa matoleo ya nafaka ya mazao ya kwanza kwa Bwana, utatoa nafaka mbichi yaliyookwa kwa moto, na yaliyopondwa.
Si autem obtuleris munus primarum frugum tuarum Domino de spicis adhuc virentibus, torrebis igni, et confringes in morem farris, et sic offeres primitias tuas Domino,
15 Lazima utaweka mafuta na ubani juu yake. Haya ni matoleo ya nafaka.
fundens supra oleum, et thus imponens, quia oblatio Domini est.
16 Kuhani atatoa sehemu ya nafaka iliyopondwa na mafuta na ubani, kama sadaka ya shukrani itolewayo kwa uzuri wa Bwana. Hii ni sadaka ya Bwana inayotolewa kwa moto.
De qua adolebit sacerdos in memoriam muneris partem farris fracti, et olei, ac totum thus.

< Mambo ya Walawi 2 >