< Maombolezo 3 >

1 Mimi ni mwanaume nilyeona maangaiko chini ya gongo la hasira ya Yahweh. 2 Amenifukuza na kunisababisha kutembea kwenye giza kuliko kwenye nuru. 3 Hakika amenigeuzia mkono wake dhidi yangu tena na tena, siku yote. 4 Amefanya mwili wangu na ngozi yangu kufifia; amevunja mifupa yangu. 5 Amejenga vifusi vya udogo dhidi yangu, na kunizingira na uchungu na ugumu. 6 Amefanya ni ishi sehemu za giza, kama hao walio kufa zamani. 7 Amejenga ukuta kunizunguka na siwezi kutoroka. Amefanya minyororo yangu mizito 8 na japo nina ita na kulilia msaada, anazima maombi yangu. 9 Ameziba njia yangu kwa ukuta wa mawe ya kuchonga; amefanya njia yangu mbaya. 10 Yeye ni kama dubu anasubiri kunishambulia, simba katika maficho; 11 amegeuza pembeni njia zangu, amenifanya ukiwa. 12 Amepindisha upinde wake na kunifanya mimi kama lengo la mshale wake. 13 Ametoboa maini yangu kwa mishale ya mfuko wake. 14 Nilikuwa kichekesho kwa watu wangu wote, kielelezo cha dhihaka yao siku nzima. 15 Amenijaza kwa uchungu na kunilazimisha kunywa maji machungu. 16 Alivunja meno yangu na kokoto; amenisukuma chini kwenye fumbi. 17 Nafsi yangu imenyimwa amani; nimesahau furaha ni nini. 18 Hivyo na sema, “Ustahimilivu wangu umeangamia na pia tumaini langu kwa Yahweh.” 19 Kumbuka mateso yangu na kuangaika kwangu, maji machungu na uchungu. 20 Ninaendelea kukumbuka na nimeinama ndani yangu. 21 Lakini ni vuta hili akilini mwangu na hivyo nina matumaini: 22 Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi, 23 ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa. 24 “Yahweh ni urithi wangu,” Nilisema, hivyo nitamtumainia. 25 Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta. 26 Ni vizuri kusubiri taratibu kwa uwokovu wa Yahweh. 27 Ni vizuri kwa mtu kubeba nira katika ujana. 28 Acha aketi peke yake katika utulivu, inapo kuwa imewekwa juu yake. 29 Acha aeke mdomo wake kwenye vumbi - kunaweza bado kuwa na matumaini. 30 Acha atoa shavu lake kwa yeye anaye mpiga, na ajazwe tele kwa aibu. 31 Kwa kuwa Bwana hatatukataa milele, 32 lakini japo anatia uzuni, ata kuwa na huruma kwa kadiri ya mwingi wa upendo wake dhabiti. 33 Kwa kuwa haadhibu kutoka moyoni mwake au kutesa watoto wa mwanadamu. 34 Kukanyaga chini ya mguu wafungwa wote wa dunia, 35 kumnyima haki mtu mbele ya uwepo wa Aliye Juu, 36 mkunyima haki mtu - Bwana hataidhinisha vitu kama hivyo! 37 Ni nani aliye zungumza na ikatimia, kama sio Bwana kutamka? 38 Sio kutoka mdomoni mwa Aliye Juu majanga na mazuri yanakuja? 39 Mtu aliye hai anawezaje kulalamika? Mtu anawezaje kulalamika kwa adhabu ya dhambi zake? 40 Natujichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Yahweh. 41 Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu kwa Yahweh mbinguni: 42 “Tumekosea na kuasi, na haujasamehe. 43 Umejifunika na hasira na kutukimbiza, umeua na haujanusuru. 44 Umejifunika na wingu ili kwamba kusiwe na ombi linaloweza kupita. 45 Umetufanya kama uchafu na taka miongoni mwa mataifa. 46 Maadui wetu wote wametulaani, 47 wasiwasi na shimo limetujia, maafa na uharibifu. 48 Macho yangu yanatiririka na miferiji ya machozi kwasababu ya watu wangu. 49 Macho yangu yatatoa machozi pasipo kikomo; pasipo hauweni, 50 mpaka atakapo tazama chini na Yahweh ataona kutoka mbinguni. 51 Macho yangu yana ni sababishia uzuni kwasababu ya mabinti wa mji wangu. 52 Nimewindwa kama ndege hao walio kuwa maadui zangu; wameniwinda pasipo sababu. 53 Wamenitupa kwenye shimo na wakanitupia jiwe, 54 na maji yaka mwagika juu ya kichwa changu. Nilisema, “Nimekatwa mbali!” 55 Nililiita jna lako, Yahweh, kutoka kina cha shimo. 56 Ulisikia sauti yangu. Ulisikia sauti yangu nilipo sema, “Usifunge sikio lako kwa kilio changu cha msaada.” 57 Ulikuja karibu siku niliyo kuiita; ulisema, “Usiogope” 58 Bwana, ulitetea kesi yangu, uliokoa maisha yangu! 59 Yahweh, umeona mabaya waliyo ni fanyia, hukumu kesi yangu. 60 Umeona matusi yao, mipango yao yote dhidi yangu - 61 Umesikia dhihaka yao, Yahweh, na mipango yao kunihusu. 62 Midomo ya hao wanao inuka kinyume changu, na mashtaka yao, inakuja dhidi yangu siku nzima. 63 Ngalia jinsi wanavyo keti na kuinuka; wana nidhihaki na nyimbo zao. 64 Walipize, Yahweh, kwa kadiri ya waliyo fanya. 65 Utaacha mioyo yao bila lawama! Hukumu yako iwe juu yao! 66 Una wakimbiza kwa hasira na kuwaharibu nchini ya mbingu, Yahweh!

< Maombolezo 3 >