< Waamuzi 9 >

1 Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda kwa jamaa za mama yake huko Shekemu, akawaambia, na jamaa yote ya mama yake, 2 Tafadhali sema haya, ili wakuu wote wa Shekemu wasikie, Ni kipi bora kwako Je, wana sabini wote wa Yerubali kutawala juu yenu, au kwamba moja tu atawale juu yenu? Kumbuka kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu. 3 Ndugu za mama yake waliongea kwa niaba yake kwa viongozi wa Shekemu, nao wakakubali kumfuata Abimeleki, wakasema, Yeye ndiye ndugu yetu. 4 Wakampa vipande sabini vya fedha katika nyumba ya Baali Berith; Abimeleki akazitumia kwa kuajiri watu wasio na sheria na wasiokuwa wajinga, waliomfuata. 5 Abimeleki akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra; na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, wana wa Yerubaali. Yotamu ndiye aliyebaki, mwana mdogo kabisa wa Yerubaali, kwa kuwa alijificha. 6 Wakuu wote wa Shekemu na Beth Milo wakaungana, wakaenda kumfanya Abimeleki mfalme, karibu na mwaloni karibu na nguzo iliyoko Shekemu. 7 Yotamu alipoambiwa juu ya jambo hilo, akaenda, akasimama juu ya Mlima Gerizimu. Alipiga kelele akawaambia, 'Sikilizeni, enyi viongozi wa Shekemu, ili Mungu awasikilize. 8 Siku moja miti ilikwenda kumtia mafuta mfalme juu yao. Wakauambia mzeituni, tawala juu yetu. 9 Lakini mti wa mizeituni ukawaambia, Je! Nitaacha mafuta yangu, ambayo hutumiwa kuheshimu miungu na wanadamu, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine? 10 Miti hiyo ikamwambia mtini, 'Njoo utawale juu yetu.' 11 Lakini mtini ukawaambia, Je, nitaacha utamu wangu na matunda yangu mazuri, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine? 12 Miti hiyo ikamwambia mzabibu, 'Njoo utawale juu yetu.' 13 Mzabibu ukawaambia, Je, nitaacha divai yangu mpya, ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, na kurudi na kuvuka juu ya miti mingine? 14 Kisha miti yote ikawaambia mchanga, 'Njoo utawale juu yetu.' 15 Miti ya miiba ikaiambia miti, 'Ikiwa unataka kunipaka mafuta niwe mfalme juu yako, njoo na upate usalama chini ya kivuli changu. Ikiwa sivyo, basi moto lazima uondoke kwenye mchanga na uiteketeze mierezi ya Lebanoni. ' 16 Basi, ikiwa umefanya kweli na uaminifu, ulimfanya Abimeleki mfalme, na ikiwa umefanya vizuri juu ya Yerubaali na nyumba yake, na ikiwa umemuadhibu kama anavyostahili, 17 - na kufikiri kwamba baba yangu alipigana kwa ajili yenu, akahatarisha maisha yake, na akawaokoa kutoka kwenye mkono wa Midiani - 18 lakini leo umeamka juu ya nyumba ya baba yangu na kuwaua watoto wake, watu sabini, juu ya jiwe moja. Na umemfanya Abimeleki, mwana wa mtumishi wake, awe mfalme juu ya wakuu wa Shekemu, kwa sababu yeye ni ndugu yenu. 19 Ikiwa mlifanya kwa uaminifu na uelekevu pamoja na Jerubalai na nyumba yake, basi mnapaswa kufurahi katika Abimeleki, naye apate kufurahi ndani yenu. 20 Lakini ikiwa sio, moto utoke kwa Abimeleki, ukawaangamize watu wa Shekemu na Beth Milo. Basi moto utoke kwa watu wa Shekemu na Beth Milo, ili kumteketeza Abimeleki. 21 Yothamu akakimbia, naye akaenda Beeri. Aliishi huko kwa sababu ilikuwa mbali na Abimeleki, kaka yake. 22 Abimeleki akatawala juu ya Israeli kwa miaka mitatu. 23 Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu. Viongozi wa Shekemu walisaliti uaminifu waliokuwa nao kwa Abimeleki. 24 Mungu alifanya hivyo ili uhalifu uliofanywa kwa wana sabini wa Yerubaali uweze kulipizwa kisasi, na Abimeleki ndugu yao atawajibishwa kwa kuwaua, na watu wa Shekemu watawajibishwa kwa sababu walimsaidia kuua ndugu zake. 25 Basi wakuu wa Shekemu wakawaweka wanaume wamkisubiri juu ya vilima ili wamwangamize, nao wakawaibia wote waliokuwa wamepita katika barabara hiyo. Hii iliripotiwa kwa Abimeleki. 26 Gaali mwana wa Ebedi akenda pamoja na ndugu zake, wakavuka Shekemu. Viongozi wa Shekemu walimwamini. 27 Wakaenda shambani wakakusanya zabibu kutoka kwa mizabibu, nao wakazikanyaga. Walifanya sherehe katika nyumba ya mungu wao, walikula na kunywa, kumlaani Abimeleki. 28 Gaali mwana wa Ebedi, akasema, Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake? Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu! Kwa nini tunapaswa kumtumikia? 29 Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu! Kisha ningemuondoa Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, 'liondoe nje jeshi lako lote.' 30 Zebul, mkuu wa mji, aliposikia maneno ya Gaali, mwana wa Ebedi, hasira yake ikawaka. 31 Akatuma wajumbe kwa Abimeleki ili wapate kudanganya, akisema, Tazama, Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wanafika Shekemu; nao wanauchochea mji dhidi yako. 32 Sasa, amka wakati wa usiku, wewe na askari pamoja nawe, na uandae uvamizi katika mashamba. 33 Kisha asubuhi, jua litakapokwisha, inuka mapema na uangamize mji. Na yeye na watu waliokuwa pamoja naye watakapokuja juu yenu, fanyeni chochote mnachoweza. 34 Basi Abimeleki akainuka usiku, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaandaa uvamizi dhidi ya Shekemu, wakagawanyika vitengo vinne. 35 Gaali mwana wa Ebedi akatoka, akasimama penye mlango wa mji. Abimeleki na watu waliokuwa pamoja naye wakatoka mahali pa kuficha. 36 Gaali alipowaona hao watu, akamwambia Zebuli, “Tazama, watu wanatoka kwenye vilima!” Zebuli akamwambia, “Wewe unaona vivuli juu ya vilima kama vile watu”. 37 Gaali akaongea tena na kusema, “Angalia, watu wanashuka katikati ya nchi, na kitengo kimoja kinakuja kwa njia ya mwaloni wa Maenenimu.” 38 Ndipo Zebuli akamwambia, “Je, maneno yako ya kiburi yako wapi sasa, wewe uliyesema, 'Abimeleki ni nani, ili tumtumikie?' Je, hao sio watu ambao uliwadharau? Toka sasa na pigana nao.” 39 Gaali akatoka na alikuwa akiwaongoza watu wa Shekemu, naye alipigana na Abimeleki. 40 Abimeleki akamfukuza, na Gaali akakimbia mbele yake. Na wengi wakaanguka na majeraha ya mauti mbele ya mingilio ya lango la mji. 41 Abimeleki alikaa Aruma. Zebul akawalazimisha Gaal na ndugu zake watoke Shekemu. 42 Siku ya pili watu wa Shekemu wakatoka shambani, na habari hii ikamfikia Abimeleki. 43 Aliwachukua watu wake, akawagawanywa katika vitengo vitatu, na wakaandaa uvamizi mashambani. Aliangalia na kuona watu wakitoka mjini. Akawakamata na kuwaua. 44 Abimeleki na vitengo vilivyokuwa pamoja naye vilishambulia na kuzuia maingilio ya lango la mji. Vitengo vingine viwili vilishambulia wote waliokuwa katika shamba na wakawaua. 45 Abimeleki alipigana na huo mji siku nzima. Aliteka mji huo, na kuwaua watu waliokuwa ndani yake. Akabomoa kuta za mji na kueneza chumvi juu yake. 46 Wakati wakuu wote wa mnara wa Shekemu waliposikia hayo, waliingia katika ngome ya nyumba ya El Berithi. 47 Abimeleki aliambiwa kuwa viongozi wote walikuwa wamekusanyika pamoja kwenye mnara wa Shekemu. 48 Abimeleki akaenda mpaka mlima wa Salmoni, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. Abimeleki akachukua shoka na kukata matawi. Akaweka juu ya bega lake na kuwaagiza watu waliokuwa pamoja naye, 'Mlichoona nimekifanya fanyeni kama nilivyofanya.' 49 Basi kila mmoja akakata matawi, wakamfuata Abimeleki. Wakayafungia juu ya ukuta wa mnara, nao wakawasha moto, hata watu wote wa mnara wa Shekemu wakafa, wanaume na wanawake elfu. 50 Abimeleki akaenda Tebezi, naye akapiga kambi dhidi ya Thebezi, akautwaa. 51 Lakini kulikuwa na mnara wenye nguvu katika mji, wanaume na wanawake wote na viongozi wote wa mji walikimbilia na kujifungia wenyewe. Kisha wakaenda juu ya paa la mnara. 52 Abimeleki alikwenda kwenye mnara na kupigana nao, naye akaenda karibu na mlango wa mnara ili kuuchoma. 53 Lakini mwanamke akatupa jiwe la juu, juu ya kichwa cha Abimeleki likavunja fuvu lake. 54 Kisha akamwita yule kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, akamwambia, “Chukua upanga wako ukaniue, kwa hiyo hakuna mtu atakayesema juu yangu, 'Mwanamke alimwua.'” Basi kijana wake akamchoma naye akafa. 55 Watu wa Israeli walipoona kwamba Abimeleki amekufa, wakaenda nyumbani. 56 Basi Mungu akalipiza kisasi cha uovu wa Abimeleki alichomfanyia baba yake kwa kuua ndugu zake sabini. 57 Mungu akafanya uovu wote wa watu wa Shekemu ugeuke juu ya vichwa vyao wenyewe, na juu yao ilikuja laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali.

< Waamuzi 9 >