< Waamuzi 6 >

1 Wana wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; naye akawatia mikononi mwa Midiani kwa miaka saba. 2 Uwezo wa Midiani uliwanyanyasa Israeli. Kwa sababu ya Midiani, watu wa Israeli walitengeneza makao wenyewe kutoka kwenye mabwawa katika milima, mapango, na ngome. 3 Kisha ikawa kwamba wakati wowote Waisraeli walipopanda mazao yao, Wamidiani na Waamaleki na watu kutoka mashariki waliwavamia Waisraeli. 4 Waliweza kutengenezajeshi lao juu ya ardhi na kuharibu mazao, mpaka njia ya Gaza. Hawakuacha chakula huko Israeli, wala kondoo wala ng'ombe wala punda. 5 Kila wakati wao na mifugo yao na mahema walipokuja, walikuja kama kundi la nzige, na haikuwezekana kuhesabu watu au ngamia zao. Walivamia ardhi ili kuiharibu. 6 Midiani iliwadhoofisha Waisraeli sana mpaka watu wa Israeli wakamwita Bwana. 7 Watu wa Israeli walipomwomba Bwana kwa sababu ya Midiani, 8 Bwana alimtuma nabii kwa wana wa Israeli. Nabii akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekuleta kutoka Misri; Nilikutoa nje ya nyumba ya utumwa. 9 Naliwaokoa kutoka kwenye mikono ya Wamisri, na kutoka kwenye mkono wa wote waliokuwa wakikunyanyasa. Niliwafukuza mbele yenu, na nimewapa nchi yao. 10 Niliwaambia, “Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; Nimewaamuru msiabudu miungu ya Waamori, ambao mnaishi katika nchi yao. Lakini hamkuitii sauti yangu.” 11 Basi malaika wa Bwana akaja na kukaa chini ya mwaloni huko Ofra, uliokuwa wa Yoashi (Mwabiyezeri), wakati Gidioni, mwana wa Yoashi, akitenganisha ngano katika sakafu, katika kikapu cha divai-kuificha toka kwa Wamidiani. 12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nanyi, mpiganaji mwenye nguvu! 13 Gideoni akamwambia, Oo, bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, kwa nini basi yote haya yanatupata? Je, yako wapi matendo yake yote mazuri ambayo baba zetu walituambia, waliposema, 'Je! si Bwana aliyetukomboa kutoka Misri?' Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia mikononi mwa Midiani. ' 14 Bwana akamtazama na kusema, “Nenda katika nguvu uliyo nayo tayari. Uiokoe Israeli kutoka mkononi wa Midiani. Je, sikukutuma?” 15 Gideoni akamwambia, “Tafadhali, Bwana, nawezeje kuwaokoa Israeli? Angalia, familia yangu ni dhaifu zaidi katika Manase, na mimi si muhimu katika nyumba ya baba yangu.” 16 Bwana akamwambia, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utalishinda jeshi lote la Midiani kama mtu mmoja.” 17 Gideoni akamwambia, “Ikiwa unapendezwa na mimi, nipe basi ishara kwamba wewe ndio unenena nami. 18 Tafadhali, usiondoke hapa, mpaka nitakapokuja kwako na kuleta zawadi yangu na kuiweka mbele yako.” Bwana akasema, “Nitasubiri mpaka utakaporudi.” 19 Gideoni akaenda, akaandaa mwana mbuzi, na efa moja ya unga akafanya mikate isiyotiwa chachu. Akaiweka nyama hiyo katika kikapu, na akaweka mchuzi ndani ya sufuria na kuviletea chini ya mti wa mwaloni, akavitowa. 20 Malaika wa Mungu akamwambia, “Chukua nyama na mikate isiyotiwa chachu, ukaweke juu ya mwamba huu, ukamwage mchuzi juu yake.” Gideoni akafanya hivyo. 21 Kisha malaika wa Bwana akashika ncha ya fimbo mkononi mwake. Kwa hiyo akagusa nyama na mikate isiyotiwa chachu; moto ukatoka nje ya mwamba, ukateketeza nyama na mikate isiyotiwa chachu. Kisha malaika wa Bwana akaenda, na Gideoni hakuweza kumwona tena. 22 Gideoni alielewa kuwa yule alikuwa malaika wa Bwana. Gideoni akasema, “Ewe Bwana MUNGU! Kwa maana nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!” 23 Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope, huwezi kufa.” 24 Basi Gideoni akamjengea Bwana madhabahu huko. Aliiita, “Bwana ni Amani.” Hadi leo bado iko katika Ofra ya jamaa ya Waabiezeri. 25 Usiku huo, Bwana akamwambia, “Twaa ng'ombe wa baba yako, na ng'ombe wa pili wa umri wa miaka saba, ukaondoe madhabahu ya Baali, ambayo ni ya baba yako, na kukata Ashera iliyo karibu nayo. 26 Jenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wako juu ya mahali pa kukimbilia, na kuijenga njia sahihi. Toa ng'ombe ya pili kama sadaka ya kuteketezwa, ukitumia kuni kutoka Ashera uliyoikata. ' 27 Gideoni akachukua watumishi wake kumi na kufanya kama Bwana alivyomwambia. Lakini kwa sababu aliogopa sana watu wa nyumba ya baba yake na watu wa mji hakufanya hivyo wakati wa mchana, alifanya hivyo usiku. 28 Asubuhi wakati watu wa mji walipoamka, madhabahu ya Baali imebomolewa, na Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na ng'ombe wa pili ametolewa sadaka kwenye madhabahu iliyojengwa. 29 Watu wa mji wakaambiana, “Ni nani aliyefanya jambo hili?” Walipokuwa wakiongea na wengine na kutafuta majibu, wakasema, 'Gidioni mwana wa Yoashi amefanya jambo hili.” 30 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi, “Mtoe mtoto wako ili afe, kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali, na kwa sababu ameikata Ashera karibu nayo.” 31 Yoashi akawaambia wote waliompinga, “Je, ninyi mtamsihi Baali? Je, mtamuokoa? Mtu yeyote atakayemtetea, basi atauawa asubuhi hii. Ikiwa Baali ni mungu, basi atajitetea mwenyewe wakati mtu anaibomoa madhabahu yake.” 32 Kwa hiyo siku hiyo wakamwita Gideoni “Yerubaali,” kwa sababu alisema, “Baali ajijitetee dhidi yake,” kwa sababu Gidioni alivunja madhabahu ya Baali. 33 Basi Wamidiani wote, Waamaleki, na watu wa mashariki walikusanyika pamoja. Wakavuka Yordani na wakapanga katika bonde la Yezreeli. 34 Lakini Roho wa Bwana akaja juu ya Gideoni. Gideoni akapiga tarumbeta, akawaita jamaa ya Abiezeri, ili wapate kumfuata. 35 Aliwatuma wajumbe wote katika Manase, na wao pia, waliitwa nje kumfuata. Naye akatuma wajumbe kwa Asheri, na Zabuloni, na Naftali; nao wakaenda kumlaki. 36 Gideoni akamwambia Mungu, “Ikiwa ungependa kunitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema, 37 tazameni, ninaweka ngozi ya samazi kwenye sakafu. Ikiwa kuna umande tu juu ya ngozi, na ni kavu duniani, basi nitajua kwamba utanitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema.” 38 Hivi ndivyo ilivyotokea-Gideoni aliamka mapama asubuhi, akaikamua ngozi hiyo, na akatoa umande kwenye ngozi, wa kutosha kujaza bakuli kwa maji. 39 Gideoni akamwambia Mungu, 'Usinikasirikie, nitasema tena kwa mara nyingine. Tafadhali niruhusu nijaribu tena kwa kutumia ngozi. Wakati huu uifanye kavu, na iwe na umande juu ya ardhi yote kuzunguka. 40 Mungu alifanya kile alichoomba usiku huo. Ngozi ilikuwa kavu, na kulikuwa na umande katika ardhi yote iliyozunguka.

< Waamuzi 6 >