< Waamuzi 15 >

1 Baada ya siku kadhaa, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mbuzi mdogo akaenda kumtembelea mkewe. Akajiambia mwenyewe, “Nitaenda kwenye chumba cha mke wangu.” Lakini baba yake hakumruhusu aingie. 2 Baba yake akasema, “Nilidhani umemchukia, hivyo nikampatia rafiki yako. Dada yake mdogo ni mzuri kuliko yeye, Mchukue badala yake.” 3 Samsoni akawaambia, 'Wakati huu sitakuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati nikiwaumiza.' 4 Samsoni akaenda na kukamata mbweha mia tatu akawafunga pamoja kila jozi, mkia hadi mkia. Kisha akachukua taa na kuzifunga katikati ya kila mkia. 5 Alipokwisha kuviwasha moto vienge, akawaachia mbweha katika nafaka za Wafilisti zilizosimama, nao wakawasha moto nafaka zote zilizopandwa, na nafaka iliyosimama shambani, pamoja na mashamba ya mizabibu na mizeituni. 6 Wafilisti waliuliza, “Ni nani aliyefanya hili?” Wakaambiwa, “Samsoni, mkwe wa Mtimna alifanya hivyo kwa sababu Mtimna alimchukua mke wa Samsoni akampa rafiki yake.” Basi Wafilisti wakamwendea wakamchoma kwa moto yeye na baba yake. 7 Samsoni akawaambia, “Ikiwa ndivyo mnavyofanya, nitalipiza kisasi juu yenu, na baada ya hayo, nitaacha.” 8 Kisha akawakata vipande vipande, paja na mguu, kwa kuwauwa sana. Kisha akashuka chini akaishi katika pango katika mwamba wa Etamu. 9 Ndipo Wafilisti wakaja, wakajitahidi kupigana vita huko Yuda, wakaanzisha jeshi lao huko Lehi. 10 Watu wa Yuda wakasema, “Kwa nini mmekuja kutupiga?” Wakasema, “Tunashambulia ili tuweze kumkamata Samsoni, na tumtendee kama alivyotutendea.” 11 Kisha watu elfu tatu wa Yuda wakashuka hata kwenye pango la Eatamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! umetutendea nini?” Samsoni akawaambia, “Kwa kadili walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao.” 12 Wakamwambia Samsoni, “Tumeshuka kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba hamtaniua ninyi wenyewe.” 13 Wakamwambia, “La, tutakufunga tu kwa kamba na kukupeleka kwao. Tunakuahidi sisi hatutakuua.” Kisha wakamfunga na kamba mbili mpya na kumleta kutoka kwenye mwamba. 14 Alipofika Lehi, Wafilisti walipiga kelele walipokutana naye. Kisha Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitambaa cha kuteketezwa, na zikaanguka mikononi mwake. 15 Samsoni alipata mfupa mbichi wa taya ya punda, naye akaichukua na kuua watu elfu kwa mfupa huo. 16 Samsoni akasema, “Kwa taya ya punda, chungu juu ya chungu, na njaa ya punda nimewaua watu elfu.” 17 Samsoni alipomaliza kuzungumza, akatupa taya, na akaita mahali pale Ramath Lehi. 18 Samsoni alikuwa na kiu sana akamwita Bwana na kusema, “Umempa mtumishi wako ushindi mkubwa. Lakini sasa nitakufa kwa kiu na kuanguka mikononi mwa wale wasiootahiriwa?” 19 Na Mungu akapafungua mahali pa shimo palipo katika Lehi, na maji yakatoka. Alipokunywa, nguvu zake zikarejea na akahuishwa. Kwa hiyo aliita jina la mahali hapo Enhakore, na ni huko Lehi hadi leo. 20 Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli katika siku za Wafilisti kwa miaka ishirini.

< Waamuzi 15 >