< Ayubu 29 >

1 Ayubu akaendelea na kusema, 2 Ee, ningekuwa kama nilivyokuwa miezi iliyopita wakati Mungu aliponiagalia, 3 taa yake ilipowaka kichwani pangu, na pale nilipotembea gizani kwa nuru yake. 4 Ee, kwamba ningekuwa kama nilivyokuwa katika siku za ujana wangu uhusiano wangu na Mungu ulivyokuwa mzuri, 5 wakati Mwenyezi alipokuwa pamoja nami, na wanangu walipokuwa karibu nami, 6 wakati maisha yangu yalipokuwa yamejawa na utele, na mwamba uliponichuruzishia chemichemi za mafuta. 7 Nilipokwenda langoni mwa mji, nilipokaa katika eneo la mji, 8 vijana waliniona na walikaa mbali kwa kuniheshimu, na wazee waliinuka na kusimama kwa ajili yangu. 9 Wana wa mfalme waliacha kuongea nilipofika; wangeweka mkono wao katika vinywa vyao. 10 Sauti za waheshimiwa zililazimishwa, na ndimi zao hazikuweza kuongea vinywani mwao. 11 Kwani baada ya kunisikia, wangenibariki; waliponiona, wangeniona na kuniheshimu 12 kwa maana nilikuwa nikiwasaidia masikini waliokuwa wakiteseka, na yatima, asiye na msaada. 13 Baraka zao waliokuwa karibu kuangamia zilinipata; niliufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha. 14 Nilijivika utakatifu, nao ulinifunika; haki yangu ilikuwa kama kanzu na kilemba. 15 Niliwasaidia vipofu; niliwasaidia walemavu. 16 Niliwasaidia wahitaji; niliwasaidia hata wasionijua. 17 Nilimnyamazisha mwovu; nilimpokonya manusura kutoka katika meno yake. 18 Kisha nilisema nitakufa mahali salama; nitazizidisha siku zangu kama mchanga. 19 Mizizi yangu imeenea majini, na umande kukaa usiku wote katika matawi yangu. 20 Heshima yangu ni mpya daima, na nguvu za upinde wangu zipo katika mkono wangu kila wakati. 21 Watu walinisikiliza; walinisubiri; walisikiliza ushauri wangu. 22 Nilipo maliza kuongea hawakunena tena, maneno yangu yaliwatia nguvu kama mvua. 23 Waliningoja kama kungoja mvua; waliyathamini maneno yangu, kama walivyotamani mvua iliyokawia. 24 Niliwafurahia bila wao kutarajia; hawakukataa uzuri wa uso wangu. 25 Nilikuwa kama mfalme wao na kuwachagulia cha kufanya; nilikuwa kama mfalme katika jeshi lake, kama awafarijiye waombolezaji mazishini.

< Ayubu 29 >