< Ayubu 27 >

1 Ayubu akaendelea kuoengea na kusema, 2 “Kama aishivyo Mungu, ameniondolea haki yangu, Mwenyezi, aliyeyafanya machungu maisha yangu, 3 kadili uhai ungalimo ndani yangu uzima wa Mungu upo puani mwangu. 4 Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kunena uongo. 5 Sitakiri kwamba mko sahihi; hata nifapo sitakana uadilifu wangu. 6 Naishikilia haki yangu na sitaiacha; nafsi yangu haitanisuta kadili ninavyoishi. 7 Adui yangu na awe kama mwovu; anayeinuka kunyume changu na awe kama asiye haki. 8 Kwani tumaini la mwovu ni nini Mungu anapomwondoa, Mungu anapochukua uhai wake? 9 Je Mungu atasikiliza kilio chake tabu zinapompat? 10 Je atajifurahisha katika Mwenyezi na kumwita Mungu nyakati zote 11 Nitawafundisha kuhusu uwezo wa Mungu; sitabatilisha mawazo ya Mwenyezi. 12 Tazama, ninyi nyote mmeona; kwa nini basi mmeongea yasiyo na maana. 13 Hii ndiyo hatima ya waovu mbele za Mungu, urithi wa mtesaji aupokeao kutoka kwa Mwenyezi. 14 Ikiwa watoto wake wataongezeka, ni kwa upanga; uzao wake utakuwa na njaa. 15 Wanaomsalia watauawa kwa tauni, na wajane wao hawatawaombolezea. 16 Japokuwa waovu hurundika mali kama mavumbi, 17 na kukusanya mavazi kama udongo, atakusanya mavazi, lakini mwenye haki atavaa, na wasio na hatia watagawana mali. 18 Hujenga nyumba yake kama buibui, kama kibanda cha muda afanyacho mlinzi. 19 Hulala kitandani akiwa tajiri, lakini hataendelea hivyo; na afumbuapo macho, hana kitu. 20 Vitisho humpata kama maji, dhoruba humwondoa usiku. 21 Upepo wa mashariki umwondoa, naye huondoka; humwondoa mahali pake. 22 Humpiga bila kukoma; hujaribu kumnasua katika uwezo wake. 23 Unampigia makofi kwa kejeli; humwondoa mahali pake.

< Ayubu 27 >