< Ayubu 23 >

1 Kisha Ayubu akajibu na kusema, 2 “Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu. 3 Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo! 4 Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja. 5 Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu. 6 Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza. 7 Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu. 8 Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona. 9 Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone. 10 Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu. 11 Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka. 12 Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake. 13 Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda. 14 Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo. 15 Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa. 16 Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha. 17 Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.

< Ayubu 23 >