< Ayubu 18 >

1 Ndipo Bildadi Mshuhi alijibu na kusema, “ 2 Je, lini utaacha kusema kwako? Fikiri, na baadaye tutazungumza. 3 Kwa nini sisi tumehesabiwa kama wanyama mwitu; kwa nini tumekuwa wapumbavu machoni pako? 4 Wewe ambaye wajirarua mwenyewe katika hasira yako, nchi haipaswi kuachwa kwa ajili yako au miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake? 5 Ni dhahiri, nuru ya watu waovu itawekwa nje; cheche ya moto wake haitanga'ra. 6 Nuru itakuwa giza katika hema yake; taa yake juu yake yeye itawekwa nje. 7 Hatua za nguvu zake yeye zitafanywa kuwa fupi; mipango yake yeye mwenyewe itamwangusha yeye chini. 8 Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko. 9 Tanzi litamchukua yeye kwa kisigino; mtego utabaki kushikilia juu yake. 10 Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi; na mtego kwa ajili yake katika njia. 11 Watishao watamfanya yeye aogope juu ya sehemu zote; wao watamkimbiza yeye kwenye visigino vyake. 12 Utajiri wake utageuka kuwa njaa, na majanga yatakuwa tayari upande wake. 13 Sehemu za mwili wake zitakuwa zimemezwa; Hakika, mzaliwa wa kwanza wa kifo atazila sehemu zake yeye. 14 Yeye ameraruliwa kutoka kwenye usalama wa hema yake na hakuweza kutembea kwenda kwa mfalme mwenye utisho. 15 Watu ambao siyo wa kwake wataishi kwenye hema yake baada ya kuona ule moto mesambaa ndani ya nyumba yake yeye. 16 Mizizi yake itanyauka chini yake; juu tawi lake yeye litakatwa. 17 Kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi; yeye hatakuwa na jina katika mtaa. 18 Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu. 19 Hatakuwa na mtoto wa kiume wala mjukuu miongonni mwa watu wake, wala kizazi chochote kitakachobakia mahali alipokuwa amekaa. 20 Wale wanaoishi upande wa magharibi watakuwa wametiwa hofu kwa kile kitakachotokea kwake siku moja; wale wanaoishi upande wa mashariki watakuwa wameogopeshwa kwa hicho. 21 Hakika hizo ni nyumba za watu wasio haki, ni sehemu ya wale wasiomjua Mungu.”

< Ayubu 18 >