< Ayubu 15 >

1 Ndipo Elifazi Mtemani alijibu na kusema, 2 Mtu mwenye hekima anapaswa kujibu kwa maarifa yasiyofaa na kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki? 3 Anapaswa kuhojiana na mazungumzo yasiyo na faida au na hotuba ambazo kwa hizo yeye hawezi kufanya mema? 4 Dhahiri, wewe wafifisha heshima ya Mungu; Wewe wazuia heshima kwa yeye, 5 kwa maana uovu wako hufundisha midomo yako; Wewe wachagua kuwa na ulimi wa mtu mwenye hila. 6 Mdomo wako mwenyewe hukukukumu wewe, siyo wangu; hakika, midomo yako mwenyewe hushuhudia dhidi yako wewe. 7 Je, wewe ni mwanadamu wa kwanza ambaye aliyezaliwa? Wewe ulikuwepo kabla ya vilima kuwepo? 8 Wewe Umewahi kusikia maarifa ya siri ya Mungu? Je, wewe wajihesabia mwenye hekima wewe mwenyewe? 9 Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho sisi hatukijui? Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho hakiko katika sisi? 10 Pamoja nasi wapo pia wenye mvi na watu wazee sana ambao ni wazee zaidi kuliko baba yako. 11 Je, faraja ya Mungu ni ndogo sana kwako, maneno ambayo ni ya upole dhidi yako wewe? 12 Kwa nini moyo wako wewe unakupeleka mbali? Kwa nini macho yako yananga'ra, 13 ili ya kwamba kuirejesha roho yako kwa Mungu na kuyatoa maneno hayo kutoka katika mdomo wako? 14 Je, mwanadamu yeye ni nini kwamba yeye anapaswa kuwa safi? Yeye mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni nini kwamba yeye anapaswa awe mwenye haki? 15 Tazama, Mungu haweki tumaini lake hata kwa mmoja wake aliye mtakatifu; Hakika, mbingu haziko safi machoni pake yeye; 16 jinsi gani asivyo safi ni mmoja aliye mbaya na mla rushwa, mtu ambaye hunywa uovu kama maji! 17 Mimi nitakuonyesha wewe; Nisikilize mimi; Mimi nitakutangazia wewe vitu ambavyo nimeviona, 18 vitu ambavyo watu wenye hekima wamepita chini yake kutoka kwa baba zao, vile vitu ambavyo mababu zao hawakuvificha. 19 Hawa walikuwa mababu zao, ambao kwao pekee nchi walipewa, na miongoni mwao hakuna mgeni aliyepita. 20 Mtu mwovu hupitia katika maumivu siku zake zote, idadi ya miaka iliyowekwa juu kwa mtesaji kuteseka. 21 Sauti ya vitisho katika masikio yake; pindi yeye yuko katika kufanikiwa, mharibu atakuja juu yake yeye. 22 Yeye hafikiri kwamba yeye atarudi kutoka katika giza; Upanga humngojea yeye. 23 Yeye huenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya mkate, akisema, 'Kiko wapi? ' Yeye anatambua kuwa siku ya giza iko mkononi. 24 Dhiki na mateso makali humfanya aogope; wao hushinda dhidi yake yeye, kama mfalme tayari kwa vita. 25 Kwa sababu yeye ameunyosha mkono wake dhidi ya Mungu na ameishi kwa kiburi dhidi ya aliye mkuu, 26 huyu mtu mwovu hukimbia kwa Mungu na shingo ngumu, kwa vifundo vikubwa vya ngao. 27 Hii ni kweli, hata ingawa yeye amefunika uso wake kwa mafuta yake na amekusanya mafuta juu ya viuno vyake, 28 na ameishi katika miji yenye ukiwa; katika nyumba ambazo hakuna mwanadamu anayeishi humo sasa na ambazo zilikuwa tayari kuwa magofu. 29 Yeye hatakuwa tajiri; utajiri wake yeye hautadumu; hata kivuli chake hakitadumu katika nchi. 30 Yeye hatatoka nje ya giza; mwali wa moto utakausha matawi yake; katika pumzi ya kinywa cha Mungu yeye ataenda zake. 31 Mwacheni yeye asitumaini katika vitu visivyofanya kazi, akijidanganya yeye mwenyewe; maana upuuzi utakuwa mshahara wake yeye. 32 Itatokea kabla ya wakati wake yeye atapaswa kufa; tawi lake halitakuwa kijani. 33 Yeye atazipukutisha zabibu zake zisizovunwa kama mzabibu; yeye atayaondoa maua yake kama mti wa mzeituni. 34 Kwa maana msaada wa watu wasiomcha Mungu utakuwa tasa; moto utateketeza hema za rushwa. 35 Wao wanabeba mimba yenye ubaya na kuzaa uovu; tumbo lao hutunga mimba ya udanganifu.

< Ayubu 15 >