< Ayubu 14 >

1 Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke, huishi siku chache tu na amejaa mahangaiko. 2 Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini; yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu. 3 Je, wewe unatazama chochote katika hivi? Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi? 4 Ni nani anayeweza kukileta kitu safi kutoka katika kitu kichafu? Hakuna awaye yote. 5 Siku za mwanadamu zimeamriwa. Idadi ya miezi yake unayo wewe; umekiweka kikomo chake ambacho hawezi kukivuka. 6 Tazama mbali kutoka kwake kwamba yeye aweze kupumzika, ili kwamba aweze kufurahia siku yake kama mtu aliyekodishwa kama yeye anaweza kufanya hivyo. 7 Kunaweza kuwa na tumaini kwa mti; kama ukikatwa chini, unaweza kuchipua tena, hivyo chipukizi lake halitapotea. 8 Japokuwa mizizi yake inakua na kuzeeka katika ardhi, na shina lake kufa katika udongo, 9 hata kama bado lina harufu ya maji pekee, litachipua tena na kutoa nje matawi kama mche. 10 Lakini mwanadamu hufa; yeye huwa dhaifu; haswaa, mwanadamu hukoma kupumua, na tena yuko wapi yeye? 11 Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka, 12 vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena. Mpaka pale mbingu zitakapokuwa hazipo tena, hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao. 13 Laiti, kwamba ungenificha mimi mbali katika kuzimu mbali kutoka katika mahangaiko, na kwamba ungenitunza mimi katika siri hadi hasira yake imalizike, kwamba ungeniwekea mimi muda maalumu wa kukaa huko na kisha kuniita mimi katika fahamu! (Sheol h7585) 14 Ikiwa mwanadamu akifa, yeye ataishi tena? Ikiwa hivyo, ningependa kusubiri kule muda wangu wote wa kuharibika mpaka kufunguliwa kwangu kutakapokuja. 15 Wewe ungeita, na mimi ningekujibu wewe. Wewe ungekuwa na shauku ya kazi ya mikono yako. 16 Wewe ungehesabu na kutunza nyayo zangu; Wewe usingejali kumbukumbu ya dhambi yangu. 17 Uovu wangu ungetiwa muhuri katika mkoba; wewe ungeufunga uovu wangu. 18 Lakini hata milima huanguka na kuwa si chochote; hata miamba huhamishwa kutoka mahali pake; 19 maji yaliyokuwa chini ya mawe; kufurika kwake huondoa mbali mavumbi ya nchi. Kama hivi, ninyi mnavyoharibu matumaini ya mwanadamu. 20 Ninyi daima humshinda yeye, na yeye hupita mbali; Ninyi mnabadilisha uso wake na kumtuma yeye mbali kufa. 21 Kama watoto wake wa kiume ni wa kuheshimiwa, yeye, hatambui hicho; na kama wakishushwa chini, yeye haoni hicho. 22 Yeye hujisikia tu maumivu ya mwili wake mwenyewe, na hujiombolezea yeye mwenyewe.

< Ayubu 14 >