< Ayubu 12 >

1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema, 2 “Hakuna shaka ninyi wanadamu; Hekima mtakufa nayo. 3 Lakini nina ufahamu kama vile ninyi; Mimi siyo duni kwenu. Ni dhhiri, ni nani asiyefahamu vitu hivyo kama hivi? 4 Mimi ni kitu cha kuchekwa na jirani-Mimi, ni mmoja aliyemwita Mungu na ambaye alijibiwa na yeye! Mimi, ni mwenye haki na mtu asiyekuwa na hatia-Mimi sasa nimekuwa kitu cha kuchekwa. 5 Katika mawazo yake mtu fulani aliye katika kufurahi, kuna kudharau kwa mashaka; hufikiri katika njia ambayo huleta mambo mabaya zaidi kwa wale ambao miguu yao inateleza. 6 Hema za wezi hufanikiwa, na wale ambao humkasirisha Mungu huhisi salama; mikono yao wenyewe ni miungu wao. 7 Lakini sasa waulize hao wanyama wa mwituni, na watakufundisha wewe; waulize ndege wa angani, na watakuambia wewe. 8 Au iambie ardhi, na itakufundisha wewe; samaki wa baharini watakutangazia wewe. 9 Ni myama yupi miongoni mwa hawa asiyefahamu kuwa mkono wa Yahwe umetenda haya? 10 Katika mkono wake mna uzima wa kila kiumbe hai na pumzi ya wanadamu wote. 11 Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile kaakaa lionjavyo chakula chake? 12 Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu. 13 Pamoja na Mungu mna hekima na ukuu; yeye anayo mashauri na ufahamu. 14 Tazama, yeye huangusha chini, na haiwezekani kujengwa tena; kama yeye akimtia gerezani mtu yeyote, hakutakuwa tena kufunguliwa. 15 Tazama, kama yeye akiyazuia maji, yanakauka; na kama akiyaachilia nje yanaitaabisha ardhi. 16 Pamoja na yeye mna nguvu na hekima; watu ambao wamedanganywa na mdanganyi wote pamoja wako katika nguvu zake. 17 Yeye huwaongoza washauri mbali bila kuvaa viatu katika huzuni; huwarudisha hakimu katika upumbavu. 18 Yeye Huondoa minyororo ya mamlaka kutoka kwa wafalme; yeye hufunika viuno vyao kwa nguo. 19 Yeye huwaongoza makuhani mbali bila kuvaa viatu na kuwapindua watu wakuu. 20 Yeye huondoa hotuba ya wale waliokuwa wameaminiwa na huondoa mbali ufahamu wa wazee. 21 Yeye humwaga aibu juu ya binti za wafalme na hufungua mishipi ya watu wenye nguvu. 22 Yeye huweka wazi vitu vya kina kutoka katika giza na kuvileta nje kumuika vivuli mahali ambapa watu waliokufa wapo. 23 Yeye huyafanya mataifa kuwa na nguvu, na pia huyaharibu; Yeye pia huyakuza mataifa, na pia yeye huyaongoza mbali kama wafungwa. 24 Yeye huondoa mbali ufahamu kutoka kwa viongozi wa watu wa nchi; huwafanya wao kutangatanga msituni mahali pasipo na njia. 25 Wao wanapapasa katika giza bila kuwa na mwanga; yeye huwafanya wao kuweweseka kama mtu mlevi.

< Ayubu 12 >