< Yeremia 36 >

1 Ilikuja tokea katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosiah mfalme wa Yuda, kwamba neno hili lilikuja kwa Yeremiah kutoka kwa Yahwe, na alisema, 2 “Chukua kitabu kwa ajili yako na uandike juu yake maneno yote ambayo nimekwisha kukuambia kuhusiana na Israel na Yuda, na kila taifa. Fanya hivi kwa kila kitu nilichokuambia tokea siku za Yosia mpaka siku ile. 3 Huenda watu wa Yuda watasikiliza majanga yote ambayo ninakusudia kuleta juu yao. Huenda kila mmoja ataacha njia zake mbaya, ili kwamba niweze kuwasamehe maovu yao na dhambi zao.” 4 Kisha Yeremia alimwita Baruku mwana wa Neria, na Baruku aliandika kwenye kitabu, kwa imla ya Yeremia, maneno yote ya Yahwe yalizunguzwa kwake. 5 Kisha Yeremia alitoa amri kwa Baruku. Alisema, “Niko gerezani na siwezi kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. 6 Kwa hiyo unapaswa uende na kusoma kutoka kwenye kitabu ulichoandika kwa imla yangu. Kwa siku ya kufunga, unapaswa usome maneno ya Yahwe kwenye masikio ya watu katika nyumba yake, na pia kwenye masikio ya Yuda yote waliokuja kutoka katika miji yao. Tangaza maneno haya kwao. 7 Huenda maombi yao ya rehema yatakuja mbele ya Yahwe. Huenda kila mtu ataacha njia mbaya, kwani gathabu na hasira ya Yahwe imetangazwa dhidi ya watu kwa ukali.” 8 Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alifanya kila kitu ambacho Yeremia nabii alimwamuru yeye kufanya. Alisoma kwa sauti maneno ya Yahwe ndani mwa nyumba ya Yahwe. 9 Ilikuja tokea katika mwaka wa tano na mwezi wa tisa kwa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kwamba watu wote Yerusalemu na watu waliotoka Yerusalemu toka miji ya Yuda walitangaza kufunga kwa kumheshimu Yahwe. 10 Baruku alisoma kwa sauti maneno ya Yeremia katika nyumba ya Yahwe, kutoka kwenye chumba cha Gamaria mwana wa Shafani mwandishi, katika ua wa juu, kwa mlango wa kuingilia wa nyumba ya Yahwe. Alifanya hivi kwa masikio ya watu wote. 11 Basi Mikaya mwana wa Gemaria alisikia maneno yote ya Yahwe kwenye kitabu. 12 Alienda chini kwenye nyumba ya mfalme, kwenye chumba cha katibu. Tazama, maafisa wote walikuwa wamekaa hapo: Elishama mwandishi, Delaiah mwana wa Shemaiah, Elnathan mwana wa Achbor, Gemaria mwana wa Shefani, na Sedekia mwana wa Hananiah, na maafisa wote. 13 Kisha Mikaya alitoa taarifa ya maneno yote kwao ambayo alikuwa amesikia ambayo Baruku alisoma kwa sauti kwenye masikio ya watu. 14 Kwa hiyo maafisa wote walimtuma Jehudi mwana wa Nethania mwana wa Shelemiah mwana wa Kushi, kwa Baruku. Jehudi alisema kwa Baruku, “Chukua kitabu katika mkono wako, kitabu ambacho ulikuwa unakisoma kwa masikio ya watu and kuja.” Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alichukua kitabu katika mkono wake na alienda kwa maafisa. 15 Kisha walisema naye,”Kaa chini na usome haya katika masikio yetu.” Kwa hiyo Baruku akasoma kitabu. 16 Ilitokea wakati waliposikia haya maneno yote, kila mtu alipatwa na hofu kwa mtu aliye karibu naye na kusema kwa Baruku, “Kwa hakika tunapaswa kutoa taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme.” 17 Kisha walimuuliza Baruku, “Tuambie, ulipataje kuandika maneno yote haya kwa imla ya Yeremia?” 18 Baruku aliwaambia, “Alitoa imla ya maneno haya yote kwangu, na nikayaandika kwa wino kwenye kitabu hiki.” 19 Kisha maafisa walisema kwa Baruku, “Nenda, jifiche mwenyewe, na Yeremiah, pia. Usipatikane mtu yeyote kujua uko wapi.” 20 Kisha walienda kwa uwanja wa mfalme na wakatoa taarifa ya maneno haya kwake. Lakini kwanza walikihifadhi kitabu kwenye chumba cha katibu Elishama. 21 Basi mfalme alimtuma Yehudi kuchukua kitabu. Yehudi alikichukua toka chumba cha Elishama katibu. Kisha alikisoma kwa sauti kwa mfalme na wote maafisa walikuwa wamesimama karibu naye. 22 Sasa mfalme alikuwa amesimama kwenye nyumba ya majira ya baridi katika mwezi wa tisa, na mkaa ulikuwa unawaka mbele yake. 23 Ilitokea wakati Yehudi aliposoma kurusa tatu au nne, mfalme angeweza kuikata kwa kisu na kuitupa kwenye moto katika mkaa mpaka kitabu chote kiliteketea. 24 Lakini wala mfalme wala yeyote wa mjakazi wake aliyesikia haya maneno yote aliogopa, wala hawakuchana nguo zao. 25 Elnathani, Delaya, na Gemaria walikuwa wamemuomba mfalme asikichome kitabu, lakini hakuwasikiliza. 26 Basi mfalme alimwamuru Yerameeli, ndugu, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kumfunga Baruku mwandishi na Yeremia nabii, lakini Yahwe alikuwa amewaficha. 27 Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia baada ya mfalme kuwa amechoma kitabu na maneno ya Baruku yaliyokuwa yameandikwa kwa imla ya Yeremia, na alisema, 28 “Rudi, chukua kitabu kingine kwa ajili yako, na uandike maneno haya yote ambayo yalikuwa kwenye kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikichoma. 29 Kisha unapaswa kusema hivi kwa mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda: 'Ulichoma hicho kitabu! Na ulisema: Kwanini umeandika juu yake, “Mfalme wa Babeli hakika atakuja na kuharibu nchi hii, kwa kuwa atawaangamiza wanaume wote na wanyama ndani yake?” 30 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, Yehoyakimu mfalme wa Yuda: “Hakuna mzao wako atawahi kukaa kwenye kiti cha Daudi. Kama wewe, maiti yako itatupwa kwenye siku ya joto na usiku wa baridi. 31 Kwa kuwa nitakuadhibu, wazao wako, na wajakazi wako kwa maovu yenu yote. Nitaleta kwenu, kwa wakazi wote wa Yerusalemu, na kwa kila mtu Yuda majanga ambayo nimewatishia ninyi, lakini kwa hamkuwa makini.” 32 Kwa hiyo Yeremia alichukua kitabu kingine na akampa Baruku mwana wa Neria mwandishi. Baruku aliandika juu yake kwa imla ya Yeremia maneno yote ambayo yalikuwa katika kitabu kilichochomwa moto na mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda. Zaidi, maneno mengi ya kufanana yaliongezwa kwenye kitabu hiki.

< Yeremia 36 >