< Yeremia 30 >

1 Neno lilokuja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe likisema, 2 “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema, 'Jiandikie mwenyewe katika baraua maneno yote niliyotangaza kwako katika barua. 3 Maana ona, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapowarudisha mateka wa watu wangu Israeli na Yuda. Mimi, Yahwe, nimesema hili. Kwa maana nitawarudisha kwenye nchi ambayo niliwapa babu zao, na wataimiliki.”' 4 Haya ni maneno ambayo Yahwe anatangaza kuhusu Israeli na Yuda, 5 “Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Tumesikia sauti ya kutetemesha ya hofu na wala siyo ya amani. 6 Ulizeni na muone kama mwanaume anamwogopa mtoto. Mbona ninamwona kila mwanaume kijana ameshika mikono yake juu ya kiuno chake kama mwanamke anayejifungua mtoto? Kwa nini nyuso zao wote zimegeuka rangi? 7 Ole! Kwa maana siku hiyo itakuwa kuu, isiyofanana na yoyote. Utakuwa wakati wa huzuni kwa Yakobo, lakini ataokolewa. 8 Kwa maana itakuwa katika siku hiyo—hili ni tangazo la Yahwe wa majeshi—kwamba nitaivunja nira ya shingo zenu, na nitaisambaza minyororo yenu, kwa hiyo wageni hawatawafanya watumwa tena. 9 Bali watamwabudu Yahwe Mungu wao na kumtumikia Daudi mfalme wao, ambaye nitamfanya mfalme juu yao. 10 Kwa hiyo wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope—hili ni tangazo la Yahwe—na usikate tamaa, Israeli. Maana ona, niko karibu kukurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya utumwa, Yakobo atarudi na kuwa katika amani; ataokolewa, na hapatakuwa na hofu zaidi. 11 Kwa maana niko pamoja nawe—hili ni tangazo la Yahwe—ili kukuokoa. Kisha nitaleta mwisho kamili kwa mataifa yote ambako nimewatawanya. Bali sitaweka mwisho kwako, ingawa ninakuadhibu kwa haki na kwa hakika sitakuacha bila kukuadhibu.' 12 Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Jeraha lako si la kupona; kidonda chako kimeenea. 13 Hakuna mtu wa kukutetea kesi yako; hakuna utetezi kwa ajili ya kidonda chako ili upone. 14 Wapenzi wako wote wamekusahau. Hawatakuangalia, kwa maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui na nidhimu ya bwana mkatili kwa sababu ya uovu wako mwingi na dhambi zako zisizohesabika. 15 Kwa nini unaita msaada kwa ajili ya jeraha lako? Maumivu yako hayaponyeki. kwa sambabu ya uovu wako mwingi, dhambi zako zisizohesabika, nimefanya mambo haya kwako. 16 Kila mtu akulaye ataliwa, na adui zako wote wataenda utumwani. Kwa maana kila aliyekuteka nyara atatekwa, na nitawafanya wote wanaokuwinda kuwa mawindo. 17 Kwa maana nitaleta uponyaji juu yako; nitakuponya majeraha yako—hili ni tangazo la Yahwe—nitafanya hivyo kwa sababu walikuita: Mwenyekutupwa. Hakuna anayeujali Sayuni.” 18 Yahwe anasema hivi, “Ona, niko karibu kuwarudisha mateka wa hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu, na jumba litakuwepo tena kama ilivyokuwa kawaida. 19 Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya ya shangwe itasikika kutoka kwao, kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza; nitawaheshimu ili kwamba wasifanywe wanyonge. 20 Kisha watu watakuwa kama ilivyokuwa mwanzo, na kusanyiko lao litaanzishwa mbele yangu wakati nitakapowaadhibu wote wanaowatesa kwa sasa. 21 Kiongozi wao atatoka miongoni mwao. Atatokeza kutoka kati yao nitakapomleta karibu na atakapanikaribia mimi. kama sitafanya hivyo, ni nani atakayethubutu kunisogelea? —hili ni tangazo la Yahwe. 22 Kisha mtakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu. 23 Ona, tufani ya Yahwe, ghadhabu yake, imekwenda nje. Ni tufani isiyokoma. Itazunguka juu ya vichwa vya watu waovu. 24 Hasira ya Yahwe haitarudi mpaka itoke na kutimiza makusudi ya moyo wake. Katika siku za mwisho mtalielewa hili.”

< Yeremia 30 >