< Yeremia 26 >

1 Mwanzoni mwa utawala wake Yehoyakimu mwana wa Yosia, neno likaja kutoka kwa Yeremia, likisema, 2 “Yahwe anasema hivi: Simama katika uwanja wa nyumba yangu na sema kuhusu miji yote ya Yuda ambao huja kuabudu katika nyumba yangu. Tangaza maneno yote niliyokuamuru kuyasema kwao. Usipunguze neno lolote! 3 Labda watasikiliza, kwamba kila mtu ataziacha njia zake mbaya, ili nighairi majanga ninayokusudia kuyaleta juu yao kwa sababu ya uovu wa matendo yao. 4 Kwa hiyo lazima useme kwao, 'Yahwe anasema hivi: Kama hamtanisikiliza ili mtembee katika sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu— 5 kama hamsikilizi maneno ya watumishi wangu manabii ambao naendelea kuwatuma kwenu—lakini hamjasikiliza! — 6 kisha nitaifanya nyumba hii kuwa kama Shilo; nitaifanya nyumba hii kuwa laana katika macho ya mataifa yote juu ya dunia. 7 Makuhani, manabii, na watu wote wakamsikia Yeremia akitangaza maneno haya katika nyumba ya Yahwe. 8 Kwa hiyo ikatokea kwamba Yeremia alipomaliza kutangaza aliyokuwa Yahwe alimwwamuru kuyasema kwa watu wote, makuhani, manabii, na watu wote wakamsimamisha na kusema, “Hakika utakufa! 9 Kwa nini umetabiri katika jina la Yahwe na kusema kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa, pasipo wakaaji?” Kwa maana watu wote wameunda kundi dhidi ya nyumba ya Yeremia. 10 Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahwe. 11 Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, “Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!” 12 Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, “Yeremia amenituma kutabiri juu ya nyumb hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia. 13 Kwa hiyo sasa, imarisheni njia zenu na matendo yenu, na sikilizeni sauti ya Yahwe Mungu wenu kwamba ataghairi kuhusu janga ambalo ametangaza dhidi yenu. 14 Mimi mwenyewe—niangalieni! —niko mikononi mwenu. Nitendeeni yaliyo mema na sahihi katika macho yenu. 15 Lakini kwa hakika lazima mjue kwamba kama mtaniua mimi, basi mnaiweka damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wakaaji wake, kwa maana Yahwe amenituma kweli kwenu ili nitangaze maneno yote kwa ajili ya masikio yenu.” 16 Kisha wakuu na watu wote wakasema kwa makuhani na manabii, “Si vyema kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametangaza mambo haya kwetu katika jina la Yahwe Mungu wetu.” 17 Kisha watu kutoka wazee wa nchi wakasimama na kusema kwa kusanyiko lote la watu. 18 Wakasema, “Mikaya Mmorashi alikuwa akitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Alinena kwa watu wote wa Yuda na kusema, 'Yahwe wa majeshi anasema hivi: Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la magofu, na mlima wa hekalu utakuwa kilima kilichoota vichaka.' Hezekia mfalme wa Yuda na Yunda wote walimuua? 19 Hakumwogopa Yahwe na kuutaka radhi uso wa Yahwe ili kwamba Yahwe angeghairi kuhusu janga ambalo alilitangaza kwao? Kwa hiyo tutafanya maovu makubwa zaidi juu ya maisha yetu sisi wenyewe?” 20 Wakati huo huo palikuwa na mtu mwingine ambaye alitabiri katika jina la Yahwe—Uria mwan wa Shemaya kutoka Kiriath Yearimu—pia alitabiri juu ya mji na nchi hii, akikubaliana na maneno yote ya Yeremia. 21 Lakini Mfalme Yohoyakimu na wanajeshi wake wote na watumishi wake wote waliposikia maneno yake, kisha mfalme alijaribu kumuua, lakini Uria alisikia na kuogopa, kwa hiyo alikimbia na akaenda Misiri 22 Kisha mfalme Yehoyakimu alituma watu kwenda Misiri—Elnathani mwana wa Achbori na watu kwenda Misiri kumfuata Uria. 23 Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida. 24 Lakini mkno wa Ahikamu mwana wa Shapni alikuwa pamoja na Yeremia, hivyo hakutiwa mikonono mwa watu ili auawe.

< Yeremia 26 >