< Yeremia 22 >

1 Bwana asema hivi, “Nenda kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda, utangaze neno hili huko. 2 Ukaseme, 'Ewe Mfalme wa Yuda, wewe aliyeketi kiti cha Daudi, usikilize neno la Bwana. Nisikilizeni, enyi watumishi wake, na ninyi, watu wake mnaokuja kwa malango haya. 3 Bwana asema hivi, “Fanya haki na uadilifu, na mtu yeyote ambaye ameibiwa-muokoeni kutoka mkononi mwa mshindani. Usimtendee mabaya mgeni yeyote katika nchi yako, au yatima au mjane. Usifanye vurugu au kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa. 4 Kwa kuwa mkifanya mambo hayo, basi wafalme wanaoketi kiti cha Daudi wataingia milango ya nyumba hii wakiendesha gari na farasi, yeye, watumishi wake, na watu wake! 5 Lakini ikiwa hamsikilizi maneno haya kutoka kwangu ambayo nimeyasema-hili ndilo tamko la Bwana-basi nyumba hii ya kifalme itaharibiwa.'” 6 Kwa maana Bwana asema hivi juu ya nyumba ya mfalme wa Yuda, “Wewe uko kama Gileadi, au kama kilele cha Lebanoni kwangu. Hata hivyo nitakugeuza kuwa jangwa, katika miji isiyo na wenyeji. 7 Kwa kuwa nimewaagiza waharibifu kuja juu yenu! Watu wenye silaha zao watakata mierezi yako iliyo bora na kuiacha kuanguka kwenye moto. 8 Kisha mataifa mengi yatapita kwenye mji huu. Kila mtu atamwambia yule anayefuata, “Mbona Bwana amefanya hivi kwa jiji hili kuu?” 9 Na mwingine atajibu, “Kwa sababu waliiacha agano la Bwana, Mungu wao, wakainama kwa miungu mingine, wakaiabudu.” 10 Usilie kwa ajili ya aliyekufa. Usiomboleze kwa ajili yake. Lakini mlilie mtu yeyote anayeingia kifungoni, kwa maana hatarudi tena kuiona nchi aliyozaliwa.' 11 Maana Bwana asema hivi juu ya Yehoahazi, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyekuwa mfalme badala ya Yosia babaye, 'ametoka mahali hapa, wala hatarudi. 12 Atakufa huko mahali ambapo walimchukua mateka, na hataiona tena nchi hii.' 13 Ole mtu yeyote anayejenga nyumba yake kwa uovu na vyumba vyake vya juu katika udhalimu; ambao wengine hufanya kazi, lakini hawalipwi. 14 Ole mtu yeyote atakayesema, 'Nitajenga nyumba ndefu na vyumba vya juu vipana, na hujenga madirisha mapana, na kuta zenye mwerezi, na huipaka rangi nyekundu.' 15 Je, hii ndiyo inakufanya uwe mfalme mzuri, kwamba unataka kuwa na mbao za mwerezi? Je baba yako hakula na kunywa, lakini lakini alifanya hukumu na haki? Kisha mambo yakawa mazuri kwa ajili yake. 16 Alihukumu maneno ya masikini na mhitaji. Ilikuwa vizuri. Je, huku siko kunijua mimi? - hili ni tamko la Bwana. 17 Lakini hakuna kitu machoni na moyoni mwako isipokuwa wasiwasi kwa faida yako isiyo ya haki na kwa kumwaga damu isiyo na hatia, kwa ukandamizaji kuwatendea jeuri wengine. 18 Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Hawatamwomboleza wakisema 'ole, ndugu yangu! au 'Ole, dada yangu!' Hawataomboleza kwa kusema 'Ole, bwana! ' au 'ole, utukufu!' 19 Atazikwa maziko ya punda, ataburuzwa mbali na kutupwa nje ya milango ya Yerusalemu. 20 Panda milima ya Lebanoni piga kelele. Paza sauti yako Bashani. Piga kelele kutoka kwenye milima ya Abarimu, kwa maana marafiki zako wote wataharibiwa. 21 Nilinena nawe wakati ulioko salama, lakini ukasema, 'Sitasikia.' Hii ilikuwa desturi yako tangu ujana wako, kwani hukusikiliza sauti yangu. 22 Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na marafiki zako watakwenda kufungwa. Hakika wewe utakuwa na aibu na kufadhaika kwa matendo yako yote mabaya. 23 Wewe mfalme, wewe ambaye huishi katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni, wewe aliyefanya kiota kati ya mierezi, utakuwa na hali ya kuhurumiwa utakapopata utungu kama wakati wa kuzaa.” 24 “Kama mimi niishivyo-hili ndilo tamko la Bwana-hata kama wewe, Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ulikuwa alama ya mkono wangu wa kulia, ningekuangusha. 25 Kwa kuwa nimewatia mikono ya wale wanaotaka uhai wenu na kwenye mkono wa wale ambao mnawaogopa, hata mkononi mwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Wakaldayo. 26 Nitawatupa wewe na mama yako aliyekuzaa katika nchi nyingine, nchi ambayo hujazaliwa, na huko utakufa. 27 Na kuhusu eneo hili ambalo watataka kurudi, hawatarudi hapa. 28 Je! Hiki ni chombo kilichodharauliwa na kilichopasuka? Je, Konia ni chombo kilichodharauliwa? Kwa nini wamemtupa yeye na wazao wake, kumpeleka katika nchi wasiyoijua? 29 Ee Ardhi, Ardhi, Ardhi! Sikieni neno la Bwana! 30 Bwana asema hivi, 'Andika juu ya mtu huyu Konia Yeye hatakuwa na mtoto. Hatafanikiwa wakati wa siku zake, wala hakuna hata mmoja kati ya uzao wake atakayefanikiwa au kuketi tena kwenye kiti cha Daudi na kutawala juu ya Yuda.'”

< Yeremia 22 >