< Isaya 7 >

1 Siku zile wakati Ahazi mtoto wa Yothani mtoto wa Uzia, mfalme wa Yuda, Rezeni mfalme wa Amramu, na Peka mtoto wa Remaelia, mfalme wa Israeli, walienda Yerusalemu kupigana vita nao, lakini hawakuweza kushinda vita. 2 Ilitaarifiwa kwa nyumba ya Daudi kwamba Amramu amejiunga na Efraimu. Moyo wake na moyo watu wake ukatetemeka, kama vile miti ya misitu inavyopepea kwa upepo. 3 Ndipo Yahwe akamwambia Isaya, ''Nenda nje na kijana wako, Sheari Jashubu ukaonane na Ahazi mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja Dobi. 4 Mwambie, 'awe makini, awe mtulivu, asiogope au vitisho kwa sababu ya mikia hii miwili ya vingi hivi vitokavyo moshi, kwa sababu ya hasira kubwa ya Resini na Amramu, na mtoto wa Remalia. 5 Amramu, Ephraimu, na mtoto wa Remaeli wamepanga mabaya juu yako; wamesema, '' njooni tuwavamie Yuda na kuwaogopesha, 6 njooni tujipange na tumueweke mfalme wetu ndani ya Yuda, mtoto wa Tabaeli.'' 7 Bwana Yahwe asema, ''haitatokea; haitaonekana, 8 maana kichwa cha Amramu ni Damaskasi, na kishwa cha Damaskasi ni Rezini. Ndani ya miaka sitini na tano, ndoto za Ephraimu zitasambaratishwa na hapatakuwa na watu. 9 Efraimu ni kichwa Samaria, na kishwa cha Samaria ni mtoto wa Remaria. Na kama hamtasimama imara katika imani yenu, hakika hamtakuwa salama''. 10 Bwana akaongea tena na Ahazi, 11 ''Omba ishara ya Yahwe Mungu wako; omba juu ya hilo kwa kina au kwa kiwango cha juu.'' (Sheol h7585) 12 Lakini Ahazi anasema, sintomba wala kumjaribu Yahwe.'' 13 Hivyo Isaya akajibu, ''sikilizen, nyumba ya Daudi. Je haijatosha kwa watu kuujaribu uvumilivu wa watu? Je ni lazima kuujaribu uvumilivu wa Mungu? 14 Hivyo basi Mungu mwenyewe atawapa yeye mwenywe ishara: ona, mwanamke bikira atapata mimba na kumzaa mtoto, na atamwita Emanueli. 15 Atakula siagi na asali na wakati anapojua kuyakataa maovu na kuchagua mema. 16 Maana kabla mtoto ajajua kuyakataa maovu na kuchagua mema, nchi ambayo wewe unawachukia wafalme itakuwa ukiwa. 17 Yahwe ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako siku hazijatimmia tangu Efraimu alipompokea Yuda- atamleta mfalme wa Asiria.'' 18 Mda huo Yahwe atapuliza filimbikwa ajili ya kupaa kutoka mkondo wa umbali wa Misri, na maana nyuki kutoka nchi ya Asiria. 19 Zitakuja na kukaa chini ya korongo, ndani ya mapango ya miamba, kwenye vichaka vya miba, na kwenye malisho. 20 Katika mda huo Bwana atamnyoa kichwani kichwani na nywele za miguuni kwa wembe ulioazimwa mto Efrarate— mfalme wa Asiria - na vilevile utasafisha ndevu zote. 21 Siku hiyo, mtu atahifadhi ndama na na kondoo wawili, 22 na kwasababu ya maziwa yatakayo patikana ni mengi, atakula siagi, maana kila atakaye bakia kwnye nchi atakula siagi na asali. 23 Mda huo, kutakuwa na maelfu ya mizabibu na thamani elfu za shekeli, hakutakuwa na kitu zaidi ya kuzalisha mbigiri na miiba. 24 Watu watenda pale kuwinda kwa upinde, kwa sababu nchi yote itazalisha mbigiri na miiba. 25 Watakaa mbali na vilima vitalimwa kwa jembe, kwa sababu ya hofu ya mbigiri na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kuchungia ngo'mbe na kondoo

< Isaya 7 >