< Isaya 66 >

1 Yahwe asema hivi, ''Mbinguni ni makao yangu, na nchi ni miguu yangu. Iko wapi nyumba uliyonitengenezea mimi? iko wapi sehemu amabayo ninaweza kupumzika? 2 Mkono wangu umeyafanya haya yote; hivi ndovyo jinsi ambavyo vitu vitatokeavyo—hili ndilo tamko la Yahwe. Mtu niliyempitisha, mwenye roho iliyopondeka na mwenye kujutia roho, na atetemekaye kwa ajili ya neno langu. 3 Yeyote achinjae ng'ombe humuua mtu pia; yeye anayetoa sadaka ya kondoo huvunja shingo ya mbwa pia; yeye anayetoa sadaka ya mavuno anatoa sadaka ya damu yangurue; yeye anayetoa kumbukumbuvumba huwabariki wakosaji pia. Wamechagua njia zao wenyewe wanachukua radhi kwa uchafu wao wenyewe. 4 Katika njia hiyo hiyo nitachagua adhabu yao wenyewe; Nitaleta juu yao kitu wanachokiogopa, maana niilpowaita, hakuna aliyeitika; nilipozungumza aliyenisikiliza mimi. Walifanya yaliyo maovu mbele yangu, na kuchagua yasiyo nipenindeza mimi.'' 5 Sikiliza neno la Yahwe, ewe utemekae kwa neno lake, ''Kaka zako wanaonichukia na kukutenga wewe kwa ajili ya jina langu walisema, 'Na atukuzwe Yahwe, halafu tutaiona furaha yenu; lakini mtatiwa katika aibu. 6 Sauti ya vita vya ghasi vinakuja katika mji, sauti kutoka hekaluni, sauti ya Yahwe anawarudia maadui zake. 7 Kabla ajaenda katika chumba, hujifungua; kabla ya uchungu kumtoka hujifungua mtoto wa kiume. 8 Ni nani asikiaye mambo haya? Ni nani aonae mambo haya? Je taifa linaweza kuanzishwa kwa wakati mmoja? lakini kwa haraka Sayuni inapokwenda katika chumba, hujifungua watoto wake. 9 Ninawezaje kumleta mtoto azaliwe na nisimruhusu mtoto azaliwe? Yahwe auliza? — au Je ninamleta mtoto wakati tu wa kujifungua na halafu nimshikilie tena - anauliza Yahwe.'' 10 Furahia na Yerusalemu na fuhahia kwa ajili yake, ninyi nyote mnaopenda yeye; furahia pamoja na yeye, ninyi mnaomboleza juu yake! 11 Maana utamuuguza na ataridhika, katika maziwa yake atakufariji; utakunywa mpaka ushibe na kufurahia kwa wingi wa utukufu wake. 12 Yahwe asema hivi, ''Ni nanakaribia kutawanya mafanikio juu katika mto, na utajiri wa mataifa kama wingi wa mkondo wa maji. Utamuuguza kwa upande wake, na kubebwa katika mikono yake, mtabebwa juu ya magoti yake. 13 Kama vile mama anavyomfariji mtoto wake, hivyo basi nami nitawafariji ninyi, na mtapata faraja katika Yerusalemu.'' 14 Utayaona haya, na moyo wako utafurahia, na mifupa yako itachipukia kama zabuni ya nyasi. Aridhi ya Yahweitajulikana kwa watumishi wake, lakini atawaonyesha hasira yake dhidi ya maadui zake. 15 Kwa kutazama, Yahwe anakuja kwa moto, na gari lake linakuja kama upepo wa dhoruba kuleta joto katika hasira yake na kukemea kwake ni kama moto uwakao. 16 Maana Yahwe ametekeleza hukumu juu ya watu kwa moto na kwa upanga wake. Wale watakaouliwa na Yahwe watakuwa wengi. 17 Watajiweka wakfu wenyewe na kujisafisha wenywe, ili waweze kuingia katika bustani, kumfuata aliyeko katikati ya wale walao nyama ya nguruwe na vitu haramu kama panya. ''Watafika mwisho - hili ni tamko la Yahwe. 18 Maana ninayajua matendo yao na mawazo yao. Wakatiutafika nitakapoyakusanya mataifa yote na lugha zote. Watakuja na kuona utukufu wangu. 19 Nitaweka ishara ya ukuu wangu miongoni mwao. Halafu nitawatuma wakazi kutoka miongoni mwao kwa mataifa. Kwa Tarshishi, Puti, na Ludi, upinde wale wanaochukua upinde wao, kwa Tubali, Javani, na umbali kuelekea katika pwani kule ambapo hawajasikia chochote kuhusu mimi wala kuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa. 20 Watawaleta kaka zako wote nje ya mataifa yote, kama sadaka kwa Yahwe. Watakuja kwa farasi na kwa gari, na kwa gari, juu ya nyumbu na juu ya ngamia, kuelekea mlima wangu mtakatifu Yerusalemu - asema Yahwe. Maana watu wangu wa Israeli wataleta sadaka ya mavuno kwenye vyombo visafi katika nyumba ya Yahwe. 21 Baadhi ya vitu hivi nitavichagua kama makuhani na walawi — asema Yahwe. 22 Maana itakuwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo nitakayoifanya ibaki mbele zangu— Hili ndilo tamko la Yahwe— Hivyo ndivyo ukoo wenu utakavyobakia, na jina lenu litabaki. 23 Kutoka mwenzi mmoja mpaka mwingine, na kutoka sabato moja mpaka nyingine, watu wote watakuja kukuinamia chini— asema Yahwe. 24 Watakwenda nje na kuona miili ya wafu ya watu walioniasi mimi, maana wadudu wawalao wao hatakufa, na moto huwaunguzao hautazimika; na itakuwa ni chuki kwa wale wote wenye mwili.''

< Isaya 66 >