< Isaya 6 >

1 Nyakati zile za kifo cha mfalme Uzzia, nilimuona Bwana akiketi katika kiti cha cha enzi; alikuw juu na mahali palipo inuka, na pindo la vazi lake limejaa hekaluni. 2 Juu yake kuna maserafi; kila moja lina mabwa sita; mawili yamefunika uso wake, na mawili yamefunika miguu yake, na mawili ya kurukia. 3 Kila mmoja anaitana na mwenzake nakusema, ''Mtakakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. ni Yahwe wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.'' 4 Misingi ya vizingiti imeshtuka kwa sauti ya mtu aliye nje, na njumba imejaa moshi. 5 Ndipo nikasema,'' Ole wangu'' ninastahili adhabu maan mimi ni mtu mwenye midomo michafu, na ninaishi na watu wenye midomo michafu, maana macho yangu yamemuona Mfalme, Yahwe, Yahwe wa majeshi.'' 6 Ndipo mmoja wa maserafi akaruka juu yangu; mkononi mwake akiwa amebeba makaa ya mawe yanayong'aa, ameyachukuwa kwa koleo mathebauni. 7 Akaugusa mdomo wangu kwa makaa ya mawe na akasema, ''Ona, makaa ya mawe yameshika midomo yako; maovu yako yameondolewa, na dhambi zako zimelipiwa kwa hili.'' 8 Nilisikia sauti ya Bwana ikisema, Nimtume nani; nani ataenda kwa niaba yetu?'' Ndipo nikasema, Niko hapa; nitume mimi.'' 9 Akasema nenda na uwambie watu, ' mnasikiliza lakini hamelewi; anaona lakini hamuangalii. ' 10 Nenda ufanye mioyo ya watu hawa kuwa migumu, na masikio yao kuwa mazito, na macho yao kuwa vipofu. Hivyo basi wanaweza kuona kwa macho yao, kusikia kwa masikioa yao, na kuelewa kwa mioyo yao wakajeuka na kuponjwa. 11 Ndipo nikasema, ''Bwana, mda gani?'' Akanijibu, mpaka mji itakapopata ajali na kuharibiwa na pasipo wakazi, na nyumba hazina watu, na nchi imeanguka katika ukiwa mtupu, 12 na mpaka pale Yahwe atakapo wapeleka watu mbali, na upweke wa nchi ni mkubwa. 13 Hata kama makumi ya watu watabaki kwenye nchi, itaharibiwa kwa mara nyingine kama mwaloni uliokatwa chini na shina lake likabaki, mbegu takatifu kwenye kisiki chake.''

< Isaya 6 >