< Isaya 55 >

1 ''Njooni, kila aliye na kiu, njooni kwenye maji! na ewe usio na pesa, njoo, ununua na ule! Njoo, nunua mvinyo na maziwa pasipo pesa na pasipo gharama. 2 Kwa nini tunapima fedha kwa kitu ambacho sio mkate? na kufanya kazi isiyoridhisha? Nisikilizeni mimi kwa makini na ule kilicho kizuri, na kujifurahisha mwenyewe kwa unono. 3 Jeuzeni masikio yenu, na mje kwangu! Sikiliza, iliuweze kuishi! Nitafanya agano ya milele na ninyi; pendo langu la kuaminika nililomuhaidi Daudi. 4 Tazama, nimwemuweka yeye kama shahidi kwa mataifa, kama kiiongozi na kamanda wa watu. 5 Tazama, utaliita taifa ambalo haulijui; na taifa ambalo halikujui wewe litakukimbilia wewe kwa sababu wewe ni Yahwe Mungu wao, Mtakatifu wa Israeli, yeye aliyekutukuza wewe. 6 Mtafuteni Yahwe maana anapatikana; muiteni yeye maana yu karibu. 7 Tuwaache waovu waziache njia zao, na mtu mwenye dhambi mawazo yake. Muache yeye arudi kwa Yahwe, na atamuhurumia yeye, na kwa Mungu wetu, yeye ambaye atamsamehe huyo kwa wingi. 8 Maana mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zangu sio njia zenu- Hili ni tamko la Yahwe- 9 maana kama vile mbingu zilivyo juu kuliko nchi, hivyo ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10 Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji, 11 hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lilie nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma. 12 Maana utakwenda nje katika furaha na utaongozwa kwa amani; Milima na vilima vitapaza sauti kwa furaha mbele yako, na miti yote shambani itapiga makofi. 13 Badala ya miiba ya porini, misonobari itakuwa; na badala ya mbigiri, mihadasi inaota, na itakuwa kwa Yahwe, maana jina lake, ni kama alama ya milele ambayo haiwezi kuondolewa.''

< Isaya 55 >