< Isaya 54 >

1 ''Imba, ewe mwanamke tasa, ewe ambaye haujazaa; imba wimbo kwa furaha na lia kwa nguvu ewe ambaye hujapata uchungu wa kuzaa. Maana watoto walio katika ukiwa ni wengi kuliko watoto wa wanawake waliolewa,'' asema Yahwe. 2 Fanya hema lako kuwa kubwa na tawanya mapazia mbali, sio kidogo; nyoosha kamba zako na imarisha vigingi vyako. 3 Maana utawanjwa katika mkono wa kulia na wa kushoto, na ukoo wako utashinda mataifa na kuwapatia miji iliyo na ukiwa. 4 Usiogope maana hautahaibika, wala kukatishwa tamaa maana hautapatwa na aibu; hutasahau aibu ya ujana wako na aibu ya kutelekezwa. 5 Maana Muumba ni mume wako; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. Mtakatifu wa Israeli yeye ni mkombozi wenu; anaitwa Mungu wa nchi yote. 6 Yahwe anakuita wew urudi kama mwanamke aliyetelekezwa na mwenye roho ya huzuni, kama mwanamke mdogo aliyeolewa na kukataliwa, asema Mungu. 7 ''Kwa kipindi kifupi nimewatelekeza ninyi, lakini kwa huruma kubwa nitawakusanya ninyi. 8 Katika gharikia ya hasira nimeuficha uso wangu kwa muda. lakini kwa agano la milele la kuaminika nitakuwa na huruma na ninyi- amesema Yahwe, aliyewakomboa ninyi. 9 Maana haya ni kama Nuhu kwangu: kama nilivyoapa maji ya Nuhu hayuatapita tena katika nchi, Hivyo nimeapa kwama sitapatwa na hasira na ninyi wala kuwakemea ninji. 10 Japo milima yaweza kuanguka na vilima vyaweza kutikiswa, japo uimara wa pendo langu hautageuka nyuma kutoka kwenu, wala agano langu la amani kutikiswa- asema Yahwe, Yeye mwenye huruma juu yenu. 11 Wanaotaabika, wanaopitia dhoruba na wasio na faraja, tazama, nitaweka lami kwa rangi nzuri, na kuweka misingi kwa yakuti. 12 Nitaufanya mnara wa akiki na lango yake ya almasi na kuta zake za nje ni za mawe mazuri. 13 Na watoto wako wote watafundishwa na Yahwe; na amani ya watoto wako itakuwakubwa. 14 Katika haki nitakuanzisha tena. Hautaona dhiki tena, maana hautaogopa, na hakuna kitu cha kutisha kitakachokuja karibu yako. 15 Tazama, ikiwa yeyote atakaye koroga matatizo, hayatako kwangu; yeyote atakaye changanya matatizo pamaoja na wewe ataanguka kwa kishindo. 16 Tazama, nimemumba fundi, anayepuliza makaa yanayoungua na na kuanda a silsha kama kazi yake, na nimemumba mharibifu ili awaharibu. 17 Hakuna silaha iliyotengenezwa dhidi yako ikafanikiwa; na utamlaani kila mmjoa anayekutusi wewe. Huu ndio urithi wa watumishi wa Yahwe, na uthibitisho wake kutoka kwangu- Hili ndilo tamko la Yahwe.''

< Isaya 54 >

A Dove is Sent Forth from the Ark
A Dove is Sent Forth from the Ark