< Isaya 51 >

1 Nisikilizeni mimi, enyi mtendao haki, enyi mtafutaye Yahwe: Tazama katika mwamba uliouchonga nakuchimba kutoka pale ulipopakata.
"Listen to me, you who follow after righteousness, you who seek Jehovah: look to the rock you were cut from, and to the hold of the pit you were dug from.
2 Mtazameni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa ninyi; maan alipokuwa na upweke yeye mwenyewe, Nilimuita yeye. Nikambariki yeye na kumfanya yeye kuwa wengi.
Look to Abraham your father, and to Sarah who bore you; for when he was but one I called him, and I blessed him, and made him many.
3 Ndio, Yahwe ataifariji Sayuni; Ataifariji miji yake yote iliyo na ukiwa; jangwa lake atalifanya kama Edeni, na jangwa lililo wazi pembeni ya bonde la mto Yordani kama bustani ya Yahwe; Furaha na shangwe vitakuwa kwake, shukrani, na sauti ya kuimba.
For Jehovah has comforted Zion; he has comforted all her waste places, and has made her wilderness like Eden, and her desert like the garden of Jehovah; joy and gladness shall be found in it, thanksgiving, and the voice of melody.
4 ''Kuwa makini kwangu, watu wangu; na nisikilizeni mimi, watu wangu! Maana nitatoa amri, na nitaifanya haki yangu kuwa sheria ya mataifa.
"Attend to me, my people; and give ear to me, my nation: for a law shall go forth from me, and I will establish my justice for a light of the peoples.
5 Haki yangu ipo karibu; wokovu wangu utaenda nje, na mikono yangu itahihukumu mataifa; Pwani itanisubiri mimi; maana wanashauku ya kuhusubiria mkono wangu.
My righteousness is near, my salvation is gone forth, and my arms shall judge the peoples; the islands shall wait for me, and on my arm shall they trust.
6 Nyanyueni macho yanu juu angani, na tazama nchi chini, maana mbingu zitatoweka mbali kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, na wenyeji wake watakufa kama inzi. Lakini wokovu wangu utaendelea daima, na haki yangu haitaacha kutenda kazi.
Lift up your eyes to the heavens, and look on the earth beneath; for the heavens shall vanish away like smoke, and the earth shall wax old like a garment; and those who dwell in it shall die in the same way: but my salvation shall be forever, and my righteousness shall not be abolished.
7 Nisikizeni mimi, enyi mnaotambua ukweli, enyi watu wangu mliobeba sheria yangu katika mioyo yenu: Msiogope matusi ya watu, wala kukatishwa tamaa na unyanyasaji wao.
"Listen to me, you who know righteousness, the people in whose heart is my law; do not fear the reproach of men, neither be dismayed at their insults.
8 Maana Nonda watawala wao kama vazi, na minyoo itawala wao kama sufu; lakini haki yangu itakwa daima, na wokovu wangu katika vizazi vyote.''
For the moth shall eat them up like a garment, and the worm shall eat them like wool; but my righteousness shall be forever, and my salvation to all generations."
9 Amka, amka, jivishe wewe mwenyewe kwa nguvu, mkono wa Yahwe. Amka kama siku za zamani, kizazi cha nyaktii za kale, Je sio wewe uliyeangamiza mnyama wa baharini, na uliyemchoma joka?
Awake, awake, put on strength, arm of Jehovah; awake, as in the days of old, the generations of ancient times. Isn't it you who cut Rahab in pieces, who pierced the monster?
10 Je haukukausha bahari, maji ya kina kirefu, na kufanya kina cha bahari kuwa nija ya ukombozi kupita?
Isn't it you who dried up the sea, the waters of the great deep; who made the depths of the sea a way for the redeemed to pass over?
11 Fidia ya Yahwe itarudi na kwenda Sayuni kwa kilio cha furaha na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao, na huzuni na kuomboleza vitatoweka mbali.
The ransomed of Jehovah shall return, and come with singing to Zion; and everlasting joy shall be on their heads. They shall obtain gladness and joy. Sorrow and sighing shall flee away.
12 ''Mimi, mimi ndiye niwapae faraja. Kwa nini uwaogope watu, ambao wanakufa, watatoto wa wanadamu, waliofanywa kama majani?
"I, even I, am he who comforts you: who are you, that you are afraid of man who shall die, and of the son of man who shall be made as grass;
13 Kwa nini umemsahau Yahwe Muumba, yeye azinyooshayembingu na kuweka misingi ya nchi? Nyie ambao mna hofu za mara kwa mara kila siku kwa sababu ya hasira ya moto ya wanyanyasaji anapo fanya maamuzi ya kuangamiza. Iko wapi hasira ya wanyanyasaji?
and have forgotten Jehovah your Maker, who stretched forth the heavens, and laid the foundations of the earth; and fear continually all the day because of the fury of the oppressor, when he makes ready to destroy? and where is the fury of the oppressor?
14 Yeye aliyeinama chini, Yahwe atafanya haraka kumuachia; hatakufa wala kwenda chini katika shimo, wala hatakosa mkate.
The captive exile shall speedily be freed; and he shall not die and go down into the pit, neither shall his bread fail.
15 Maana Yahwe Mungu wenu, anaye ifanya bahari itembee, hivyo mawimbi yake yavume kwa kishindo- Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
For I am Jehovah your God, who stirs up the sea, so that its waves roar: Jehovah of hosts is his name.
16 Niweka maneno yangu mdomoni mwako, na nimekufunika wewe kwa kivuli cha mkono wangu, ili niweze kupanda mbingu, kuweka misingi ya nchi, na kutamkia Sayuni, 'ninyi ni watu wangu.''
I have put my words in your mouth, and have covered you in the shadow of my hand, that I may plant the heavens, and lay the foundations of the earth, and tell Zion, 'You are my people.'"
17 Amka, amka, simama juu, Yerusalemu, ewe unyweae katika kikombe cha hasira ya Yahwe kutoka mkononi mwako; umekunjwa katika kikombe, kikombe cha mateso, na umekunjwa na kumaliza.
Awake, awake, stand up, Jerusalem, that have drunk at the hand of Jehovah the cup of his wrath; you have drunk from the bowl, of the cup of staggering, and drained it.
18 Hakuna hata mmoja miongoni mwa watoto aliyewazaa wa kumuongoza yeye; hakuna hata mmoja miongoni mwa wote aliyewalea wa kumshika mkono wake.
There is none to guide her among all the sons whom she has brought forth; neither is there any who takes her by the hand among all the sons who she has brought up.
19 Shida hizi mbili ziliwatokea ninyi- ni nani atahuzunika pamja nanyi? - ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga. Ni nani atakayekufariji wewe?
These two things have happened to you. Who will grieve for you? Desolation and destruction, and the famine and the sword. Who will console you?
20 Watoto wako walizimia; walilala kila kona ya mtaa, kama swala kwenye mtego; Wamejawa na hasira ya Yahwe, Laana ya Mungu wako.
Your sons have fainted, they lie at the head of all the streets, as an antelope in a net; they are full of the wrath of Jehovah, the rebuke of your God.
21 Lakini sasa sikiliza hili, ewe uliodhulumiwa na kulewa, lakini sio kwa mvinyo:
Therefore hear now this, you afflicted, and drunk, but not with wine:
22 Bwana wenu Yahwe Mungu, anayewasihi watu wake, asema hivi, ''Tazama, Nimechukua kikombe cha ukubwa mkononi mwako- ukubwa wa kikombe cha hasira yangu - ili usiweze kunjwa tena.
Thus says your Lord Jehovah, your God who pleads the cause of his people, "Look, I have taken out of your hand the cup of staggering, even the bowl of the cup of my wrath; you shall no more drink it again:
23 Nitakuweka kwenye mikono ya watesaji, wale waliokuambia wewe, Lala chini, ili tutembee juu yako'; wameufanya mgongo wako kama uwanjwa na kama wao wa.''
and I will put it into the hand of those who afflict you, who have said to your soul, 'Bow down, that we may walk over you;' and you have laid your back as the ground, and as the street, to those who walk over."

< Isaya 51 >