< Isaya 48 >

1 Sikiliza hili, nyumba ya Jakobo, mlioitwa kwa jina la Israeli, na mmetoka katika mbegu ya Yuda; yeye akirie kwa jina la Yahwe na kumuhusisha Mungu wa Israeli, lakini sio kweli wala kwa namna ya haki. 2 Maana wanajiita wenyewewatu wa mji mtakatifu na kumuamini Mungu wa Israeli; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. 3 ''Nimetangaza vitu kutoka siku nyingi; Wamekuja nje kutoka mdomoni mwangu, na nimewafanya wajulikane; halafu gafla nimewafanyia, na yakatimia. 4 Kwa sababu nilijua kwamba wewe ni mkaiidi, misuli ya shingo yako ni kama ya chuma, na paji la uso ni kama shaba, 5 Hivyo basi nilitangaza vitu hivi kabla havijatokeo hivyo, nilikujulisha wewe, 'Sanamu yangu imefanya haya au sanamu yangu ya kuchonga na sanamu yangu ya kuyeyusha, yamekwishisha vitu. 6 Umesikia kuhusu mambo haya; angalia ushahidi wote; na wewe, Je hautakubali kwamba ninacho kisema ni cha kweli? Kuanzia sasa na kuendelea Nitawaonyesha vitu vipya, mambo yaliyofichika ambayo hamkuyajua. 7 Sasa, na sio yaliyopita, yamekuwa sasa, na kabla ya leo hamkusikia kuhusu wao, hivyo hautaweza kusema, 'Ndio, nilijua kuhusu wao.' 8 Haukusikia; haukuelewa; haya mambo hayakufuniliwa katika masikio kabla ya. Maana nilijua kwamba umekuwa mdanganyifu, na kwamba umekuwa muasi kutoka kuzaliwa. 9 Kwa niaba ya jina langu nitahairisha asira yangu, na kwa heshima yangu nitajizuia kutokumuharibu yeye. 10 Tazama, Mimi niliwaandaa ninyi, lakini sio kama fedha; Nimekusafisha wewe katika tanuru la mateso. 11 Kwa niaba yangu, kwa niaba yangu nitafanya; maana ni kwa jinsi gani niruhusu jina langu lisiheshimike? Sitampa utukufu wangu mtu yeyote. 12 Nisikilize mimi, Yakobo, na Israeli niliyekuita: Mimi ndiye; Mimi ni wa kwanza, na pia wa mwisho. 13 Ndio, mkono wangu umeweka msingi wa nchi, na mkono wangu wa kuume ulizitawanya mbingu, zimesimama juu kwa pamoja. 14 Jikusanyeni wenyewe, nyinyi nyote, na sikilizeni; ni nani miongoni mwenu atangazaye mambo haya? Yahwe atakamilisha lengo lake dhidi ya Babeli. Atachukua mapenzi ya Yahwe dhidi ya wa Wakaldayo. 15 Mimi, nimezungumza, ndio, nimemchagua yeye, nimemleta yeye, na yeye atafanikiwa. 16 Sogea karibu na mimi, sikiliza hili; kutoka mwanzo sikuzungumza katika siri; lakini ilipotokea, Mimi niko hapa; na sasa Bwana Mungu amenituma mimi, na Roho wake.'' 17 Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli anasema, ''Mimi ni Yahwe Mungu wenu, ninayewafundisha juu ya kufanikiwa, ninayewaonyesha njia mtakayoiptia. 18 Ikiwa kama mtaheshimu amri zangu! Hivyo amani na maendeleo yatatiririka kama mto, na wokovu wenu ni kama mawimbi kwenye bahari. 19 Watoto wako watakuwa wengi kama mchanga, na watoto kutoka kwenye tombo zenu watakuwa wengi kama nafaka kwenye mchanga; majina yao hayataondolewa wala kufutwa mbele yangu. 20 Tokeni nje ya Babeli! wakimbieni Wakaldayo! kwa sauti ya kupiga kelele tangaza kwamba! hakikisha hili linajulikana, hakikisha hili linafika mpaka miisho ya nchi! sema 'Yahwe amemkomboa Yakobo mtumishi wake. 21 Hawakupatwa na kiu alipowaongoza katika jangwa, alifanya maji kutokea kwenye mwamba kwa ajili yao; aliugawa na kufungua mwamba, na maji yakatoka nje. 22 Hakuna amani kwa watenda makosa- amesema Yahwe.''

< Isaya 48 >