< Isaya 45 >

1 Yahwe asema hivi kwa mapakwa mafuta, kwa Koreshi, niliyemshika kwa mkono wa kuume, illi niweze kuangamiza mataifa mbele yake, kuwalinda wafalme, kufunguo milango mbele yao, ili lango liwe wazi: 2 ''Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja vipandevivande milango ya shaba na kukuta vipandevipande nguzo za chuma, 3 Nitakupa hazina iliyo gizani na utajiri uliofichwa mbali, ili ujue kwamba ni mimi Yahwe, niliyekuita kwa jina lako, Mimi, Mungu wa Israeli. 4 Kwa niaba ya Jakobo mtumishi wangu, na Israeli chaguo langu, Nimekuita wewe kwa jina lako: nimekupa heshima iliyotukuka, jabo hakunijua mimi. 5 Mimi ni Yahwe na hapana mwingine; hakuna Mungu ila mimi. Nitakuimarisha katika vita, japo hamkunifamu mimi; 6 kwamba watu wajue kutoka mapambazuko ya jua, na kutoka magharibi, kwamba hakuna mungu mwngine ila mimi: Mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine. 7 Nimefanya mwanga na nimeumba giza; Ninanateta amani na ninaumba majanga; Mimi Yahwe, nifanyae haya yote. 8 Enyi mbingu, nyesha kutoka juu! Acha anga lishushe chini haki, na acha nchi inyonje haki, ili wokovu uweze kuchipukia juu, na haki kutawanyika kwa pamoja. Mimi Yahwe nimewumba wote kwa pamoja. 9 Ole kwa yeyote anayesema kwa yule aliyemfanya yeye, kwake yeye ni kama chungu cha udongo miongoni mwa vyingu vya udongo katika aridhi! Je udongo umwambia mfinyanzi, 'Unatengeneza nini? au ' Kazi yako haina kitu cha kushika? 10 Ole wake asemae kwa baba, 'Unanizaa nini? au kwa mwanamke, 'unanizaa mimi nin?' 11 Yahwe asema hivi, yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, muumbaji wake: 'Kwa nini unauliza swali kuhusu nini nitakacho kifanya kwa watoto wangu? Je unaweza kuniambia kuuhusiana na kazi ya mikono yangu? 12 Nimeifanya nchi na kuumba mtu juu yake. Ni mkono yangu mimi nilioinyoosha ju ya mbingu, na nikazimuru nyota zote kutokea. 13 Nimemuinua Keroshi juu katika haki yangu, na nitalainisha njia zake zote. Ataujenga mji wangu kwa upya; atawachia walioko uhamishoni kurudi nyumbani kwao, na so kwa pesa wala kwa rushwa,'' asema Yahwe wa majeshi. 14 Yahwe asema hivi, mapato ya Misri na bidhaa ya Ethiopia pamoja na Waseba jamii ya watu werefu, tatawaleta kwenu. Watakuwa wa kwenu. Watafuata baada yenu, watakuja na minyororo. Watakuinamia chini na kukuomba huku wakisema, 'Hakika Mungu yuko pamoja na wewe na hakuna mwingine ila yeye.'' 15 Hakika mna Mungu aliyejifisha ndani yenu, Mungu wa Israeli, Mkombozi. 16 Wote wataabishwa na kuzaraliwa kwa pamoja; wale wachongao sanamu watatembea katika udhalilishaji. 17 Lakini Israeli itakombolewa na Yahwe kawa wokovu wa milele; na wala hautaabika tena au kudhalilishwa. 18 Yahwe asem hivi, nani aliyeziumba mbingu, Mungu wa kweli ndiye aliyeiumbwa nchi na kuifaya, ndiye aliyeianzisha nchi. Aliiumba yeye, sio kama taka, aliimba ili pawe na wenyeji: ''mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine. 19 Sijaongea katika siri, katika maeneo ya siri; Sijauambia ukoo wa Daudi, 'Nitafute bure! Mimi ni Yahwe ninayezungumza ukweli; Ninatangaza vitu vilivyo vya kweli. 20 Jikusanjeni wenyewe na mje! kusanyikeni kwa pamoja, enyi wakimbizi kutoka miongoni mwa mataifa! Hawana maarifa, wale wanaobeba sanamu ya kuchonga na kuiomba miungu asiyewasidia. 21 Sogeeni karibu na mnitangazie mimi, leteni ushahidi! waache walete mashauri kwa pamoja. Ni nani aliyewaonyesha haya kutoka zamani? Ni nani aliyetangaza? Je sikuwa mimi, Yahwe? na hakuna Mungu mwingine ila mimi, Mungu mwenye haki; na mkombozi; hakuna mwingine zaidi yake. 22 Nijeukieni mimi, na mkaokolewe, miisho yote ya nchi; Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine. Mimi mwenyewe ninaapa, ninaongea katika haki yangu, na sitarudi nyuma: 23 'kwangu kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri. 24 Wataniambia mimi, Ni katika Yahwe peke yake kuna wokovu na nguvu.'' wataaibika wale wote wenye hasira na Mungu. 25 Katika Yahwe makabila yote ya Israeli yataalalishwa; watachukua kiburi katika yeye.

< Isaya 45 >