< Isaya 32 >

1 Tazama, mfalme atatawala kwa haki, wakuu wataongoza kwa haki. 2 Kila mmoja atakuwa kama makazi kutoka kwenye upepo na kimbilio kutoka kwenye dhoruba, kama mifereji kwenye sehemu kavu, kama kivuli kwenye mwamba mkubwa katika nchi iliyochoka. 3 Halafu macho ya waie wanaoona hayataona giza, na masikio ya wale wanosikia yatasikia vizuri. 4 Wenye upele watafikiria kwa makini kwa uelewa wao, na wenye kigugumizi watazungumza dhahiri na kwa urahisi. 5 Mjinga hataitwa tena muheshimiwa, wala muongo hataitwa mkuu. 6 Maana mjinga anazungumza ujinga, na moyo wake unapanga maovu na matendo ya wasiomcha Mungu, na anaongea mambo mabaya kuhusu Yahwe. Na anawafanya wenye njaa kuwa tupu na wenye kiu kukosa maji 7 Njia ya muongo ni maovu. Anajua kubuni mipango mibaya ya kuwalagai masikini kwa uongo, na hata kama masikini atazungumza ukweli. 8 Lakini watu wa heshima wanapanga mipango ya kuheshimika; na kwa sabaubau ya matendo ya wenye heshima tuatasimama. 9 Nyanyukeni juu, enyi wanawake mlio wepesi, na sikilizeni sauti yangu; enyi mabinti msiowangalifu, nisikilizeni mimi. 10 Maana kwa mda mfupi zaidi ya mwaka ujasiri wenu utavunjika, nyie wanawake msiojali, maana mavuno ya zabibu yatakwama, mavuno hayatakuwepo. 11 Tetemekeni, enyi wanawake, mliowadhaifu; taabikeni enyi msikuwa wangalifu; ondoeni nguo zenu nzuri mbaki wazi; 12 Vaeni nguo za magunia katika viuno vyenu. Ole watakaojichukulia mashamba mazuri, kwa mzabibu ulio zaa sana. 13 Kwenye aridhi ya watu wangu kutamea miiba na mbigiri, hata juu ya nyumba za furaha na mji ulio na shangwe. 14 Maana jumba litaachwa, mji uliosongamana utakuwa faragha; kilima na mnara vitakuwa mapango daima, furaha ya punda, malisho ya mifugo; 15 mpaka roho itushukie sisi kutoka juu, na jangwa litakuwa shamba linalozaa, na shamba linalozaa litachukuliwa kama msitu. 16 Wenye haki wataishi jangwani; na wenye haki wataishi katika shamba linalozaa matunda. 17 Kazi ya mwenye haki itakuwa ni ya amani; na matokeo ya wenye haki, ni utulivu na kujiamini daima. 18 Watu wangu wataishi katika makao ya amani, na katika nyumba salama na mahali tulivu pa kupumzikia. 19 Lakini hata kama ni mvua ya mawe na msitu umeharibiwa, na mji umeteketezwa, 20 yule ambae anaye panda pembezoni mwa mifereji atabarikiwa, na yule atakaye wapeleka ng'ombe na punda kuchunga.

< Isaya 32 >