< Isaya 30 >

1 Ole wa watoto waasi, ''Hili ni tamko la Yahwe. ''Wataweka mipango, lakini haitatoka kwangu; wataungana na mataifa mengine, lakini hawakuongozwa na Roho wangu, hivyo wanongeza dhambi baada ya dhambi. 2 Wanapanga kushuka chini Misri, lakini hawajaniomba niwaelekeze. Wanatafuta ulinzi kutoka kwa Farao kuchukua kimbilio katika kivuli cha Misri. 3 Hivyo basi ulinzi wa Farao utakuwa aibu yenu, na kimbilio lenu katika kivuli cha Misri, kitakuwa udhalilishaji wenu, 4 japo wakuu wako Sayuni, na wajumbe wao wamekuja Hanesi. 5 Watahaibika kwa sababu ya watu ambao hawawezi kuwasaidia, wala kuwa na faida, lakini ni aibu, na fedheha. 6 Tamko kuhusu mnyama wa Negevi: kupitia kwenye mlango wa mateso na hatari, wa simba jike na simba dume, nyoka na nyoka wa moto aneyepaa, wamebeba utajiri wao kwenye mgongo wa punda, na hazina yao katika mabega ya ngamia, kwa watu ambao hawana msaada kwao. 7 Maana msaada Misri hauna maana; hivyo basi nimemwita Rahabu, aliyekaa bado. 8 Sasa nenda, andika hili mbele yao juu ya meza, na uyaandike katika kitabu, iliyaifadhiwe kwa mda mrefu kama ushuhuda. 9 Maana ni watu waasi, watoto waongo, watoto ambao hawaskilizi maelekezo ya Yahwe. 10 Wanawambia waonaji, ''msiangalie; na kwa manabii, ''msitabiri yaliyoyakweli kwetu; zungumza maneno ya kujipendeza kwetu, tabiri udanganyifu. Geukeni katika njia, 11 ondokeni kwenye njia; maana Mtakatifu wa Israeli amesitisha kuongea mbele ya uso wetu. 12 Hivyo basi mtakatifu wa Israeli asema, ''Kwa sababu umekataa maneno haya na kujifunza ukandamizaji na udanganyifu, 13 hivyo dhambi hii itakuwa kwenu kama kitu kilichovunjika tayari kwa kuanguka, kama kitu katika ukuta mrefu ambao anguko lake linakaribia, papo kwa hapo.'' 14 Atavunja kama chombo cha mfinyanyanzi kivunjavyo, hivyo basi hakitabaki kitu, hivyo hakuna vipande vyovyote vya kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, kuchota maji kisimani. 15 Maana Bwana Yahwe, Mtakatifu wa Israeli asema hivi, ''Kwa kurudi na kwa kupumzika mtaokolewa; katika utulivu na imani itakuwa ni nguvu zako, Lakini hamkuwa tayari. 16 Amesema, 'Hapana, maana kukimbia kwa farasi; hivyo tutakimbia; tutakimbia kwa kutumia farasi mwepesi; hivyo basi watakaojingiza watakuwa wepesi. 17 Watu eflu moja watakimbia kwa kumuhofia mtu mmoja; kwa vitisho vya watu watano mtakimbia mpaka mtakuwa kama nguzu ya bendera iliyoko juu ya mlima, au kama bendera kwenye kilima.'' 18 Lakini Bwana anawasubiri ili awape neema yake, Hivyo basi yuko tayari kuwaonyesha huruma. Maana Yahwe na Mungu wa haki; Huwabarikiwe wale wanaomsubiri yeye. 19 Maana watu wataishi Sayuni, na Yerusalemu na hawatalia tena. Hakika atakuwa neema kwenu kwa sauti ya kilio chenu. Atakaposikia tu, atawajibu ninyi. 20 Kupitia Yahwe tunapata mkate wa shida na maji ya mateso, hata sasa, mwalimu wako hatajifisha mwenyewe tena, lakini utamuona mwalimu wako kwa macho yako mwenyewe. 21 Masikio yako yatasikia maneno yanayosemwa nyuma, Hii ndio njia, pitia hii, ''utakapogeuka upande wa kulia au utakageuka upande wa kushoto. 22 Mtakinajisi kifuniko chenu mlichokiweka juu ya pesa na dhahabu na kukitupa. Mtakitupa mbali kama hedhi kali, '''utawambia wao, ''Ondokeni hapa.'' 23 Naye atatoa mvua kwanye mbegu zenu mtakapopanda kwenye aridhi, na mkate utakuwa kwa wingi kutoka kwenye aridhi na mazao yatazaa kwa wingi. Katika siku hizo ng'ombe zako zitachungwa katika eneo kubwa. 24 Ng'ombe na punda, wanaolima kwenye aridhi, watakula chakula cha majira kilicho tawnywa kwa koleo na uma. 25 Juu ya mlima mrefu na juu ya kilima kirefu, kutapitasha vijito na mifereji ya maji, katika siku siku ya machinjio makuu pale minara yote itakapoanguka. 26 Mwanga wa mwenzi utakuwa kama mwanga wa jua, na mwanga wa jua utang'aa mara saba, kama mwanga wa siku saba. Yahwe atakapofunga kuvujwa kwa watu wake na kuyaponya majeraha waliyoyapata. 27 jina la Yahwe limekuja kutoka sehemu ya mbali, Linawaka kwa hasira yake na katika moshi mnene. Midomo yake imejaa hasira, na lugha yake nia kama moto unaoangamiza. 28 Punzi yake ni kama maji yaliyojaa yanayofika mpaka katikati ya shingo, kwa ajili kuchuja mataifa kwa kuhamasisha uharibifu. Pumzi yake ni mzabuni katika taya za watu wanowasababisha kutangatanga mbali. 29 Utakuwa na wimbo kama usiku pale sherehe takatifu itakapofanyika, na moyo wenye furaha, pindi mmoja atakopo kwenda na katika mlima wa Yahwe, katika mwamba wa Israeli. 30 Yahwe atafanya mapambo ya sauti yake inayosikika na atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo na dhouba ya hasira yake na moto uwakao, pamoja na upepo mkubwa, mvua kubwa, na mvua ya mawe. 31 Maana kwa sauti ya Yahwe, Asiria itanyamazishwa; atahiaribu kwa fimbo. 32 Na kila adhabu iliyochaguliwa amechagua fimbo ambayo Yahwe ataiweka juu yao na wakisidikizwa na mziki wa kigoma na kinubi kama wataanzisha vita na kupgana nao. 33 Maana sehemu ya kuchoma iliandaliwa toka zamani. kweli, imeandaliwa kwa mfalme, na Mungu amelifanya kuwa na kina na upana. Rundo liko tayari kwa moto na kuni za kutosha. Punzi ya Yahwe, ni kama mkondo kiberiti, na utawsha moto.

< Isaya 30 >