< Isaya 2 >

1 Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu. 2 Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale. 3 Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu. 4 Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena. 5 Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe. 6 Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni. 7 Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari. 8 Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza. 9 Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu. 10 Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake. 11 Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo. 12 Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini- 13 na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani. 14 Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu, 15 na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukutaunaojitokeza, 16 na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli. 17 Kiburi cha mwanaume kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo. 18 Sanamu zote zitaondolewa. 19 Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi. 20 Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo. 21 Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake, 22 usimwaminia mtu, ambae pumzi yake inatokea katika pua yake, ni kwa kiasi gan?

< Isaya 2 >