< Isaya 18 >

1 Ole kwa nchi ya wezi wa mabawa, iliyoko mbali kupitia mito ya Ethiopia; 2 wanowatuma mabalozi wao kwa kupitia bahari, na vyombo vya majani juu ya maji. Nendeni enyi wajumbe wepesi, kwa watu warefu na laini waishio kwenye nchi, kwa watu wanogopa mbali na karibu, taifa lenye nguvu, wakanyagao watu, ambao mito imegawanya nchi yao. 3 Watu wote wakaao duniani nao wakaao katika nchi, pale ishara itakaponyanyuliwa juu ya milima, angalia; na sikilizeni mbiu itakapopulizwa. 4 Yahwe asema hivi, ''nitachunguza kimyakimya kutoka nyumbani kwangu, kama kupika joto kwenye jua, na kama ukungu kwenye joto la mavuno. 5 Kabla ya mavuno, pale kipindi cha maua kinapoisha, na maua yako tayari kuwa zabibu. Atakata matawi kwa kupogoa ndoano, na atakatiwa chini na kuchukua matawi yaliyotawanyika. 6 Wataachwa kwa pamoja maana ndege wa milimani na wanyama wa duniani. Ndege watatua kwao majira ya joto, na wanyama wote watakuwa kwao kipindi cha baridi.'' 7 Kwa mda huo kodi italetwa kwa Yahwe wa majeshi kwa watu warefu na laini, kwa watu wanohofia umbali na ukaribu, taifa imara na kukanyagwa chini, ambayo nchi yao imegawanjwa na mito, Kwa sehemu ya jina la Yahwe wa majeshi, mpaka mlima Sayuni.

< Isaya 18 >