< Isaya 14 >

1 Yahwe atakuwa na huruma juu ya Yakobo; atamchagua tena Israeli na kumrudisha tena kwenye nchi yake. Wageni wataungana nao na wataambatana wenyewe na nyumba ya Yakobo. 2 Mataifa yataletwa katika maeneo yao wenyewe. Ndipo nyumba ya Israeli itawachukwa katika nchi ya Yahwe kwa watumishi wa kiume na wakike. Watachukuwa wafungwa wale waliokamatwa, na watawaongoza wale waliokuwa wanawanyanyasa. 3 Siku hiyo Yahwe atatoa pumziko kutoka kwenye mateso na maumivu, na kutoka kwenye kazi ngumu ambayo waliitajika kuzifanya, 4 mtaimba hii kauli wimbo juu ya mfalme wa Babeli, ''Ni kwa jinsi gani wayanyasaji wamefika mwisho, kiburi cha hasira kimekwisha! 5 Yahwe amevunja wafanyakazi waovu, fimbo ya hao viongozi, 6 inayowapeleka watu kwenye laana na mapigo yasiyopimika, wanoongoza taifa kwa hasira, 7 yote iko katika punziko na utulivu; wmeanza kusherekea kwa kiimba. 8 Hata mti wa mseprasi inafuhaia pamoja mierezi ya Lebanoni; inasema, Tangu ulipoweka chini, hakuna mkata kuni aliyekuja kutungusha sisi, 9 Kuzimu haina hamu kwa ajili yako unaye enda pale. Watafufuka waliokufa kwa ajili yako, wafalme wote wa dunia, wafanje watoke katika viti vyao vya enzi, wafalme wote wa mataifa. (Sheol h7585) 10 Watazungumza na kukuambia wewe, 'umekuwa dhaifu kama sisi. 11 Kiburi chako kimeshushwa kuzimu na sauti kifaa cha kamba yako. Buu wameongezeka chini yako na vijidudu vinakufunika wewe.' (Sheol h7585) 12 Kwa jinsi gani ulivyoanguka kutoka mbinguni, nyota ya siku, jua la asubuhi! ni kwa jinsi gani mlivyoshushwa chini, umeyashinda mataifa! 13 Unasema katika moyo wako, ' Nitapaa kutoka juu mbinguni, nitanyanyua enzi yangu juu ya nyota za Mungu, na nitakaa kwenye mlima wa kukusanyikia, kwa mbali kufika kaskazini. 14 Nitapaa juu umbali wa mawingu; Nitalifanya mimi mwenyewe kama Mungu aliye juu zaidi.' 15 Lakini kwa sasa umeshushwa chini kuzimu, kwenye kina cha shimo. (Sheol h7585) 16 Wale wanaokuona watakuangalia wewe, watakuangalia sana. Watasema, Je ni huyu mtu aliyefanya dunia itetemeke, nani aliyetingisha falme, 17 ni nani aliyefanya dunia kama jangwa, ni nani aliyeharibu miji yake, na hataki kuwachia wafungwa waende nyumbani?' 18 Wafalme wote wamataifa, wote kwa pamoja wamelala chini kwa heshima, kila mtu kwa kaburi lake. 19 Lakini umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lilivyotupwa mbali. Maiti imekufunika kama vazi, na wale wanaochomwa kwa upanga, nani wale washukao mpaka misingi ya shimo. 20 Hautaunganishwa pamoja katika mazishi, kwa sababu umeiharibu nchi yako na kuuwa watu wako. Watoto wa watenda maovu hawatatajwa tena.'' 21 Anda machinjio kwa ajili ya watoto wake, kwa sababu ya uovu wa mababu zao, hivyo basi hawatanyanyuka juu na na kuimiliki aridhi ya nchi iliyojaa miji ya dunia yote.'' 22 Nitapanda juu yao''- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi. Nitang'oa jina katika Babeli, uzao, na ukoo''- hili ndilo tamko la Yahwe. 23 Tena nitaifanya nchi hiyo kuwa makao ya bundi, dimbwi la maji, nanitawafagia kwa mfagio wa uharibifu''- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi. 24 Yahwe wa majeshi ameapa, ''Hakika, kama nilivyodhamiria, itakuwa kama ilivyo; na kama nilivyo kusudia itakuwa: 25 Nitawavunja Waasiria kwa mikono yangu, na kukanyaga milima kwa miguu yangu mwenyewe. Hivyo nira yake itanyanyuliwa juu yao na mzigo juu ya mabega yao.'' 26 Huu ni mpango uliokusudiwa katika nchi yote, na huu ndio mkono ulionyanyuliwa juu ya mataifa. 27 Kwa maana Yahwe wa majeshi amepanga hivi; ni nani atakayemzia yeye? Mkono wake umenyanyuliwa juu, ni nani atakajemrudisha nyuma? 28 Katika miaka ambayo mfalme Ahazi alipokufa, hili ndio tamko lilokuja: 29 Msishangilie, enyi wafilisti wote, kwamba fimbo ya kukupigia wewe imevunjika. Maana katika njia ya nyoka atatoka fira, na watoto wake watakuwa moto nyoka wanaopaa. 30 Na mtoto wa kwanza wa maskini watachunga kondoo wao kwenye malisho yangu, na wahitaji watalala chini salama. Nitaiuwa mizizi yenu kwa njaa ambayo atawauwa wakazi wenu wote. 31 Omboleza, ewe lang, lia, ewe mji; ninyi nyote mtayeyukia mbali, Ufilisti. Maana kutoka kaskazini limetoka wingu la moshi, na hakuna hata mmoja atakaye odoka kwenye nafasi yake. 32 Ni kivipi mtu mmoja atamjibu mjumbe wa taifa? Kwamba Yahwe ameipata Sayuni, na ndani yake walionewa watatafuta kimbilio.

< Isaya 14 >