< Hosea 8 >

1 “Weka tarumbeta katika midomo yako! Tai anakuja juu ya nyumba ya Bwana kwa sababu watu wamevunja agano langu na waliasi dhidi ya sheria yangu. 2 Wananililia,'Mungu wangu, sisi katika Israeli tunakujua.' 3 Lakini Israeli amekataa mema, na adui atamfuata. 4 Wameweka wafalme, lakini sio kwa shauri langu. Wamewafanya wakuu, lakini sikuwa na habari. Kwa fedha zao na dhahabu wamejifanyia sanamu wenyewe, ili wakatiliwe mbali.” 5 “Ndama yako imekataliwa, Samaria. Hasira yangu inawaka juu ya watu hawa. Kwa muda gani watakuwa na hatia? 6 Kwa maana sanamu hii ilitoka Israeli; fundi aliifanya; si Mungu! Ndama ya Samaria itavunjwa vipande vipande. 7 Kwa maana watu hupanda upepo na kuvuna kimbunga. Mbegu zilizosimama hazina vichwa; haitoi unga. Ikiwa itakomaa, wageni watakula. 8 Israeli imemezwa; sasa wanalala kati ya mataifa kama kitu kisicho na maana. 9 Kwa maana walikwenda Ashuru kama punda wa mwitu pekee. Efraimu ameajiri wapenzi kwa ajili yake mwenyewe. 10 Hata ingawa wameajiri wapenzi kati ya mataifa, sasa nitawakusanya pamoja. Wao wataanza kupotea kwa sababu ya unyanyasaji wa mfalme wa wakuu. 11 Kwa maana Efraimu imeongeza madhabahu kwa sadaka za dhambi, lakini zimekuwa madhabahu kwa kufanya dhambi. 12 Niliweza kuandika sheria yangu kwao mara elfu kumi, lakini wangeiona kama kitu cha ajabu kwao. 13 Kwa ajili ya dhabihu za sadaka zangu, hutoa nyama na kuila, lakini mimi, Bwana, siwakubali. Sasa nitafikiri juu ya uovu wao na kuadhibu dhambi zao. Watarudi Misri. 14 Israeli amenisahau mimi, Muumba wake, na amejenga majumba. Yuda ameimarisha miji mingi, lakini nitatuma moto juu ya miji yake; itaharibu ngome zake.

< Hosea 8 >