Hosea 13

1 Efraimu alipozungumza, kulikuwa na tetemeko. Alijikuza katika Israeli, lakini akawa na hatia kwa sababu ya ibada ya Baali, naye akafa. 2 Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi. Wanatengeneza sanamu za chuma kutoka kwenye fedha zao, sanamu kwa kadiri ya ufanisi wao, zote ni kazi ya mafundi. Watu wanasema juu yao, 'Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama.' 3 Kwa hiyo watakuwa kama mawingu ya asubuhi, kama umande unaoondoka mapema, kama makapi yanayotokana na upepo kutoka kwenye sakafu, na kama moshi utokao kwenye bomba. 4 Lakini mimi ndimi Bwana, Mungu weko, tangu nchi ya Misri. Hutamjua Mungu mwingine bali mimi; wala zaidi yangu, hakuna mkombozi mwingine. 5 Nilikujua jangwani, katika nchi yenye kame. 6 Wakati ulipokuwa na malisho, ulishiba; na wakati uliposhiba, moyo wako ukainuliwa. Kwa sababu hiyo umenisahau. 7 Nitakuwa kama simba; kama chui nitaangalia kando ya njia. 8 Nitawaangamiza kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nami nitararua vifua vyao, na huko nitawaangamiza kama simba, kama vile mnyama wa mwitu atakayerarua vipande vipande. 9 Nitawaangamiza, Israeli; nani atakayekusaidia? 10 Mfalme wako yuko wapi, ili akuokoe katika miji yako yote? Wako wapi wakuu, ambao kwao umeniambia hivi, 'Nipe mfalme na wakuu'? 11 Nimekupa mfalme kwa hasira yangu, nikamchukua kwa ghadhabu yangu. 12 Uovu wa Efraimu umehifadhiwa; hatia yake imehifadhiwa. 13 Atakuwa na uchungu wa kujifungua, lakini ni mwana mjinga, kwa maana wakati wa kuzaliwa, hatatoka tumboni. 14 Je, nitawaokoa na mkono wa kaburi? Je, nitawaokoa na kifo? Ewe Mauti yako wapi mapigo yako? Ewe kaburi kuko wapi kuharibu kwako? Huruma itafichwa na macho yangu. (Sheol h7585) 15 Ingawa Efraimu anafanikiwa kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja; upepo wa Bwana utapiga kutoka jangwani. Kijito cha maji cha Efraimu kitauka, na kisima chake hakitakuwa na maji. Adui yake atapora ghala lake la kila kitu cha thamani. 16 Samaria itakuwa na hatia, kwa sababu amemuasi dhidi ya Mungu wake. Wataanguka kwa upanga; watoto wao wadogo watavunjwa, na wanawake wao wajawazito watatambuliwa wazi.