< Hagai 2 >

1 Katika Mwezi wa saba siku ya ishirini na moja ya mwezi, Neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa Nabii Hagai, na kusema, 2 “Ongea na mkuu wa mkoa wa Yudah, Zerubabeli mwana wa Sheltieli, na kwa kuhani mkuu Yehozadaki; na kwa masalia ya watu. Waambie, 3 Ni nani amebaki kati yenu aliuona utukufu wa nyumba ya kwanza? Na mnauonaje huu wa sasa? Je si kama si chochote machoni penu? 4 Sasa, muwe hodari, Zerubabeli' -hili ni tamko la Bwana - na uwe hodari, kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki; muwe hodari, enyi watu wa nchi! - hili ni tamko la Bwana - na kazi, kwa kuwa ni pamoja nawe! hili ni tamko la Bwana wa majeshi. 5 Kutegemeana na ahadi ilioko katika agano nililofanya na ninyi mlipotoka Misri na Roho yangu ilisimama katikati yenu, msiogope' 6 Kwa kuwa Bwana wa majeshi anasema hivi: 'kitambo kidogo kwa mara nyingine nitatikisa mbingu na dunia, bahari na nchi kavu! 7 Na nitatikisa kila taifa, na kila taifa wataleta vitu vya thamani kwangu, na kuijaza nyumba hii na utukufu!' asema Bwana wa Majeshi 8 Dhahabu na fedha ni yangu' - hili ni tamko la Bwana wa majeshi. 9 Utukufu wa nyumba hii utakuwa mkuu zaidi ya utukufu wa nyumba ya kwanza ', asema Bwana wa majeshi,' na nitawapa amani katika sehemu hii'- hili ni Tamko la Bwana wa majeshi 10 Katika siku ya ishirini na nne mwezi wa tisa, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Hagaina kusema, 11 “Bwana wa majeshi asema hivi: Muulize kuhani kuhusu sheria, na kusema: 12 kama mtu akibeba nyama iliyotolewa kwa Bwana katika pindo la vazi lake, kama upindo utagusa mkate au mchuzi, mvinyo au mafuta, au chakula kingine, je chakula hicho kinafanyika kitakatifu?”Kuhani alijibu akasema, “hapana” 13 Halafu Hagai akasema.”Kama mtu mchafu najisi kwa ajili ya kumgusa maiti na kugusa vitu hivi, wote wanaweza kuwa wachafu?” Kuhani akajibu na kusema, “Ndiyo, watakuwa wachafu.” 14 Kwa hiyo Haghai akajibu nakusema, “Ni pamoja na hawa watu na pamoja na taifa liliko mbele yangu! - haya anayasema Bwana- na pia kila kitu kimekwisha kwa mkono wake: walichotoa hakikuwa kisafi kilikuwa kichafu. 15 Kwa hiyo, fikiri kutoka siku hii ya leo na za nyuma, kabla hata jiwe halijawekwa kwenye jiwe lingine katika hekalu la Bwana, 16 ilikuwaje basi? kila mtu alipokuja kwenye vipimo ishirini vya nafaka, kumbe kulikuwa na vipimo kumi tu, na aliyekuja na aliyekuja kuchota divai ya vipimo hamsini, kumbe kuliwa na vipimo ishirini tu. 17 Niliwataabisha ninyi na kazi za mikono yenu kwa doa na koga, nalikini hamkunirudia'- asema Bwana. 18 tafakari siku hii ya leo na kuendelea, kutoka siku ya ishirini na nne katika mwezi mwezi wa tisa, toka siku ile msingi wa hekalu la Bwana kuwekwa. Tafakarini hilo! 19 Je, bado kuna mbegu katika ghala? Mzabibu, mti wa mtini, komamanga, na mti wa mzeituni havikuzaa matunda! lakini kutoka siku hii ya leo nitawabariki!”' 20 Tena neno la Bwana likaja kwa mara ya pili kwa Haghai siku ya ishiri na nne katika mwezi kusema, 21 “Sema na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli umwambie, 'Nitatikisa mbingu na dunia. 22 kwa hiyo nitaanhusha kiti cha falme na kuharibu nguvu ya falme za mataifa! nitaangusha magahari na wapandao; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa sababu ya upanga wa ndugu zake. 23 Siku hiyo '-hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi- 'Nitakuchukua wewe Zerubabeli mwana wa Sheltieli, kama mtumishi wangu'- hivi ndivyo Bwana anavyosema. “Nitakutuma kama pete ya muhuri wangu, kwa sababu mimi ndiye niliyekuchagua!'- asema Bwana wa majeshi!”

< Hagai 2 >