< Habakuki 3 >

1 Maombi ya Habakuki nabii: 2 Yahwe, nimesikia taarifa zako, na mimi naogopa. Yahwe, fufua kazi yako katikati wakati; katikati ya muda huu; fanya hiyo ijulikane; kumbuka kuwa na rehema katika ghadhabu yako. 3 Mungu alikuja kutoka Temani, na yule Mtakatifu kutoka Parani. (Sela) Utukufu wake umezifunika mbingu, na dunia ilikuwa imejaa utukufu wake. 4 Miali miwili ya mikono yake ilikuwa iking'aa kama mwanga, ambapo uweza wake ulifichwa. 5 Ugonjwa wa kuua ulitangulia mbele yake, na adha iliifuta miguu yake. 6 Yeye alisimama na akaipima nchi; aliangalia na aliyatikisa mataifa. Hata milima ya milele iliharibiwa kabisa, na vilima vya milele vilianguka chini. Njia yake ni ya milele. 7 Niliona mahema ya Wakushi katika mateso, na vitambaa vya mahema katika Midiani vinatetema. 8 Yahwe alikuwa na hasira pale mtoni? Ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya mito, au hasira yako dhidi ya bahari, unapopanda juu ya farasi wenye mikokoteni na wa ushindi wako? 9 Umeleta upinde wako bila mfuniko; unaweka mishale kwenye upinde wako! (Sela) uliigawa nchi na mito. 10 Milima ilikuona wewe na kugeuka kwa huzuni. Maji yaliyomwagwa chini yalipita juu yao; kina cha bahari kilipaza sauti. Mawimbi yake yakainuka juu. 11 Jua na mwezi vilisimama imara juu mahali pake katika mwanga wa mishale yako na ilipaa, pale katika uangavu wa mwanga wa mikuki yako. 12 Umetembea juu ya nchi kwa uchungu. Katika ghadhabu umepukuchua mataifa. 13 Ulikwenda nje kwaajili ya wokovu wa watu wako, Kwaajili ya wokovu wa mteule wako. Wewe pondaponda kichwa cha nyumba ya mwovu kuweka wazi msingi wa shingo. (Sela) 14 Umekichoma kichwa cha wapiganaji wake kwa mshale wake mwenyewe sababu walikuja kama upepo kututawanya sisi, wivu wao ulikuwa kama mtu ambaye anamteketeza masikini katika mahali pamaficho. 15 Umesafiri juu ya bahari kwa farasi wako, na kuyapita maji makuu. 16 Nilisikia, na ndani yangu nilitetemeka! midomo yangu ilitetemesha sauti. Uozo unakuja katika mifupa yangu, na chini yangu mwenyewe nilitetemeka kama nasubiri kwaajili ya siku ya kuhuzunisha ifike juu ya watu waliotushambulia sisi. 17 Ingawa mtini hauchipui na hauzai kutokana na mzababibu; na ingawa kuzaa kwa mti wa mzaituni hakuridhishi na mashamba hayatoi chakula; na ingawa kundi mifugo limetoweka na hakuna ng'ombe katika zizi, hiki ndicho nitakacho kifanya. 18 Bado, nitafurahia katika Yahwe. Nitakuwa nafuraha kwa sababu ya Mungu wa wokovu wangu. 19 Bwana Yahwe ni nguvu yangu na anaifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya mimi niende mbele mahali pangu pa juu. - kufuata maelekezo ya muziki, katika vyombo vyangu vya nyuzi.

< Habakuki 3 >