< Habakuki 2 >

1 Nitasimama kwenye nguzo yangu ya ulinzi na kujiweka mwenyewe juu ya mnara wa mlinzi, na nitatazama kwa makini kuona yeye atasema nini kwangu na namna gani nitageuka kutoka kwenye lawama yangu. 2 Yahwe alinijibu na alisema, “Rekodi maono haya, na uandike dhahiri juu ya kibao ili kwamba anayesoma anaweza kukimbia. 3 Sababu maono haya bado ni kwa wakati ujao na hatimaye atazungumza bila kuanguka. Ingawa inachelewa, isubiri. Sababu kwa hakika itatakuja na haitachelewa. 4 Tazama! yule ambae hamu yake siyo sawa ndani yake anapumua kwa nguvu. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani. 5 Sababu mvinyo ni msaliti wa kijana mwenye kiburi ili kwamba asistahimili, lakini hukuza tamaa yake kama kaburi na, kama kifo, haitaweza kuridhishwa. Yeye anajikusanyia kila taifa na anakusanya kwaajili yake watu wote. (Sheol h7585) 6 Haya yote hayatatengeneza usemi kumdhihaki na wimbo wa dhihaka unaomhusu, 'ole wake yule aongezaye visivyo vya kwake! kwa muda gani utaongeza uzito wa dhamana uliyochukua?' 7 Wale wanao ngojea kwako hawatainuka ghafla? na wale wanaokutetemesha kuamka? Utakuwa mwathirika kwaajili yao. 8 Kwasababu umeteka nyara watu wengi, mabaki yote ya watu, yatakuteka nyara wewe. Sababu umemwaga damu nyingi za watu na umetenda kwa uasi kinyume cha nchi, miji, na wote wanaokaa ndani yake. 9 Ole kwa yule anayechonga mapato maovu kwaajili ya nyumba yake, hivyo anaweza kutengeneza kiota chake juu kumweka yeye salama mbali na mikono ya uovu. 10 Umebuni aibu kwa nyumba yako kwa kuwakata watu wengi, na umefanya dhambi dhidi yako mwenyewe. 11 Sababu jiwe litapaza sauti kutoka ukutani, na pao la mbao litawajibu, 12 'Ole wake yule ajengaye mji kwa damu, na anayeimarisha mji kwa katika uovu. 13 Hii haitoki kwa Yahwe wa majeshi kwamba watu wafanye kazi kwa moto na mataifa yote mengine yanachakaa menyewe bila kitu? 14 Bado nchi itajaa maarifa ya utukufu wa Yahwe kama maji yanavyojaza bahari. 15 'Ole wake yule anayemfanya jirani yake alewe, wewe ambaye unaye ongeza sumu uwafanye walewe ili uweze kutazama uchi wao. 16 Utavimbiwa na aibu zaidi kuliko utukufu. Kunywa hiyo vilevile, na funua uchi wako mwenyewe. Kikombe cha mkono wa kuume wa Yahwe utakuja katika kukugeukia wewe, na aibu itafunika heshima yako. 17 Vurugu iliyofanywa kwa Lebanoni itakufunika na uharibifu wa wanyama utakuogopesha. Sababu umemwaga damu za watu na umetenda kwa uasi dhidi ya ile nchi, miji, na wote wanaokaa humo. 18 Sanamu iliyochongwa inakufaidia nini? Sababu yule aliyeichonga hiyo, au ambaye kaisubu kwa kuiyeyusha metali, ni mwalimu wa uongo; Sababu anaiamini kazi ya mikono yake anapotengeneza miungu hii isiyoongea. 19 'Ole kwa yule anayeuambia ubao, Amka! Au kwa jiwe lisiloongea, Inuka!' Vitu hivi vinafundisha? Angalia, hiki juu kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, lakini ndani yake hakipumui kabisa. 20 Lakini Yahwe yumo katika hekalu lake takatifu! Nchi yote iwe kimya mbele zake.

< Habakuki 2 >