< Mwanzo 20 >

1 Abraham akasafiri kutoka pale hadi nchi ya Negebu, na akakaa kati ya Kadeshi na Shuri. Akawa mgeni akiishi Gerari. 2 Abraham akasema kususu mkewe Sara, “ni dada yangu.” Kwa hiyo Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wake kumchukua Sara. 3 Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, “Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu.” 4 Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, “Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki? 5 Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.' Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia.” 6 Kisha Mungu akasema naye katika ndoto, “Kweli, ninajua pia kwamba umefanya hili katika uadilifu wa moyo wako, na pia nilikuzuia usitende dhambi dhidi yangu mimi. Ndiyo maana sikuruhusu umshike. 7 Kwa hiyo, mrudishe huyo mke wa mtu, kwa kuwa ni nabii. Atakuombea, na utaishi. Lakini usipo mrudisha, ujuwe kwamba wewe pamoja na wote walio wa kwako mtakufa hakika. 8 Abimeleki akaamka asubuhi na mapema akawaita watumishi wake wote waje kwake. Akawasimulia mambo haya yote, na watu wale wakaogopa sana. 9 Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, “Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa.” 10 Abimeleki akamwambia Abraham, “Nini kilikushawishi wewe kutenda jambo hili?” 11 Abraham akasema, “Ni kwasababu nilifikiri hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.' 12 Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu. 13 Wakati Mungu aliponiondoa katika nyumba ya baba yangu na kusafiri kutoka mahali kwenda mahali pengine, nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unioneshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, “Ni kaka yangu.”''' 14 Ndipo Abimeleki akatwaa kondoo, maksai, watumwa wa kiume na wa kike akampatia Abraham. Basi Abimeleki akamrudisha Sara, mke wa Abraham. 15 Abimeleki akasema, Tazama, Nchi yangu i mbele yako. Kaa mahali utakapopendezewa.” 16 Na kwa Sara akasema, Tazama, nimempatia kaka yako vipande elfu vya fedha. Navyo ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe, na mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki.” 17 Kisha Abraham akaomba kwa Mungu, Na Mungu akamponya Abimeleki, mkewe, na watumwa wake wa kike kiasi kwamba wakaweza kupata watoto. 18 Kwa kuwa Yahwe alikuwa amewafanya wanawake wote wa nyumaba ya Abimeleki kuwa tasa kabisa, kwa sababu ya Sara, mke wa Abraham.

< Mwanzo 20 >