< Mwanzo 17 >

1 Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, “Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu. 2 Kisha nitalithibitisha agano langu kati yangu mimi na wewe, na nitakuzidisha sana. 3 Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema, 4 “Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi. 5 Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Nitaimarisha agao langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele, nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako. 8 Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao.” 9 Kisha Mungu akamwambia Abraham, “nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao. 10 Hili ndilo agano langu, ambalo utalishika, kati yangu na wewe na wazao wako baada yako: Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe. 11 Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele, na hii itakuwa ishara ya agano kati yangu mimi na ninyi. 12 Kila mwanaume wa kwenu aliye na umri wa siku nane lazima atahiriwe, katika vizazi ya watu wenu. Hii ni pamoja na yule azaliwaye katika nyumba yako na yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni yeyote ambaye si mmoja wa wazao wako. 13 Mtu ambaye amezaliwa katika nyumba yako na yule aliye nunuliwa kwa fedha yako lazima atahiriwe. Hivyo agano langu litakuwa katika mwili wenu kuwa agano la milele. 14 Mwanaume yeyote asiye tahiriwa katika mwili govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake. Amevunja agano langu.” 15 Mungu akamwambia Abraham, “kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara. 16 Nitambariki, na nitakupatia mtoto wa kiume kwake. Nitambariki, na atakuwa mama wa mataifa. Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye. 17 Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?” 18 Abraham akamwambia Mungu, “Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!” 19 Mungu akasema, Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake. 20 Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na mbili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu. 21 Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.” 22 Alipo kuwa amemaliza kuzungumza naye, Mungu akaondoka kwa Abraham. 23 Kisha Abraham akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote ambao walizaliwa katika nyumba yake, na wote ambao walinunuliwa kwa fedha yake, kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham, walitahiriwa mwili wa magovi ya ngozi ya mbele katika siku iyo hiyo, kama Mungu alivyo kuwa amesema. 24 Abraham alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele. 25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele. 26 Siku ile ile ambayo wote wawili Abraham na Ishmael mwanawe walipotahiriwa, ndipo 27 wanaume wote wa nyumba yake walitahiriwa pia, hawa ni pamoja na wale waliozaliwa katika nyumba ile na wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni.

< Mwanzo 17 >