< Mwanzo 10 >

1 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika. 2 Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi. 3 Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama. 4 Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu. 5 Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao. 6 Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani. 7 Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. 8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi. 9 Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.” 10 Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari. 11 Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala, 12 na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa. 13 Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi, 14 Wapathrusi na Wakasluhi ( ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori. 15 Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi, 16 pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi, 17 Mhivi, Mwarki, Msini, 18 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa. 19 Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha. 20 Hawa walikuwa wana wa Ham, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao. 21 Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi. 22 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu. 23 Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi. 24 Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber. 25 Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani. 26 Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27 Hadoram, Uzali, Dikla, 28 Obali, Abimaeli, Sheba, 29 Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani. 30 Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki. 31 Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao. 32 Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.

< Mwanzo 10 >