< Ezekieli 8 >

1 Hivyo ikawa kuhusu katika mwaka wa sita na mwezi wa sita, katika siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa nimeketi kwenye nyumba yangu na wazee wa Yuda waliketi mbele yangu, kwamba mkono wa Bwana Yahwe ukanijaza juu yangu huko. 2 Hivyo nikaona, na tazama, kulikuwa na mfano kama mwonekano wa mwanadamu. Kutoka kwenye mwonekano wake wa nyonga kwenda chini kulikuwa na moto. Na kutoka kwenye nyonga kwenda juu kulikuwa na mwonekano wa kitu kinachong'aa, kama mng'ao wa chuma. 3 Kisha akanyoosha kutoka kwenye mkono na kunichukua kwa nywele za kichwa changu; Roho akaniacha juu kati ya dunia na mbingu, na katika maono kutoka kwa Mungu, akaniletea hata Yerusalemu, kwenye mlango wa kuingia ndani ya lango la kaskazini, ambako sanamu ile iletayo wivu mkubwa ilipokuwa imesiamama. 4 Kisha tazama, utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa huko, kulingana na ono nililokuwa nimeliona kwenye uwanda. 5 Kisha akanambia, “Mwanadamu, inua juu macho yako kwenda upande wa kaskazini.” Hivyo nikainua macho yangu kuelekea kaskazini, na kwenye lango la kaskazini kulekea kwenye madhabahu, huko kwenye lango la kuingilia, kulikuwa na sanamu ya wivu. 6 Hivyo akanambia, “Mwanadamu, unaona wanayoyafanya? Haya ni machukizo makubwa ambayo nyumba ya Israeli wanayoyafanya hapa kunifanya niende mbali kutoka patakatifu pangu. Lakini utageuka na kuona machukizo makubwa zaidi.” 7 Kisha akanileta hata kwenye mlango wa uzio, na nikatazama, kulikuwa na shimo kwenye ukuta.” 8 Akanambia, “Mwanadamu, chimba kwenye huu ukuta.” Basi nikachimba kwenye huo ukuta, na kulikuwa na mlango. 9 Kisha akanambia, “Nenda na ukaone machukizo ya uovu ambayo wanayoyafanya hapa.” 10 Basi nilipokuwa nikienda ndani na nikaona, na tazama! Kulikuwa na kila umbo la vitu vikitembea polepole na mnyama achukizaye sana! Kila sanamu wa nyumba ya Israeli ilikuwa imechongwa kwenye ukuta pande zote. 11 Wazee sabini wa wa nyumba ya Israeli walikuwa huko, na Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama katikati yao. Walikuwa wamesimama mbele ya picha, na kila mtu alikuwa na chetezo kwenye mkono wake ili kwamba harufu ya ubani ingeweza kupanda juu. 12 Akanambia, “mwanadamu, unaona kile ambacho wazee wa nyumba ya Israeli wanachokifanya kwenye giza? Kila mmoja hufanya hivi kwenye chumba cha sanamu yake, kwa kuwa husema, 'Yahwe hatuone! Yahwe ameitelekeza hii nchi.”' 13 Kisha akanambia, “Geuka tena na tazama machukizo makubwa ambayo wanayoyafanya.” 14 Tena akanileta kwenye lango la kuingia la nyumba ya Yahwe lililokuwa upande waa kaskazini, na tazama! Wanawake walikuwa wameketi huko wakimlilia Tamuzi. 15 Hivyo akanambia, “Umeiona hii, mwanadamu? Geuka tena na uone machukizo makubwana zaidi kuliko hayo.” 16 Akanileta hata kwenye uzio wa ndani wa nyumba ya Yahwe, na tazama! huko kwenye lango la kuingia kwenye madhabahu, kulikuwa na takribani watu ishirini na tano waliokuwa wamelipa mgongo hekalu la Yahwe na nyuso zao kuelekea mashariki, na walikuwa wakiabudu jua. 17 Akanambia, “Unaona hii, mwanadamu? Je ni kitu kidigo kwa ajili ya nyumba ya Yuda kufanya haya machukizo wanayoyafanya? Kwa kuwa wameijaza nchi kwa uovu na wamerudi tena ili kuniletea hasira, kuweka tawi kwenye pua zao. 18 Hivyo nitatenda miongoni mwao pia; jicho langu halitakuwa na huruma, sitaacha kuwaharibu. hata watalia kwenye masikio yangu kwa sauti kubwa, sitawasikia.”

< Ezekieli 8 >