< Ezekieli 45 >

1 Wakati mtakapogawanya nchi kama urithi, mtafanya sadakwa kwa Yahwe; sadaka hiyo itakuwa sehemu takatifu ya nchi, dhiraa elfu ishirini na tano urefu, na dhiraa elfu kumi upana. Patakuwa patakatifu, ndani ya mipaka yake yote. 2 Kutoka hapa kutakuwa na dhiraa mia tano kwa dhiraa mia tano za mraba kuzunguka mahali patakatifu, kwa kuuzunguka mpaka dhiraa hamsini upana. 3 Kutoka hili eneo utapima fungu ambalo ni dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana; patakuwa patakatifu; mahali patakatifu palipo tukuka. 4 Patakuwa patakatifu katika nchi kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Yahwe, ajaye kwa Yahwe kumtumikia. Patakuwa mahali kwa ajili ya nyumba na eneo takatifu kwa ajili mahali patakatifu. 5 Hivyo itakuwa dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana, patakuwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaotumika kwenye nyumba. 6 Mtadhihirisha eneo moja kwa ajili ya mji, dhiraa elfu tano na urefu ishirini na tano, hapo patakuwa kando kando ya eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu; huu mji utakuwa wa mali ya nyumba yote ya Israeli. 7 Nchi ya mwana mfalme itakuwa kwa pande zote za eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu na mji. Patakuwa kwa upande wao wa magaharibi na upande wa mashariki. Urefu utalingana na urefu wa moja ya hayo mafungu, kutoka magaribi hata mashariki. 8 Hii nchi itakuwa mali ya mwana mfalme katika Isaraeli. Wana wafalme hawatawakandamiza watu wangu; badala yake, watawapatia nchi kwa nyumba ya Israeli, kwa ajili ya makabila yao. 9 Bwana Yahwe asema hivi: Inatosha kwa ajili yenu, mwana mfalme wa Israeli! Ondoa dhuluma na mgogoro; fanya hukumu na haki! Usiwafukuze wapangaji wa watu wangu! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. 10 Mtakuwa na mzani sahihi, efa sahihi, na bathi sahihi! 11 Efa na bathi zitakuwa kiasi kile kile, ili kwamba bathi iwe zaka ya homeri; efa itakuwa zaka ya hamori moja. Vipimo vyao vitakuwa vinafanana na homeri. 12 Shekeli zitakuwa gera ishirini, shekeli sita zitakuwa mane yenu. 13 Hili ndilo toleo mtakalotoa: efa sita kwa kila homeri ya ngano, na mtatoa efa sita kwa kila homeri ya shayiri. 14 Sadaka ya kawaida ya mafuta itakuwa zaka ya bathi kwa kila kori (ambazo ni bathi), au kwa kila hamori, kwa kuwa hamori moja ni bathi kumi pia. 15 Kondoo mmoja au mbuzi kutoka mifugo kwa kila wanyama mia mbili kutoka malisho ya maji ya mikoa ya Israeli yatatumika kwa sadaka ya kuteketezwa yoyote au sadaka ya amani kufanya upatanisho kwa ajili ya watu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. 16 Watu wote wa nchi watatoa hii sadaka kwa mwana mfalme wa Israeli. 17 Utakuwa wajibu wa mwana mfalme kutoa wanyama kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka ya unga, sadaka ya kinywaji, katika siku za sikukuu na sherehe za mwezi mpya, na katika siku za Sabato-sikukuu zote za kudumu za nyumba ya Israeli. Ataandaa kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za unga, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani kwa ajili ya upatanisho badala ya nyumba ya Israeli. 18 Bwana Yahwe asema hivi: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utachukua ng'ombe mmoja asiyekuwa na dosari kutoka kwenye kundi na kufanya sadaka ya dhambi kwa ajili ya patakatifu. 19 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi na kuiweka juu ya miimo ya mlango na kwenye pembe nne za mpaka wa madhabahu, na miimo ya lango la uzio wa ndani. 20 Utafanya hivyo siku ya saba ya mwezi kwa dhambi ya kila mtu kwa ajali au ujinga; katika njia hii mtaipatanisha hekalu. 21 Katika siku ya mwezi siku ya kumi na nne ya mwezi, mtakuwa na sikukuu, sikukuu ya siku saba. Matakula makate usiotiwa chachu. 22 Siku hiyo, mwana mfalme ataandaa ng'ombe kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wote wa nchi kama sadaka ya dhambi. 23 Kwa siku saba za sikukuu, mwana wa mfalme ataandaa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Yahwe: ng'ombe saba na kondoo dume saba zisizokuwa na dosari kila siku kwa mda wa siku saba, na mbuzi dume kila siku kama sadaka ya dhambi. 24 Kisha mwana mfalme atatengeneza sadaka ya chakula ya efa moja kwa kila ng'ombe na efa moja kwa kila kondoo dume pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa. 25 Katika siku ya saba ya mwezi siku ya kumi na tano ya mwezi, katika sikukuu, mwana wa mfalme atafanya matoleo katika siku hizi saba: sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za chakula, na sadaka za mafuta.

< Ezekieli 45 >