< Ezekieli 22 >

1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema, 2 “Sasa wewe, mwanadamu, Je! Utanihukumu? Utauhukumu mji kwa damu? Mfanye ajue machukizo yake yote. 3 Utasema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Huu ndiyo mji umbao umwagao damu kati yake ili kwamba mda wake ufike; mji ufanyao sanamu ili ujitie unajisi. 4 Umekuwa na hatia kwa damu uliyoimwaga, na kufanya unajisi kwa sanamu ulizozitengeneza. Kwa kuwa umezileta karibu siku zako na kuzikaribia siku zako za mwisho. Kwa hiyo nitakufanya lawama kwa mataifa na kejeli katika uso wa kila nchi. 5 Wote walio karibu na wale walio mbali nawe watakudhihaki, wewe mji mchafu, ujulikanao kila mahali kwa sifa mbaya kama kujaa machafuko. 6 Tazama! Wakuu wa Israeli, kila mmoja kwa nguvu yake, wamekuja kwako kumwaga damu. 7 Wamefanya udanganyifu kwa baba na mama ndani yako, na wametenda yaliyo kinyume juu ya wageni kati yako. Wamewatenda vibaya yatima na wajane ndani mwako. 8 Umevidharau vitu vyangu vitakatifu na kuinajisi Sabato yangu. 9 Watu wasingiziaji wamekuja kati yako ili kumwaga damu, na hula juu ya milima. Hufanya uovu kati yako. 10 Uchi wa baba umefunuliwa ndani yako. Wamemtukana mwanamke mchafu ndani yako wakati wa uchafu wake. 11 Watu waliofanya machukizo pamoja na wake za majirani zao, na watu wafanyao uchafu wa aibu kwa mke wa mwanao mwenyewe; watu wawatukanao dada zao wenyewe-binti za baba zao wenyewe-haya yote yapo miongoni mwanu. 12 Hawa watu huchukua rushwa kati yenu ili kumwaga damu. Umechukua faida na kuongeza riba nyingi sana, na umenisahau-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. 13 Tazama! Kwa mkono wangu nimeipiga faida ambayo uliyoitengeneza kwa njia isiyo halali, na damu iliyo kati yako. 14 Je! Moyo wako utasimama, mikono yako itakuwa hodari katika siku wakati mimi mwenyewe nitakapo kushughulikia? Mimi, Yahwe, nasema hivi, na nitalifanya. 15 Hivyo nitakutawanya kati ya mataifa na kukutawanya kati ya nchi mbali mbali. Katika njia hii, nitausafisha uchafu kutoka kwako. 16 Hivyo utakuwa mchafu machoni mwa mataifa. Kisha utajua kwamba mimi ni Yahwe.”' 17 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema, 18 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa takataka kwangu. Wote wamekuwa masazo ya shaba na bati, na chuma na risasi kati yenu. Watakuwa kama takataka ya fedha katika tanuu. 19 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu mmekuwa kama takataka, kwa hiyo, tazama! Nataka kuwakusanya katikakati ya mji wa Yerusalemu. 20 Kama kukusanya fedha na shaba, chuma, risasi na chuma kati ya tanuu ili kuvifukutia moto na kuviyeyusha juu yake, nitawayeyusha. Hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu. Nitawaweka hapo na kufukutisha moto juu yake ili kuiyeyusha; hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu, na nitawaweka hapo na kuwayeyusha. 21 Basi nitawakusanya na kuwafukutia kwa moto wa hasira yangu juu yenu hivyo basi mtamwagwa kati yake. 22 Kama kuyeyusha fedha kati ya tanuu, mtayeyushwa chini kati yake, na mtajua yakwamba mimi, Yahwe, nimemwaga ghdhabu yangu juu yenu!”' 23 Neno la Yahwe likanijia, kusema, 24 “Mwanadamu, mwambie, 'Wewe ni nchi ambayo haijasafishwa. Hakuna mvua siku ya hasira! 25 Kuna njama ya manabii wake kati yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo. Wamekula uhai na kuchukua utajiri wa thamani; wamewafanya wajane wengi ndani yake! 26 Makuhani wake hufanya kinyume na sheria yangu, na wamevinajisi vitu vyangu vitakatifu. Hawawezi kutofautisha kati ya vitu vitakatifu na vitu vya najisi. Wanaficha macho yao kutoka Sabato zangu hivyo basi nimetiwa unajisi kati yao. 27 Wakuu wake ndani mwake wamekuwa kama mbwa mwitu wakirarua mawindo yao. Wamemwaga damu na kuharibu maisha, ili kupata faida kwa njia ya udanganyifu. 28 Manabii wake wamepakwa chokaa; wanaona maono ya uongo na kutabiri uongo kwao. Wanasema “Bwana Yahwe asema hivi”' wakati Yahwe hajanena. 29 Watu wa nchi wamewakandamiza kwa kutaka kwa nguvu na kuwanyang'anya kwa nguvu, na wamewatesa maskini na wahitaji, na kuwakandamiza wageni bila haki. 30 Hivyo nimetafuta mtu kutoka kwao ambaye ataweza kujenga ukuta na ambaye atakayeweza kusimama mbele yangu katika uvunjaji wake kwa ajili ya nchi basi sitaweza kuiharibu, lakini sikuona mtu. 31 Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao. Nitawamaliza kwa moto wa ghadhabu yangu na kuweka njia yao juu ya vichwa vyao wenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'

< Ezekieli 22 >