< Kutoka 26 >

1 Lazima ufanye hiyo maskani iwe na mapazia kumi ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi. Kazi ya fundi stadi. 2 Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne. Mapazia yote yatakuwa ya kipimo kimoja. 3 Mapazia matano yataungwa pamoja, na mapazia matano mengine yataungwa pamoja. 4 Lazima ufanye tanzi za rangi ya samawati upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake. Vivyo hivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili. 5 Fanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upande wa mwisho wa ile pazia iliyo katika kuungana kwa pili. 6 Fanya hivi ili hizo tanzi zielekeana. Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganisha hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo na hiyo maskani itakuwa ni moja. 7 Lazima ufanye mapazia ya nywele za mbuzi yawe hema juu ya maskani. Lazima ufanye mapazia kumi na moja. 8 Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne. Hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja. 9 Lazima utaunganisha mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalikunja hapo upande wa mbele wa ile hema. 10 Ufanye tanzi hamsini upande wa mwisho wa pazia lile lililo la mwisho katika hayo yaliyounganywa pamoja, na tanzi hamsini upande wa mwisho wa lile pazia lililo nje katika hayo ya pili yaliyounganywa pamoja. 11 Kisha ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja. 12 Kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani. 13 Lazima kuwe na dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili - ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika. 14 Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo. 15 Nawe lazima ufanye hizo fremu za maskani za mti wa mjohoro. 16 Kila fremu utakuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wake kila ubao utakuwa dhiraa moja na nusu. 17 Kila fremu itakuwa na ndimi mbili, zenye kuunganishwa huu na huu. Ndivyo utakavyozifanya mbao zote za maskani. 18 Kisha ufanye zile mbao za maskani, mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini. 19 Lazima nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile fremu ishirini. Vitako viwili chini ya fremu moja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya fremu nyingine kupokea zile ndimi zake mbili. 20 Kwa upande wa pili wa maskani, upande wa kaskazini, mbao ishirini 21 na vitako vyake vya fedha arubaini. Lazima kuwe na vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya fremu nyingine. 22 Ufanye fremu sita kwa ajili ya upande wa nyuma wa maskani kuelekea magharibi. 23 Tena ufanye fremu mbili kwa ajili ya hizo pembe za maskani zilizo upande wa nyuma. 24 Hizi fremu zitakuwa zimetengana upande wa chini, lakini zimeshinkana kwa juu ya duara moja. 25 Fremu zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha. Vitako kumi na sita, vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili. 26 Lazima ufanye mataruma ya mti wa mshita- mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani, 27 na mataruma matano kwa ajili ya fremu za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya fremu za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi. 28 Na hilo taruma la katikati lililo katikati ya zile fremu, litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu. 29 lazima uzifunuke hizo fremu kwa dhahabu. Nawe lazima ufanye maduara yake ya za dhahabu, kuwa kama vishikizo, na hayo mataruma utayafunika dhahabu. 30 Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani. 31 Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi. 32 Kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne. 33 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda. Lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana. 34 Nawe lazima utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. Na ile meza utaiweka nje ya pazia. 35 Lazima uweke kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini. Lile meza utaiweka upande wa kaskazini. 36 Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa hema, cha nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji wa taraza. 37 Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu. Nawe utasubu vitako vya shaba vitano kwa ajili yake.

< Kutoka 26 >