< Kutoka 25 >

1 Yahweh akamwambia Musa, 2 “Waambie Waisraeli wanitolee sadaka kila mtu nawe utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu. Lazima upokee hizi sadaka kwa ajili yangu. 3 Hizi ndio sadaka utakazopokea kwao; dhahabu, fedha na shaba, 4 buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na manyoya ya mbuzi; 5 na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, miti ya mjohoro, 6 mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; 7 mawe ya shohamu na mawe mengine ya kutiwa kwa ile naivera na kwa kile kifuko cha kifuani. 8 Waache wanifanyie patakatifu ili nipate kukaa kati yao. 9 Lazima ufanye sawa na haya yote nikuoneshayo mfano wa maskani, na vifaa vyake, ndivyo utakavyovifanya. 10 Wana paswa wafanye sanduku la mti wa mjohoro. Urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu; na upana wake moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. 11 Lazima ulifunike nadni kwa dhahabu safi, na utie na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. 12 Nawe uta yayusha katika viduara vinne vya dhahabu, na kuviweka katika miguu yake minne; viduara viwili upande mmoja, na viduara viwili upande wake wa pili. 13 Nawe lazima ufanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu. 14 Nawe lazima uweka hiyo miti katika vile viduara vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku. 15 Hiyo miti itakaa katika vile viduara vya sanduku; haitaondolewa. 16 Kisha weka ndani ya sanduku hizo amri nitakazokupa. 17 Nawe lazima utengeneze kifuniko cha dhahabu safi. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu katika hiyo miisho miwili ya kiti cha rehema. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja wa kiti cha rehema, na kerubi la pili mwisho wa pili. Lazima hao makerubi wawe kitu kimoja na kiti cha rehema. 20 Na hao makerubi watainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao. Nyuso zao makerubi zitaelekeana na zitaelekea kiti cha rehema. 21 Lazima uweke kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha uwe hizo amri nitakazokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo katika sanduku. Nitazungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema. Itakuwa katikati ya hao makerubi mawili waliyo juu ya sanduku la ushuhuda nitakapo zungumza na wewe katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. 23 Nawe fanya meza ya mti wa mshiti. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. 24 Uifunike dhahabu safi na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote. 25 Lazima ufanyie fremu ya kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, ukingo wa dhahabu wa kuuzunguka fremu pande zote. 26 Uifanyie viduara vinne vya dhahabu na kuvitia vile viduara katika pembe zake nne, katika miguu yake minne ilipo kuwa. 27 Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza. 28 Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo. 29 Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia. Vifanye vyote vya dhahabu safi. 30 Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima. 31 Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho. 32 Nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake - matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili. 33 Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara. 34 Katika hicho kinara, lazima kuwe na vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake. 35 Lazima kuwe na tovu chini ya matawi - mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara. 36 Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho, kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi. 37 Lazima nawe uzifanye hivyo vinara saba na taa zake saba, nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake. 38 Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi. 39 Tumia talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote. 40 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.

< Kutoka 25 >