< Kutoka 24 >

1 Kisha Yahweh akamwabia Musa, “Njoo juu kwangu -wewe, Aruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli, na kuniabudu kwa mbali. 2 Musa peke yake anaweza kuja karibu yangu. Wengine hawapaswi kuja karibu, wala watu kuja juu na yeye.” 3 Musa akaenda juu na kuwaambia watu maneno yote ya Yahweh na amri zake. Watu wote wakajibu kwa sauti moja na kusema, “Tutafanya maneno yote Yahweh aliyo tuamuru.” 4 Kisha Musa akaandika chini maneno yote ya Yahweh. Asubui mapema, Musa akajenga madhabahu chini ya mguu wa mlima na kupanga nguzo kumi na mbili za mawe, ili mawe yawakilishe makabila kumi na mbili ya Israeli. 5 Aliwatuma vijana Wakiisraeli kutoa sadaka ya kuteketeza na kutoa dhabihu za ng'ombe za sadaka ya ushirika kwa Yahweh. 6 Musa allichukuwa nusu ya damu na kuweka kwenye mabeseni; alinyunyuzia nusu ingine kwenye madhabahu. 7 Alichukuwa kitabu cha agano na kuwasomea kwa nguvu watu. Walisema, “Tutafanya yote Yahweh aliyo sema. Tutakuwa watiifu.” 8 Kisha Musa akachukuwa damu na kunyunyiza kwa watu. Alisema, “Hii ni damu ya agano Yahweh alilo lifanya nanyi kwa kuwapa hii ahadi kwa maneno yote haya.” 9 Kisha Musa, Aruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli wakaenda juu ya mlima. 10 Walimuona Mungu wa Israeli. 11 Chini ya miguu yake kulikuwa na sakafu iliyo jengwa kwa jiwe la yakuti samawi, safi kama mbingu yenyewe. Mungu hakugusa na mkono kwa hasira viongozi Waisraeli. Walimuona Mungu, na wakanywa na kula. 12 Yahweh akamwambia Musa, “Njoo juu kwangu mlimani na ubaki pale. Nitakupa saani za mawe na sheria na amri nilizo ziandika, ili uwafundishe.” 13 Hivyo Musa akaenda na msaidizi wake Yoshua na kwenda juu mlima wa Mungu. 14 Musa akawaambia wazee, “Baki hapa na mtusubiri hadi tutakapo warudia. Aruni na Huri wapo nanyi. Kama kuna mtu mwenye malalamiko, acha awaende.” 15 Hivyo Musa akaenda juu ya mlima, na wingu likafunika. 16 Utukufu wa Yahweh ukabaki juu ya Mlima wa Sinai, na wingu likafunika kwa siku sita. Siku ya saba alimuita Musa kutoka ndani ya wingu. 17 Utukufu wa Yahweh ulikuwa kama moto ulao juu ya mlima kwenye macho ya Waisraeli. 18 Musa akaingia kwenye wingu na kwenda juu ya mlima. Alikuwa mlimani siku arobaini na usiku arobaini.

< Kutoka 24 >