< Torati 1 >

1 Haya ni maneno ambayo Musa aliyasema kwa Israeli wote ng'ambo ya jangwa la Yordani, katika tambarare ya mto wa Yordani juu ya Suph, katikati mwa Paran, Topheli, Laban, Hazeroth, na Di Zahab. 2 Ni safari ya siku kumi na moja toka Horabu kupitia njia ya mlima wa Seir kwenda Kadeshi Barnea. 3 Ilitokea kwenye mwaka wa nne, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa alizungumza kwa watu wa Israeli, kuambia yote yale Yahwe aliyomwamuru kuhusu wao. 4 Hii ilikuwa baada ya Yahwe kumvamia Sihoni mfalme wa Amoria, ambaye aliishi huko Heshboni, na Ogi mfalme wa Bashani, ambaye aliishi huko Ashtarothi ya Edrei. 5 Ng'ambo ya Yordani, katika nchi ya Moabu, Musa alianza kutangaza maelekezo haya, akisema, 6 “Yahwe Mungu wetu alisema nasi huko Horebu, akisema, umeishi vya kutosha katika milima ya nchi hii. 7 Geuka na uanze safari yako, na uende kwenye nchi ya milima ya Amorites, na kwenye maeneo yote karibu na tambarare ya mto Yordani, katika nchi ya milima, na nyanda za chini, huko Negev, na pwani - nchi ya Wakanani na huko Lebanoni mbali ya mto mkuu wa Euphratesi. 8 Tazama, nimetenga nchi kwa ajili yako, nenda ndani na umiliki nchi ambayo Yahwe aliapa kwa baba zako, Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kuwapa na uzao wao baada yao. 9 Nilisema nawe kwa wakati huo, nikisema, siwezi nikakubeba peke yangu, 10 Yahwe Mungu wako amekuzidisha, na tazama, leo umekuwa umati wa nyota angani. 11 Yahwe aweza, Mungu wa baba zako, kukufanya wewe mara elfu moja zaidi ya ulivyo, na kukubariki, kama alivyokuahidi! 12 Lakini inawezekanaje mimi peke yangu kubeba shehena zako, mizigo yako, na migogoro yako? 13 Chukua wanaume wa hekima, wanaume waelewa, na wanaume walio na sifa nzuri toka kila kabila, nitawafaya kuwa vichwa juu yenu. 14 Mlinijibu na kusema, 'Jambo ulilolisema ni zuri kwetu kufanya.' 15 Kwa hiyo nilichukua vichwa vya makabila yenu, wanaume wa hekima, na wanaume wenye sifa nzuri, na nikawafanya kuwa vichwa juu yenu, jemedari kwa elfu, jemedari kwa hamsini, jemedari kwa kumi, na maakida, kabila kwa kabila. 16 Niliwaamuru waamuzi wenu kwa wakati huo, kusema, 'Zikiliza mabishano kati ya ndugu zenu, na muhukumu ya haki kati ya ndugu na ndugu zake, na mgeni aliye pamoja naye. 17 Hamtaonesha upendeleo kwa yeyote katika mgogoro, mtasikia madogo na makubwa pia. Hamtaogopa uso wa mtu, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Migogoro iliyo migumu kwenu, mtaniletea mimi, na mimi nitaisikiliza. 18 Niliwaamuru kwa wakati huo mambo yote mtakayofanya. 19 Tulisafiri toka Horebu na kwenda kupitia jangwa lile kubwa lote na lenye kutisha lile mliloliona, katika njia yetu kuelekea nchi ya milima huko Amorites, kama Yahwe Mungu wetu alivyotuamuru sisi, na tukaja Kadeshi ya Barnea. 20 Niliwambia, mmekuja kwenye nchi ya milima ya Amorites, ambayo Yahwe Mungu wetu anatupa sisi. 21 Tazama, Yahwe Mungu wenu amekwisha weka nchi mbele yenu; nenda juu, muimiliki, kama Yahwe, Mungu wa baba zenu, amekwisha zungumza nanyi, msiogope wala kukata tamaa. 22 Kila moja wenu alikuja kwangu na kusema, 'Basi tutume watu mbele yetu, ili kwamba waweze kupepeleza nchi kwa ajili yetu, na kutuletea sisi neno kuhusiana na njia ya wapi tuvamie, na kuhusiana na miji tutakayoingia. 23 Shauri hilo lilinibariki mimi, 'Nilichukua watu kumi na mbili kutoka kwenu, mtu moja kwa kila kabila. 24 Waligeuka na kwenda juu ya nchi ya milima, kufika kwenye bonde la Eshcol na kufanya upepelezi wa kina. 25 Walichukua baadhi ya mazao ya ardhi mikononi mwao na kuleta kwetu, Pia walileta neno na kusema, 'Ni nchi nzuri ambayo Yahweh Mungu wetu anatupa sisi' 26 Bado mlikataa kushambulia, lakini mliasi dhidi ya amri ya Yahwe Mungu wenu. 27 Mlilalamika katika mahema yenu na kusema, “Ni kwa sababu Yahwe alituchukia sisi kwa kuwa ametutoa katika nchi ya Misri, kuteweka katika mikono ya Amorites kutuangamiza. 28 Tuende wapi sasa? Ndugu zetu wamefanya mioyo yetu kuyeyuka, kusema, Hao watu ni wakubwa na warefu zaidi yetu, miji yao ni mikubwa na imeimarishwa kwenda mbinguni; zaidi ya yote, tumewaona wana wa Anakim huko” 29 Kisha nikasema nao, msitishwe wala msiwaogope. 30 Yahwe Mungu wenu, ambaye aenda mbele yenu, atawapigania, kama yote aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu, 31 na pia katika jangwa, ambapo mmekwisha muona Yahwe Mungu wenu jinsi alivyowabeba, kama mtu abebavyo mtoto wake, kokote mlikoenda mpaka kufika hapa.' 32 Bado licha ya neno hili hakumwamini Yahwe Mungu wenu, 33 aliyeenda mbele yenu kwenye njia kutafuta eneo kwa ajili yenu kuweka kambi, katika moto kwa usiku, katika mawingu kwa mchana. 34 Yahwe alisikia sauti ya maneno yenu na alikasirika; aliapa na kusema, 35 Hakika hakuna mmoja ya hawa watu wa kizazi hiki kiovu wataona nchi nzuri ambayo niliapa kuwapa babu zao, 36 kasoro Kalebu mwana wa Jephuneeh; yeye ataiona. Yeye nitampa nchi ambayo amekwisha kuikanyanga, na watoto wake, kwa sababu alimfuata Yahwe kwa ukamilifu.' 37 Pia Yahweh alinikasirikia mimi kwa sababu yenu, kusema, 'Wewe pia hautaingia huko, 38 Yoshua mwana wa Nuh, ambaye amesimama mbele yako, yeye ataingia, mtie moyo, kwani yeye atawaongoza Israeli kuimiliki. 39 Zaidi ya yote, watoto wenu wadogo, ambao mlisema watakuwa waathirika, ambao leo hawana elimu ya uzuri au ubaya-wataenda ndani huko. Wao nitawapa nchi hiyo, na wataimiliki. 40 Lakini ninyi, geuka na muuanza safari kwenda jangwani kwa kuambaa njia ya bahari ya mianzi'. 41 Kisha mlinijibu na kusema kwangu, 'Tumetenda dhambi dhidi ya Yahwe, tutaenda juu na kupigana, tutafuata yote ambayo Yahwe Mungu wetu ametuamuru sisi kufanya'. Kila mtu miongoni mwenu aliweka silaha za vita, na mlikuwa tayari kuvamia nchi ya milima. 42 Yahwe alisema nami, 'Waambie, msivamie na kupigana, kwa kuwa sitakuwa pamoja nanyi, na mtashindwa na adui zenu'. 43 Nilizungumza nanyi kwa njia hii, lakini hamkunisikiliza, Mliasi dhidi ya amri ya Yahwe, mlikuwa wenye kiburi na mlivamia nchi ya milima. 44 Lakini Amorites, ambayo waliishi katika nchi hiyo ya milima, walitoka dhidi yenu na kuwafukuza kama nyuki, na kuwapiga chini huko Seir, mbali kama Hormah. 45 Mlirudi na kulia mbele ya Yahwe; lakini Yahwe hakusikiliza sauti zenu, wala hakuwa makini kwenu. 46 Kwa hiyo mlibaki Kadeshi siku nyingi, siku zote mlibaki huko.

< Torati 1 >