< Torati 4 >

1 Sasa, Israeli, sikiliza sheria na amri ambayo niko karibu kukufundisha, kuzifanya, ili kwamba uweze kuishi na kuingia ndani na kumiliki nchi ambayo Yahwe, Mungu wa baba zako, anakupa. 2 Hautaongeza maneno ambayo nakuamuru, wala hautayapunguza, ili kwamba uweze kushika amri ya Yahwe Mungu wako ambazo naenda kukuamuru. 3 Macho yako yamekwisha ona nini Yahwe alifanya kwa sababu ya Baal Peor, kwa kuwa watu wote waliomfuata Baali Peor, Yahwe Mungu wenu amekwisha kuwaangamiza kutoka miongoni mwenu. 4 Lakini walioambatana na Yahwe Mungu wenu wako hai leo, kila moja wenu. 5 Tazama, nimewafundisha sheria na amri, kama Yahwe Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ila kwamba mfanye hivyo katikati mwa nchi ambayo mnaiendea ili kusudi muimiliki. 6 Kwa hiyo washikilieni na kuwafanya, kwa kuwa hii ni hekima yenu na uelewa wenu mbele ya macho ya watu watakaosikia amri hizi zote na kusema, “Hakika taifa hili kubwa lina watu wa hekima na uelewa.' 7 Kuna taifa gani jingine la vile liko hapo lina mungu karibu nao, kama Yahwe Mungu wetu tunapomwita wakati wowote? 8 Kuna taifa kubwa gani jingine liko hapo ambalo lina sheria na amri ili kwamba haki pamoja na sheria ambayo ninaweka mbele yenu leo? 9 Zingatia peke na kuwa makini kujilinda, ili usisahau mambo ambayo macho yako yameona, ili kwamba yasiuwache moyo wako kwa siku zote za maisha yako. Badala yake, yafanye yajulikane kwa watoto wako na wana watoto wako. 10 Kuhusu siku ile uliyosimama mbele ya Yahwe Mungu wako katika Horeb, wakati Yahwe alisema nami, 'Nikusanyie watu, na nitawafanya wasikia maneno yangu, ili kwamba waweze kujifunza kuniogopa mimi siku zote ambazo wanazoishi duniani, na kwamba waweze kuwafundisha watoto wao. 11 Mlikuja karibu na kusimama katika wayo wa mlima. Mlima uliwaka moto kwenye moyo wa mbinguni, pamoja na giza, mawingu na giza jembamba. 12 Yahwe alizungumza katikati ya moto, ulisikia suati pamoja na maneno yake, lakini hakuona umbo, ila ulisikia sauti peke. 13 Alitangaza kwenu agano lake ambalo aliwaamuru ninyi kulifanya, amri kumi. Aliziandika kwenye vibao viwili vya mawe. 14 Yahwe aliniamuru mimi kwa wakati huo kuwafundisha sheria na amri, ili kwamba muweze kuzifanya katika nchi mnaoivuka kwenda kuimiliki. 15 Basi iweni waangalifu ninyi wenyewe - kwa kuwa mliona hakuna namna ya umbo siku hiyo ambapo Yahweh alizungumza nanyi huko Horeb kutoka katikati mwa moto, 16 ili kwamba usiharibike na kuchonga umbo katika sura ya kiumbe chochote, umbo la mwanaume au mtu wa kike, 17 au sura ya mnyama aliye katika nchi, au sura ya ndege yoyote wa mabawa arukae katika anga, au 18 sura ya kitu chochote kitambaacho katika ardhi, au sura ya samaki yoyote katika maji chini ya ardhi. 19 Hautainua macho yako juu mbinguni na kutazama jua, mwezi, au nyota - jeshi lote la mbinguni- ukusogezwa na kuviabudu na kuvisujudia- vile vyote ambavyo Yahwe Mungu wenu amewapa hisa watu wote walio chini ya anga lote. 20 Lakini Yahwe amewatoa ninyi na kuwaleta nje ya tanuru la chuma, nje ya Misri, kuwa kwake watu wa urithi wake, kama mlivyo leo. 21 Yahwe alinikasirikia mimi kwa sababu yenu; aliapa kwamba nisiende ng'ambo ya Yordani, na kwamba nisiende kwenye nchi nzuri, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ninyi kama urithi. 22 Badala yake, ninapaswa kufa katika nchi hii, sipaswi kwenda ng'ambo ya Yordani, lakini mtaenda ng'ambo na kuimiliki nchi nzuri 23 Zingatia ninyi wenyewe, ili kwamba msisahau agano la Yahwe Mungu wenu, alilolifanya pamoja nanyi, na kujichongea mfano wa sanamu katika uombo la kitu chochote ambacho Yahwe Mungu wenu amewakataza kufanya. 24 Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ni moto ulao, Mungu wa wivu. 25 Wakati mnapozaa watoto na wana watoto, na wakati mtakapo kuwa katika nchi kwa muda mrefu, na kama mtaharibikiwa ninyi na kuchonga umbo la umbo lolote, na kufanya uovu machoni pa Yahwe Mungu wenu, kumchoche katika hasira- 26 Nitaita nchi na mbingu kushuhudia dhidi yenu leo kwa kuwa mapema kabisa mtaangamia kutoka katika nchi ambayo mnaiendea huko ng'ambo ya Yordani kuimiliki, hamtazidisha siku zenu ndani yake, lakini mtaangamizwa kabisa. 27 Yahwe atawatawanyisha ninyi miongoni mwa watu, na mtabaki wachache ki-idadi miongoni mwa mataifa, ambapo Yahwe atawaongoza mbali. 28 Huko mtatumikia miungu mingine, kazi ya mikono ya watu, mbao na mawe, ambayo wala haioni, kusikia, wala kunusa. 29 Lakini kuanzia hapo mtamtafuta Yahwe Mungu wenu, na mtampata, wakati mtakapomtafuta kwa moyo wenu wote na roho zenu zote. 30 Wakati mnakuwa katika dhiki, na wakati haya yote yatakuwa yamekuja kwenu, katika siku za badae mtamrudia Yahwe Mungu wenu na kusikia sauti yake. 31 Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ni Mungu wa rehema; hatawaangusha wala kuwaangamiza ninyi, wala kusahau agano la baba zenu ambalo aliapa kwao. 32 Kwa ajili ya kuuliza sasa kuhusu siku zilizopita ambazo zilikuwa mbele yenu: tangu siku ile ambayo Mungu alimuumba mtu katika nchi, kutoka pande moja ya mbingu hadi nyingine, uliza kama kumekuwepo chochote kama hiki kikubwa, au chochote kama hicho imewahi kusikiwa? 33 Ilishawahi kutokea watu kusikia sauti ya Mungu kuongea katikati ya moto, kama mlivyosikia, na kuishi? 34 Au Mungu ameshawahi kujaribu kwenda na kujichukulia kwa ajili yake taifa kutoka miongoni mwa taifa, kwa majaribu, ishara na maajabu na kwa vita, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoshwa, na magaidi wakuu, vile vyovyote ambavyo Yahwe Mungu wenu alifanya kwa ajili yenu Misri mbele ya macho yenu? 35 Kwenu haya yalioneshwa, ili muweze kujua kuwa Yahwe ni Mungu, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake. 36 Toka mbinguni alifanya msikie sauti yake, ili kwamba aweze kuwaelekeza, juu ya nchi aliwafanya muone moto wake mkuu, mlisikia maneno yake toka katikati ya moto. 37 Kwa sababu aliwapenda baba zenu, alichagua wazao wao baada yao, na kuwatoa ninyi Misri kwa uwepo wake, kwa nguvu yake kubwa, 38 ili kusudi awatowe kutoka mbele ya mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi, kuwaleta ndani, kuwapa ninyi nchi yao kama urithi, hivi leo. 39 Tambua hivi leo, weka kwenye moyo wako, Yahwe ni Mungu juu ya mbingu na chini ya dunia, hakuna mwingine yeyote. 40 Mtazishika sheria zake na amri zake ambazo nawaamuru leo, ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu na watoto wenu baada yenu, na kwamba muweze kuongeza siku zenu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu amewapa milele.” 41 Kisha Musa alichagua miji mitatu mashariki mwa Yordani, 42 ili kwamba yoyote aweze kukimbia kati ya moja yao kama imemuua mtu mwingine kwa ajili, pasipo kuwa adui hapo awali. Kwa kukimbilia kwenye moja ya miji hii, atakuwa amenusurika. 43 Walikuwa: Bezeri katika jangwa, nchi tambarare, kwa Warubenites; Ramothi huko Gileadi, kwa Gadites; na Golani huko Bashani, kwa Manassites. 44 Hii ni sheria ambayo Musa aliweka mbele ya watu wa Israeli, 45 hizi ni amri za agano, sheria, na amri zingine alizungumza na watu wa Israeli wakati walipotoka Misri, 46 pindi walikuwa Mashariki mwa Yordani, katika bonde mkabala wa Beth Peori, katika nchi ya Sihoni, mfalme wa Amorites, aliyewahi kuishi Heshbon, ambaye Musa na watu wa Israeli waliwahi kumshinda wakati walipotoka Misri. 47 Walichukua nchi yake kama urithi, na nchi ya Ogi mfalme wa Bashani- hawa, wafalme wawili wa Amorites, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani kuelekea Mashariki. 48 Himaya hii ilienda kutoka Aroer, katika ukingo wa bonde la Arnon, kwa mlima wa Sion (mlima Hermon), 49 na ilijumuisha tambarare zote za bonde la mto Yordani, Mashariki mwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kuelekea bahari ya Arabah, kuelekea miteremko ya mlima Pisgah.

< Torati 4 >